Habari ndugu wasomaji,
Naandika UZI huu ili tu kujaribu kushaire kile ninachokifahamu.
Maarifa haya yanatokana na uzoefu wangu na dhana kutoka katika hekima ya vitabu kadhaa ikiwemo pia kutoka kwenye mitazamo ya watu makini kwenye Tasnia husika.
Mada ni QNET as E-commerce;
Ningependa kulist ecommerce platforms maarufu mfano, EBAY, ALIBABA, AMAZON hiyo ni mifano ya ecommerce platforms ambapo mtu anaweza nunua bidhaa yeyote akiwa popote duniani. Dunia imekua kijiji bidhaa yoyote iliyopo popote inaweza nunuliwa na yeyote aliyepo popote duniani na akaipata. Platforms hizi zimeundwa kwa utaalamu mkubwa na hivyo kutoruhusu mianya yeyote ya wizi au ulaghai kati ya wanunuzi na wasambazaji. Ukiwa unatumia mifumo hii kununua bidhaa basi hatua zote za ununuzi hufanywa ndani ya hiyo mifumo hatua kwa hatua.
Hizi ecommerce platforms nyingi zilizopo zimeundwa ili kukutanisha wanunuzi na wasambazaji. Waasisi wa mifumo hii (hiyo niliyoitolea mfano) huwa hawana bidhaa yeyote mule bali bidhaa zote zilizomo mule ni za wasambazaji husika.
Lakini pia zipo E commerce platforms zingine ambazo ni kwa ajili ya bidhaa za kampuni fulani tu ambapo wanunuzi wake huitumia ili kununua bidhaa hizo.
E commerce platforms imepelekea watu kupata wateja kirahisi na katika wingi usio na kikomo lakini pia imepelekea wanunuzi kuwa na uwezo wa kupata wigo mkubwa wa uchaguzi wa bidhaa watakazo kutoka mahali popote duniani.
Wajasiriamali wa kileo wamerahisishiwa sana kazi zao kutokana na uwepo wa mifumo ya aina hii.
Qnet ni E commerce sytem ambayo ipo kwa ajili ya bidhaa za kampuni fulani tu (bidhaa za QI company), ni ofauti na platforms zingine ambazo wajasiriamali huweka bidhaa zao humo ili kupata wanunuzi, kwenye QNET huwezi ku upload bidhaa yako.
Kwa kipekee kabisa E commerce platform ya QNET, bidhaa za mule zote huwa zinauzwa na wasambazaji wao tu. Hapa inamaana kampuni ya QNET imetoa haki ya umiliki wa online shop yake kwa 100% kwa wasambazaji wake waliothibitishwa ( IR).
Hii imekaa vipi... ni hivi;
Online shop ni moja dunia nzima ambapo bidhaa hubadilika kutokana na nchi aliyopo mnunuzi.. Lakini kila mnunuzi akiwa anafuata hatua za ununuzi online basi hutakiwa kuweka special Id Number ya IR aliyempa taarifa ya bidhaa za qnet ili afanikiwe kununua la sivyo hatoweza kununua.
Na hawa IRs hulipwa commision zao kupitia online acconts zao mara tu mauzo yakikamilika.
Hivyo QNETni E commerce platform pekee ambayo wajasiriamali wanahaki ya kuuza bidhaa zilizomo dukani na ilihali si zao.
Yaani ni kwamba Mjasiriamali yeyote anaweza kumilikishwa E commerce system with full of products ambapo at any time product inauzika anakuwa akipata faida ya mauzo yale.
Kwa leo nililenga eneo hili tu..
Till next time..
Thanks.