Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hii timu kuna kazi kubwa sana ya kufanya, nadhani City walikuwa wanatuonyesha ni jinsi gani tunatakiwa kucheza. Wanajua kujipanga,wanafungua nafasi,yani mimi sijui José anafundisha nini hawa wachezaji wetu,sijui!
Mkuu nimecheka sana yani kwa kuumia...Mara nyingi mno najiuliza mazoezini Kocha anawaelekeza wachezaji nini..... Au anawafundisha kuzuia tu maana hatuna uwezo wowote wa kuucheza mpira tunategemea bahati tu
 
Mkuu nimecheka sana yani kwa kuumia...Mara nyingi mno najiuliza mazoezini Kocha anawaelekeza wachezaji nini..... Au anawafundisha kuzuia tu maana hatuna uwezo wowote wa kuucheza mpira tunategemea bahati tu
Yani timu imekuwa ya kushinda kibahati bahati,hamna kinachoeleweka.

Ukiwatazama City unaona kabisa hata wakiokoa mpira wanajipanga haraka wanafungua nafasi unakuta kila mchezaji yupo tayari kupokea mpir,njoo sasa kwenye timu yetu.

Lakini pia wao kila mchezaji ni hatari,sisi kwetu Matic anaonesha kushuka kiwango lakini ukitazama bench hamna kitu.

José akiendelea kuwa kocha pale utashangaa hadi Fred anaonekana garasa.
José hadi sasa naamini sio kochamzuri na hili sitaki kumlazimisha mtu kukubali.


Fikiria mtu kama Martial ambaye José amemchelewesha sana angekuwa chini ya Pep angekuwa vipi leo?
 
Tangu siku inaanza nilikuwa sina amani kwa kuamini leo tutadhalilishwa na vijana wa pep,nikajiaminisha kuwa vyovyote matokeo yatakavyokuwa nitaridhika kutokana na tofauti ya ubora wetu na city. Lakini baada ya matokeo nimeumia zaidi kwa kutambua kuwa bado tuna safari ndefu sana kufikia kuchukua ubingwa wa ligi kuu achilia mbali kucheza fainali ya ligi ya mabingwa.

Matokeo hayajanihuzunisha sana kama ambavyo tumekuwa wanyonge mbele ya city ukizingatia uwekezaji wetu na wao hatukupaswa kuwa na tofauti kubwa sana aidha kiuchezaji au mtizamo tunaoingia nao dimbani. Ni dhahiri tangu upangaji wa vikosi vilivyoanza mou hakutegemea pointi 3 kwa city bali alihitaji droo kwanza na point 3 zije kama ziada flani hivi. Angalia mid field yetu ilivyokuwa nzito kutembeza mipira kwenda mbele. Kwa mechi tatu zilizopita tumeshuhudia umuhimu wa mata katika kuichangamsha timu kwa mipira ya kwenda mbele,lakini hofu ya mou imemzidi akamweka huyu mtu nje hadi pale alipoona yuko nyuma kimatokeo.

Kama ambavyo wengi tumeona na kuamini kuwa kukosekana kwa pogba kumechangia matokeo mabaya lakini binafsi sikubaliani na sababu hiyo kwa asilimia nyingi sana. Pogba anakuwa mzuri timu inaposhambulia Ila kwa mpira wa city unahitaji kiungo anayeshambulia na kukaba kwa haraka,na sio pogba anayejivuta vile. Kwa mawazo yangu ili kukabiliana na city yenye wachezaji wanyumbulifu tulihitaji viungo ambao ni attack minded ili kuwatia hofu city wasije wengi langoni kwetu hasa beki zao. Angalia long range alizokuwa anafanya fernandinho kisa tu hakuna mtu wa kumbughudhi. Kama mou alikuwa ni wa kujifunza,Wolverhampton walituonyesha jinsi ya kucheza na city,kupishana. Najua hapa watu watasema hatuna wachezaji wenye ubora wa kupishana na city,he wolves wana kikosi kizuri kuliko united?


Kwa game ya leo,city ni bora kwa mchezaji mmoja mmoja na kimbinu pia walituzidi. Mbali na martial sijaona mchezaji yeyote wa united ambaye anaweza walau kumtoka beki mmoja wa city wakiwa 1x1 ila city wanawatoka wachezaji wa united kirahisi sana. Leo hii no aibu na dhihaka kubwa sana kumuona Felipe Anderson anaichezea westham,Madison anaichezea Leicester, Richarlson anakipoga Everton, wakati sisi tuna lingaard kama namba 10 wetu. Tuna shida katika soko la usajili kama ambavyo mkuu Damushin amekuwa akidai. Saa nyingine huwa najiuliza mou huwa anawafundisha nini hawa wachezaji wetu pale carrington maana mbinu yetu kubwa ya magoli imekuwa ni mipira iliyokufa zaidi. Set up ya mashambulizi imekuwa ni dhaifu mno tena ni hadi adui atuchokoze. Kwa sasa pale EPL hakuna timu tunayoizidi kucheza mpira mzuri kati ya timu zote 19 maana hata Leicester wanaugusa mwingi kuliko sisi.

Nimalizie kwa kusema kwamba kwa mwenendo huu mwakani tujiandae kucheza Europa ligi na nangojea kukutana na akina BATE Borisov ,spartak Moscow na wenzake.
Mniwie radhi wakuu maana nimeandika kwa hasira kidogo maana sioni tumaini kwa hii timu kufikia hapa.
GGMU
 
Mkuu Radika........... Manchester United malengo yenu msimu huu ni nini timu mechi 11 ina -1
Daaaa hapa mkuu mwenyewe nashangaa kwamba mourinho anafanya kusudi kumkomoa ed woordward au anatafuta sababu afukuzwe bek wale wale msumu uliopita walicheza vizur na kuruhusu goli chache msimu imekimuwaje? Rojo na bailly wapo nje valencia hachez hapa kuna kitu pia toka kwa kocha
 
Jose ni tatizo kubwa kuliko tunavyofikiri.
Wachezaji nao viwango vidogo kulinganisha na City. Wanaonekana hawana nguvu, pace, hawawezi kukaba. Angalia Young alivyokuwa hawezi kukaba zaidi ya kuwaita adui kwenye box.

Vichezaji vyetu havijiamini hata hivyo. Anapoteza mpira, anamwacha adui aliyempokonya, anakimbilia kwenye box
 
Wachezaji nao viwango vidogo kulinganisha na City. Wanaonekana hawana nguvu, pace, hawawezi kukaba. Angalia Young alivyokuwa hawezi kukaba zaidi ya kuwaita adui kwenye box.

Vichezaji vyetu havijiamini hata hivyo. Anapoteza mpira, anamwacha adui aliyempokonya, anakimbilia kwenye box
Herrera nae alikatika muda sana pale kati, kutojiamini lilikuwa tatizo kubwa.
 
Daaaah umenikumbusha hiki kimeo mkuu, MOUH japo ana wakat mgumu na hiki kikosi ila alikosa au kwa makusudi aligoma kupanga vizur kikosi.
Mi naona alileta masihara tu hamna namna sasa lingard kwa ile mech umeache bench mata na fred aisee nani anakuwa kiungo mbunifu? Herrera,fellain na matic walikuwepo katikati yani nilipoona hicho kikosi hata sikuelewa kitu
 
Mi naona alileta masihara tu hamna namna sasa lingard kwa ile mech umeache bench mata na fred aisee nani anakuwa kiungo mbunifu? Herrera,fellain na matic walikuwepo katikati yani nilipoona hicho kikosi hata sikuelewa kitu
Kweli ni masikhara, kwa kile kikosi hakukuwa na mbunifu bora Martial alijuwa anajaribu kuwatoka mabeki japo mipira ilikuwa inaishia miguun mwao.
 
Kweli ni masikhara, kwa kile kikosi hakukuwa na mbunifu bora Martial alijuwa anajaribu kuwatoka mabeki japo mipira ilikuwa inaishia miguun mwao.
Nlikuwa naona kwa kuwa pogba hayupo basi fred alitakiwa kuwepo uwanjani sasa sijui kamnunua wa nini na kwa hela ndefu kama ile halafu anakaa bench fred akicheza juu huwa namuona anafanya vizur
 
Back
Top Bottom