Mambo Mengi muda mchache, kijana aende wapi kati ya diploma ya CLINICAL MEDICINE NA PHARMACY

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,039
2,000
Mwambie aende Clinical Medicine, coz clinical medicine kwa uelewa wangu anaweza fanya pharmacy pia ila pharmacy hawezi kazi za clinical medicine
Perfect, very high reasoning. asante sana. All is done and I close the deal. (Nadhani limanisha kuwa Pharmacy hawezi kufanya MD)

TCU guide sijui inasemaje, nimesoma hawajaweka wazi kama pharmacy diploma anaweza kusoma MD ila wamesema related health courses kwenda kusoma degree za health.
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
415
500
Njia panda! Nisaidieni aende wapi , with reason.
Vyote ni vyuo vya serikali amechaguliwa.

Swala la msingi ni kuelewa mhusika ana wito wa kuhudumia jamii kupitia mlengo upi?

Atakachokichagua akifanye kwa uaminifu na uhakika kitamfaa maishani na kwa jamii.

Mfamasia bado anaweza kusoma na kwenda juu zaidi ya tunavyofikiria ndani ya mkondo huohuo kama ilivyo kwa daktari.

Wote wana nafasi sawa kwenye maisha, suala ni kwa jinsi gani unatumia elimu uliyoipata.

Ndani ya makundi yote:
1: Kuna madaktari waliofanikiwa na elimu yao si kubwa, kuna waliofanikiwa wakiwa na elimu kubwa na kunawalioshindwa kufanikiwa wakiwa na elimu kubwa.

2: Kuna wafamasia wamefanikiwa na elimu yao si kubwa, kuna waliofanikiwa wakiwa elimu kubwa na kuna wasiofanikiwa na elimu kubwa wanayo.

Msikilize wito wake na upime, pia umuandae kuitumia vyema elimu atakayoipata.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,820
2,000
Naskia ukisoma clinical medicine ukitaka degree unachagua wewe tu uende wapiiii.

Ila ukisoma kozi zingine zisizokuwa CLINICAL MEDICINE degree unaenda kozi hiyo hiyo,sijui hili limekaaje ?
 
zink

JF-Expert Member
Sep 18, 2021
717
1,000
Naskia ukisoma clinical medicine ukitaka degree unachagua wewe tu uende wapiiii.

Ila ukisoma kozi zingine zisizokuwa CLINICAL MEDICINE degree unaenda kozi hiyo hiyo,sijui hili limekaaje ?
Nahisi kwa kuwa clinical medicine wanasoma mambo mengi maana nasikia watu wa C.O wanasoma vitu vya pharmacy, laboratory pamoja na nurse
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,968
2,000
Njia panda! Nisaidieni aende wapi , with reason.
Vyote ni vyuo vya serikali amechaguliwa.
Kipi hukijui? Hivi unapopanga kwenda hospitali unaenda kumuona Pharmacist au Mganga? Je, kuna kituo cha Afya ambacho mkuu wake ni Pharmacist? Je wajua kuwa Pharmacist kazi yake ni kugawa au kuuza dawa iliyoandikwa na Mganga? Mpaka hapo hujaona kuwa Pharmacist ni mtumishi wa Mganga? Mpeleke akasome Clinical Medicine iwapo ana angalau D ya Physics
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,820
2,000
Kipi hukijui? Hivi unapopanga kwenda hospitali unaenda kumuona Pharmacist au Mganga? Je, kuna kituo cha Afya ambacho mkuu wake ni Pharmacist? Je wajua kuwa Pharmacist kazi yake ni kugawa au kuuza dawa iliyoandikwa na Mganga? Mpaka hapo hujaona kuwa Pharmacist ni mtumishi wa Mganga? Mpeleke akasome Clinical Medicine iwapo ana angalau D ya Physics
Ndio maana famasi imekuwa haithaminiki kwa sababu imeonekana kama kazi yao kugawa dawa ambazo daktari ndio ameandika.

Hivyo uhitaji unakuwa sio mkubwa,lakini mfamasia kwenye nchi za wenzetu ni mtu ambaye anaheshimika sana
 
Tupo nchi hizi. Ukienda Roma fanya kama waroma
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
13,662
2,000
Ndio maana famasi imekuwa haithaminiki kwa sababu imeonekana kama kazi yao kugawa dawa ambazo daktari ndio ameandika.

Hivyo uhitaji unakuwa sio mkubwa,lakini mfamasia kwenye nchi za wenzetu ni mtu ambaye anaheshimika sana
Kwani famasi inatofauti gani na mangi muuza duka...maana ye anakuwa amesomea bidhaa(dawa)... kutengenezea hatengenezi yeye
 
Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
1,125
2,000
Kipi hukijui? Hivi unapopanga kwenda hospitali unaenda kumuona Pharmacist au Mganga? Je, kuna kituo cha Afya ambacho mkuu wake ni Pharmacist? Je wajua kuwa Pharmacist kazi yake ni kugawa au kuuza dawa iliyoandikwa na Mganga? Mpaka hapo hujaona kuwa Pharmacist ni mtumishi wa Mganga? Mpeleke akasome Clinical Medicine iwapo ana angalau D ya Physics
Ni mgawanyo wa kazi. Daktari naye haruhusiwi kugawa dawa, kuuza wala kufungua duka. Na ripoti zinaonyesha kuwa watu wengi wakiumwa, mtu wa kwanza kumuona ni mfamasia dukani.
 
Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
1,125
2,000
Kwani famasi inatofauti gani na mangi muuza duka...maana ye anakuwa amesomea bidhaa(dawa)... kutengenezea hatengenezi yeye
Vitu vikubwa ambavyo wafamasia wanasoma ni:

1. Jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini.
2. Jinsi ya kutengeneza dawa.

Hiyo ya kutoa dozi ni kitu kidogo sana, kinasomwa semester moja tu.
 
Expected Value

JF-Expert Member
Mar 29, 2016
1,419
2,000
Vitu vikubwa ambavyo wafamasia wanasoma ni:

1. Jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini.
2. Jinsi ya kutengeneza dawa.

Hiyo ya kutoa dozi ni kitu kidogo sana, kinasomwa semester moja tu.
Samahani mkuu hivi hapo namba 1 Daktari hajajifunza hivyo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom