DOKEZO Mtendaji Kata ya Malindi anakodisha eneo la shule kwa maslahi binafsi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Afisa mtendaji wa kata ya Malindi, iliyoko tarafa ya Mlalo, wilaya ya Lushoto - Tanga, amechukua maeneo makubwa ya shule ya sekondari Mtumbi na kuyakodisha kwa watu mbalimbali kwa manufaa binafsi. Maeneo mengine machache amewapa walimu wa shule hiyo ili wasimuulize juu ya eneo la shule analohodhi. Mtu huyu ni jeuri haswa kutokana na kupata sapoti kutoka kwa diwani wa kata ya Malindi na viongozi wengine wa CCM. Mkurugenzi wa Lushoto tumempelekea malalamiko mara nyingi na hili analijua ila amelifumbia macho.

Tunamuomba katibu mkuu OR - TAMISEMI angilie kati ili eneo hili litumike na wanafunzi kwa shughuli za kilimo zitakazowasaidia kuwapatia chakula shuleni na kuwafunza stadi za maisha ili waweze kujitegemea watakapohitimu masomo yao. Pia OR - TAMISEMI ilete wataalamu waje kupima eneo lote la shule na kuweka alama za kudumu kwani wanakijiji wanakata miti ya mpakani na kuingia eneo la shule jambo linalosababisha eneo la shule kuzidi kupungua.

Kwa kuwa viongozi wa CCM wana nguvu kubwa kimaamuzi katika eneo hili na maeneo mengi ya Lushoto, wanachama wa ccm wamepewa eneo na wanalima ndani ya eneo la shule. Tuomba nao waondolewe ili wanafunzi walime eneo hili.

Mimi ni mzazi wa watoto wawili wanaosma shule ya sekondari Mtumbi pamoja na wazazi wengine tunaomba eneo hili lirudi shuleni kuzalisha chakula kwa ajili ya watoto wetu ili itupunguzie mzigo wa michango ya chakula shuleni.
 
Back
Top Bottom