Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Football is teamwork sports unlike boxing or golf. Only Messi & CR7 ndio wanaweza kufanya hicho unachotaka Lukaku akifanye

Sio lazima Lukaku ndio aipe ushindi kila mechi angalia Man City wana wachezaji wafungaji zaidi ya 7 (Aguero,Jesus,Sane,Sterling,Fernandinho,Otamendi,KDB,Silva).Hata enzi za SAF kuna game kina Fletcher,Oshea,Macheda,Keane ndio wanaipa ushindi timu

Angalia contribution ya defenders wa Chelsea kwenye magoli misimu ambayo wamechukua ubingwa
 
Sijakataa ila nazani utakumbuka mara ngapi pia Rooney,Van nistelrooy, etc walitutoa kwenye mechi pale mambo yalipokuwa hayaendi mie napenda Lukaku awe striker tishio.
 
ha ha mkuu wengine tunainjoi kuona mapicha picha yasio na maelezo toka kwa fildi masho RUTTA
 
 
Unajua watu wanamuonea wivu ruta. Sidhan kama mapicha ni hoja. Ruta ana likes nyingi, hapo ndio wivu ulipo. Mambo ya kijinga
Mkuu sio wivu kwa hiyo tumuonee wivu Ruta kwa ajili ya likes anazopata kweli...????
Shida yetu kwake anaijua ndo maana kila mtu anaiongelea na wala sio hizo likes unazosema wewe.
 
Jukwaa limevamiwa na watoto ambao wanataka waone man utd inacheza na kila timu kama ilivyocheza na everton au west ham. Lukaku msimu huu kahusika na magoli kumi.
Mechi iliopita ndio kapiga cross Rashford akafunga,jana katoa assist Martial kamalizia.
Nafasi nzuri aliopata kagongesha mwamba. Half chance ingine kipa kaokoa sijui wanaosema Lukaku mbovu wanatumia vigezo gani?
Wengine wanasema tumu imepaki bus ukiangalia stats wanachoongea hakina ukweli wowote, ila wanataka timu icheze na timu kubwa kama inavyocheza na west ham hivi.
Liverpool wanajidai wanajua kushambulia wamepigwa 4-1 na spurs, 5-1 na city je mnapenda man utd wajiachie wapigwe 5?!
Mechi ambazo Mou atapaki bus iliobaki ni moja tu vs man city away. Lakini vs chelsea tunaenda nao mguu kwa mguu, arrsenal tunaenda nao mguu kwa mguu.
Kila mechi ina uxito tofauti na approach tofauti.
 
lukaku ndio analead attack hivyo ni lazima mfumo umfaidishe yeye hilo sio jambo la ajabu,

na pia kina martial wanafaidika, sababu angekuwa striker ni Ibra ambae hana movement wote wangekuwa ni ovyo kama msimu uliopita, stats zao za msimu huu ni way better kuliko msimu uliopita.

mkuu bado naendelea kutolea mfano goli la jana, angalia lukaku wakati anatoa ile pasi anakabwa na nani na nani, kuna wachezaji kama watatu hapa, wawili ninao waona vizuri ni Aurrier na huyu namba 4 yaani Toby Alderweireld, hivyo tayari kisiki kimoja lukaku amekivuta nje ya box sababu ya movement zake then alivyotoa pasi martial alibaki na Vertonghen tu, huu ndo msaada wa lukaku kwa kina martial na Rashford.

Na watu walisema Lukaku Ataflop mechi kubwa mpaka sasa ameshacheza mechi 3
-amewafunga madrid
-ya liverpool hakufunga
-assist ya spurs.

pia wakasema ataflop UEFA mpaka sasa ana goli 3 mechi 3

Naona Online wengi wanaandika stats za kupika za Lukaku against top teams.
 
Pep na Wenger wanatumia possession based approach. Attacking/pressing ni approach ya Poche na Klop.

Hata hivyo falsafa km hizi huwa ni za vilabu, kocha hupaswa kufit humo.

United toka hata enzi za Fergie, tupo kati, pressing na defensive. Rejea mechi ya Uefa tuliyocheza fainali Urusi dhidi ya Chelsea, possession ilikuwa 75/25

Kuna Mechi ya Uefa pia tuliwahi kumfunga Barca kimoja, akiwa na possession ya 79/21.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…