Mkuu unatuvunja mbavu 😀😀😀😀
Hoja kubwa ya wanaomtetea Mourinho wanasema "Hajapewa Wachezaji Anaowataka" Sasa Najiuliza Ikiwa Klopp Kaweza Kumtumia mbilikimko XHAQIRI na ROBERTSON asiyejuilikana hata Background yake alitokea wapi ni mchezaji just from nowhere, Je ni Kweli Moutinho ndiyo Kashindwa Kuwatumia Pogba n Martial?
Au Mourinho anataka kuwaaminisha Watu Kuwa Xhaqiri ni bora kuliko Pogba, Martial na Mata?
Vile ni Visingizio tu kuwa Hakupewa Wachezaji anaowataka lakini kwanza angeliwagumia hao alionao.
Hivi ni kweli Mido ya GIN-HENDERSON-MILNER ni bora kuliko ya HERRERA-POGBA-MATA?
Sasa kwanini ya Kina Milner inadeliver lakini Mou kashindwa kuifanya ya kina Pogba kudeliver?
Hapo ni wazi kuwa tatizo si wachezaji bali ni kocha kutokuwa na mbinu za kisasa na kutokuwa na uwezo wa kucontrol dressing room kwani hata kama angepewa Messi na Ronaldo basi angeligombana nao tu.
Mkuu ukitumia akili kubwa sana kuongea baadhi ya mambo utachoka na kujitafutia maradhi ya moyo.
Shabiki makini yoyote Wa Manchester. Ambae walau amejitahidi kutumia kichwa chake kufikiri na si kunyolea VIDUKU. Lazima awe na hicho ulichoandika hapo juu. Bahati nzuri humu tumeshawahi kutifuana kuhusu hilo la wachezaji na niliishia kusema "CHINI YA MOURINHO KILA MCHEZAJI ATAONEKANA MBOVU"
Haikuchukua hata miezi mawili Mickytaryan moja ya wachezaji bora akapelekwa Arsenal. Paul Pogba alifuatia. Rojo alimanusura auzwe last transfer window. Hivi kweli hii scenario yote ni ubovu wa wachezaji?????.
Pumbavu zake mpaka linaondoka shetani hili lilikuwa limeanza kumpiga kama si kumchomesha mahindi Antonio Valencia moja ya wachezaji ninaowahusudu pale united kutokana na utiririkaji wake ule upande wa kulia Mwa kiwanja chochote pale kwa malkia .. Masikini ya mungu Valencia kwenye international break match almanusura nitokwe na machozi alipohojiwa kwao kwanini hachezi na wakati hana injury. Kijana huyu asiekuwa na makuu na mtu zaidi ya kuchomekea shati na kuupiga mpira kisawa sawa alijibu " Naamini mwalimu anajua uwezo wetu, naheshimu maamuzi na uwezo wa wachezaji wenzangu wanaopangwa"
Hiyo kauli iliniuma sana na kama si kuwa ninaishi huku uswekeni maramba mawili , kama ningekuwa pale jiji la Manchester ningekuwa nimefanya kitu cha ajabu sana kwa Mou pale viunga ama viwanja vya mazoezi vya AON COMPLEX.
Kuna mambo hayahiji ROCKET SCIENCE kujua nini tatizo. Kama mtu nchi hii ameshindwa kujua kama si kuoambanua tatizo la team ya Manchester Mchawi namba moja alikuwa huyo mmakonde kutoka ile nchi wanayokula kama si kubugia PANYA (Msumbiji). Basi taifa hili kuendelea ni mpaka yatokee maafa makubwa kama ya kipindi cha nuhu ili vichwa maji wote wasagwe na ije generation mpya yenye new Mentality. Jokes
Hahahahaha
Muhudumu Sogeza ni kwa hisani ya
Mou Faya , Mou Energy, Mou Pesa , Mourinho.