mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Tunaomba serikali na hasa Wizara ya Elimu na ike ya Tamisemi waliangalie sana hili na kulitolea muongozo mapema.
Malalamiko yenyewe ni kwamba kumekuwa na utaratibu kwa shule za binafsi hasa zile za English Medium kuzuia wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwenda likizo hasa ya mwezi wa sita.
Inajulikana kwamba utaratibu wa likizo upo duniani kote kwa binadamu wote wanaofanya kazi wakiwepo wanafunzi. Na hili linafanyika baada tafiti kuonesha kwamba binadamu hawawezi kufanya kazi mfululizo bila kupumzika kwani hilo linaadhiri ufanisi wao katika kazi.
Sasa inashangaza kuona shule hizi za msingi za binafsi zinawanyima wanafunzi wa darasa la nne na la sita kwenda mapumziko ya mwezi mmoja eti kisa wanawaandaa kwa mitihani ijayo.
Hawa ni watoto wadogo, wanasoma mfulilizo bila kupumzika kisa mitihani kweli hili ni sawa? Kaka na dada zao wa Form Two na Form Four wana mitihani mwishoni mwa mwaka huu lakini wapo likizo. Sasa iweje hawa wa form two na darasa la sita? Ni nini hasa so special kwa hawa wanafunzi wa English Medium schools.
Je, ni kweli kwamba muda uliopo hautoshi kuwaandaa hawa watoto kufanya vizuri kwenye mitihani yao?
Hao watalaam wa elimu na wanasaikolojia waliopendekeza utaratibu huo na ukakubalika pengi walikosea?
Isitoshe, kwa sasa kuna waraka wa serikali unaokataza shule za serikali kutofunga shule au kuongeza muda wa masomo kwa wanafunzi bila ruhusa ya mkurugenzi/serikali. Tena yamewekwa masharti na mambo ya kuzingatia kama shule itataka kutumia muda wa mapumziko wa wanafunzi kufundisha.
Je, Shule hizi za private hazifungwi na taratibu na secular hizo za serikali? Wanaruhusiwa kufanya mambo wanavyoona tu wao? Kiholela.
Tunaomba serikali na bunge waliangalie hili na liwekewe utaratibu mzuri kwa sababu linaleta usumbufu mkubwa kwa wazazi na kunyima haki ya watoto kupumzika "from daily routines za shule!"