Daa huu uzi umenisaidia sana. Mm jamaa yangu aliita ktk style zote ambazo nimezisoma humu na nikafika nikasalimiwa good morning wakati ilikuwa saa 11 jioni ila nikavumulia tuu. Nikaingia kwenye mafunzo ya awali ila nilitoka sijaelewa kitu na nikaahidiwa nitaelewa vizur kwenye mafunzo ya pili. Kwasababu mm huwa ni mwoga sana wa michezo ya upatu, pia nikawa bize na kazi zangu nikawa sijahudhuria mafunzo ya awamu ya pili ila jamaa ana push sana niende, hata wiki mbili zilizopita alinialika kuwa kuna maonesho ya bidhaa ofcn kwao, nilitamani kuhudhuria ila ratiba ikanibana nikashindwa. Hv bado nilikuwa na nia ya kwenda kupata mafunzo ya awamu ya pili ila sikujua kama kuna kiingilio kama hicho. Huyu jamaa keshanikosa maana biashara ya upatu sifanyi.