Shule za English medium zisizo na remedial za lazima

mzeemzima

Senior Member
Apr 14, 2010
122
78
Wadau,

Moja kati ya kero yangu kubwa kwenye hizi english medium ni huu mfumo wa kulazimisha watoto wa Standard 4 na 7 kufanya remedial kwa lazima , hata pale ambapo hakuna ulazima huo. Najua shule zinafanya biashara lakini si kwa kuwapa watoto stress zisizo na lazima . Watoto mwaka mzima kuanzia asubuhi mpaka jioni kama sio usiku ni kukaririshwa tu bila kupewa elimu yoyote ya kuwajenga kwa stadi za maisha na skills zitakazowasaidia wao na maisha yao ya baadae.

Kwa sababu hiyo naomba kujuzwa kama kuna shule zozote ambazo hazina hii programu ya remedial kwa haya madarasa na hasa zile ambazo ziko wilaya ya kinondoni au ubungo.

Natanguliza shukrani
 
hadi st kayumba madarasa hayo wana remedial labda IST ndo
kunaweza kuwa hakuna
 
Kuna mdau humu alileta uzi akionesha matokeo ya mtoto wa max m wa jf huko feza,aalivyopiga 1.7
Nashangaa uzi umeondolewa mbali

Aise wapelekeni watoto wenu shule za maana

Ova
 
Nimegundua kuwa Feza primary iliyoko Kawe na Feza Shamsiye kule Mbweni zote hazina mambo ya remedial wala kulazimisha wazazi standard 4 & 7 kukaa boarding na shuleni wanatoka saa nane kasorobo mchana lakini wao ndio wanafaulu kwa viwango vya juu kuliko hizi shule za remedial zinazokaririsha watoto kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2 usiku. Hili ni somo tosha kuwa kukaririsha watoto masaa mengi sio kufaulu lakini mtoto akifundishwa vizuri masaa machache na akawa na muda wa kutosha wa kupumzika na kujifunza stadi na elimu nyingine za maisha anakuwa katika nafasi ya kufaulu vizuri hata katika academics.
 
wakuu , kuna yeyeote anejua shule zaidi ambazo zinafuata mtaala wa NECTA , na hazina mambo ya remedial kwa darasa la 4 na la 7? Tafadhali naomba kujuzwa. asante sana
 
Wadau,

Moja kati ya kero yangu kubwa kwenye hizi english medium ni huu mfumo wa kulazimisha watoto wa Standard 4 na 7 kufanya remedial kwa lazima , hata pale ambapo hakuna ulazima huo. Najua shule zinafanya biashara lakini si kwa kuwapa watoto stress zisizo na lazima . Watoto mwaka mzima kuanzia asubuhi mpaka jioni kama sio usiku ni kukaririshwa tu bila kupewa elimu yoyote ya kuwajenga kwa stadi za maisha na skills zitakazowasaidia wao na maisha yao ya baadae.

Kwa sababu hiyo naomba kujuzwa kama kuna shule zozote ambazo hazina hii programu ya remedial kwa haya madarasa na hasa zile ambazo ziko wilaya ya kinondoni au ubungo.

Natanguliza shukrani

wakuu , kuna yeyote anejua shule zaidi ambazo zinafuata mtaala wa NECTA , na hazina mambo ya remedial kwa darasa la 4 na la 7? Tafadhali naomba kujuzwa. asante sana
 
Back
Top Bottom