Mambo Mengi muda mchache, kijana aende wapi kati ya diploma ya CLINICAL MEDICINE NA PHARMACY

Naskia ukisoma clinical medicine ukitaka degree unachagua wewe tu uende wapiiii.

Ila ukisoma kozi zingine zisizokuwa CLINICAL MEDICINE degree unaenda kozi hiyo hiyo,sijui hili limekaaje ?

Big NO...!
Ukisoma clinical medicine,huwezikusoma degree ya pharmacy kwa Tanzania never......ila utasoma MD,clinical nutrition,health information system,health system mx ,,,,,na ukisoma diploma ya pharmacy huwez soma MD degree......according to TCU guide 2021/2022.
 
Ushauri wangu kwa kijana....!
Kama anatamani kuwa daktari (MD),mpeleke private’s ili apate gpa asonge zake mbele,,,hata hio pharmac pia kama anataka aje kupiga barchelor ya pharmac mpeleke private’s...
kama uwezo wa private’s haupo mwambie akasome sana na kuwa karibu na tutors
*shukran
 
Naskia ukisoma clinical medicine ukitaka degree unachagua wewe tu uende wapiiii.

Ila ukisoma kozi zingine zisizokuwa CLINICAL MEDICINE degree unaenda kozi hiyo hiyo,sijui hili limekaaje ?
Aisee hivi watu huwa mnapata wapi ujasiri wa kuandika vitu vya uongo na ambavyo hamvielewi si bora uulize kwanza.......inasikitisha sana.

Hakuna CO anayeruhusiwa kusoma BScLAB,pharmacy wala bsc nursing.
 
Mkuu kuwa muelewa basi nimeshasema hapo kwenye comment yangu kuwa "sijui hili lomekaaje" kwa maana sijajua uhakika wake na mimi nasikia tu..

Unakuja kunituhumu kwa uongo inakuwaje mkuu
 
MD na Pharmacy, Hii vita si ya nchii ,

Pharmacy wanaichukulia poa sana, tena naona na sababu zinazotolewa hata hazina mashiko ukiwa field Mfano kama Madaktari wanasoma mambo mengi sjjui nini, mara mwingine mfamasia anajua kutoa dawa tu!

anyway bora muendelee ku'diverge huko huko ila wafamasia wasiwe wengi kivile waendelee kupiga hela zao kimya kimya!

wanasahau kuna mambo mengi ya pembeni yanaendelea ya maana si lazima kuyaweka wazi hapa, Trust me hamjaingia uwanjani kuujua mchezo, ila ukishaingia uwanjani ni kama Asali huwezi toka na kusema otherwise.

anyway kwa kuwa mdogo wako anasomea kwa level diploma hiyo CO kila la heri yake, ila kama angekuwa mdg wang na anafikiria kuendelea mbele ningemshauri vinginevyo na mipango yenu!
 
Nahisi kwa kuwa clinical medicine wanasoma mambo mengi maana nasikia watu wa C.O wanasoma vitu vya pharmacy, laboratory pamoja na nurse

Sio kwamba CO wanasoma hayo mambo ya pharmacy,lab na nurse in deeep.....”NO” wanasoma basics tuuu tena shallow saaanaaaaa
 
Vigezo vya MD uwe na C.O tena GPA ianzie 3 ila mkuu kuna wenye hasi 4+ na wanasugua gaga kupata MD kiufupi now MD ni kisanga kupata..

Kama lengo kujiajiri na kupara digrii kiurahisi mpeleke Dental,Radiology japo atadili na meno na tiba za picha tu ila kuna hela hapo..na bado wanahitajika sana hao watu japo C.O ni mkubwa kuliko hao kwa level yake ila now C.O kama ualimu tu mkuu.
Perfect, very high reasoning. asante sana. All is done and I close the deal. (Nadhani limanisha kuwa Pharmacy hawezi kufanya MD)

TCU guide sijui inasemaje, nimesoma hawajaweka wazi kama pharmacy diploma anaweza kusoma MD ila wamesema related health courses kwenda kusoma degree za health.
 
Hakuna kitu kama hicho now ukisoma C.Medicine huwezi kusoma Dental,Radiology wala pharmacy kwa level ya digrii wewe ni MD na Nesi nadhani kiufupi now ni kugumu sio kama nyuma.
Naskia ukisoma clinical medicine ukitaka degree unachagua wewe tu uende wapiiii.

Ila ukisoma kozi zingine zisizokuwa CLINICAL MEDICINE degree unaenda kozi hiyo hiyo,sijui hili limekaaje ?
 
Mkuu hiyo GPA anaweza pata ila Private na akaze hasa na baso pia kamari kupata chuo cha serikali kama huna hela ya private mtoto ataishia hapo
lengo ni kwenda MD, kama huwezi pata GPA ya kuweza kwenda MD over 4.5, preferably 4.7), nimemwambia bora aache atafute mambo mengine
 
Mkuu Pharmacy usiidharau hata kidogo kwa mtu mwenye vision bonge la kozi hiyo...
Kipi hukijui? Hivi unapopanga kwenda hospitali unaenda kumuona Pharmacist au Mganga? Je, kuna kituo cha Afya ambacho mkuu wake ni Pharmacist? Je wajua kuwa Pharmacist kazi yake ni kugawa au kuuza dawa iliyoandikwa na Mganga? Mpaka hapo hujaona kuwa Pharmacist ni mtumishi wa Mganga? Mpeleke akasome Clinical Medicine iwapo ana angalau D ya Physics
 
Hakuna kitu kama hicho now ukisoma C.Medicine huwezi kusoma Dental,Radiology wala pharmacy kwa level ya digrii wewe ni MD na Nesi nadhani kiufupi now ni kugumu sio kama nyuma.

Hata nesi husomi,ukikosa MD utaishia kozi za uongozi ,informations na lishe tuu
 
Back
Top Bottom