Nakuunga mkono kwa asilimia 100.Mfumo wetu wa Elimu unaangalia mtu aliyefaulu mtihani na si vinginevyo.Tena ufaulu wa A kwa wanafunzi wote.Hata mzazi anapotaka kupeleka mtoto shule haangalii shule inayotoa likizo yote kwa watoto bali inayofaulisha watoto wengi kwenye mitihani.Mkuu, utafiti unaonesha muda wa masaa nane hautoshi kuifikisha nchi kama Tanzania kwenye nchi ya asali na maziwa.
Tunahitaji sana kufanya kazi kwa muda zaidi ya huu wa sasa.
Turudi kwenye mada yako.
Kwanza jambo hili hujalifanyia utafiti wa kutosha, matokeo yake umeleta hoja ambayo kimsingi inachafua huduma nzima ya Elimu hasa kwa shule binafsi. Pengine na wewe unaweza kuwa unasadifu mapungufu ya mfumo wetu wa Elimu. (kwa kipindi fulani kama taifa tumekuwa na tabia ya kukurupuka. Watoa maoni tunakurupka, na viongozi wanakurupukia maoni, matokeo yake yanatolewa maamuzi mabaya ambayo hayana tija).
Huu utaratibu wa kuwabakiza watoto wa madarasa ya mitihani shuleni ni utaratibu ambao kwa miaka ya hivi karibuni unaratibiwa na mamlaka za elimu. Uratibu na utekelezaji wake hutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na malengo. Na kwa bahati nzuri au mbaya siku hizi shule zote za serikali na private zinalazimika kuwabakiza watoto wa madarasa ya nyakati za likizo kwa maelekezo ya viongozi. Na hata utoaji wa likizo kwa walimu wa serikali halmashauri unazingatia majukumu ya walimu wakati wa likizo. (Yaani walimu wengine wanapewa likizo mwezi June wengine wanapewa mwezi December) kwa hiyo baadhi ya Halmashauri walimu watakaobaki June watafundisha watoto darasa la saba na la nne. Wale watakaobaki Dec watafundisha darasa la sita na la tatu. Au baadhi ya Halmashauri katika mgawanyo wa vipindi shuleni wanazingatia mwaka huu usipofundisha darasa la mitihani mwaka kesho lazima upewe ili kubalance likizo. n.k n.k YAANI KWA KIFUPI SUALA LA ELIMU LIKO VERY COMPLICATED.
HOJA YAKO YA KUHUSU BINADAMU WANATAKIWA KUPUMZIKA.
Uzoefu wa huduma ya Elimu unaonesha kuwa mara nyingi watoto wanaporudi nyumbani bado wazazi wengi huwatafutia tuition. Kwa hiyo hata ile dhana ya KUPUMZIKA nayo inakosekana.
Pia Wataalam kule shuleni nako huwa wana mitazamo tofauti na tuition.
A. Shule nyingi huamini watoto wengi hujiingiza kwenye makundi yasiyofaa kupitia hizi tuition.
B. Wakati mwingine(mara nyingi kwa watoto wa shule za msingi), tuition pia huleta confusion kwa watoto kati ya kile kilichofundishwa shuleni na tuition. Walimu wetu wa tuition hawafanyi pre assessment kwa mtoto kabla ya kufundisha.
C. UONGOZI WA SHULE NA WALIMU NAO WANAZITAMANI HIZO HELA ZA TUITION 🤑🤑😋😋. KWA HIYO WANAAMUA KUBUNI MBWINU YA KIHALALI YA KUZIPATA HIZO SHEKELI😂😂😂.
MORE IMPORTANTLY UZOEFU UNAONESHA WATOTO WETU WANAPORUDI SHULENI BAADA YA LIKIZO WANAKUWA WAMESAHA. YAANI WALIMU WANAANZA UPYAAAA (Hili angalau linatatulika) 😁😁
KUHUSU UTEKELEZAJI WA MTAALA.
Hili ni suala ambalo wengi tunajitia kulijua ila hata hatujui Changamoto za utekelezaji wa mtaala.
Nimeona mdau mmoja hapo juu amesema walimu watumie muda vizuri😅😅. Ni rahisi kusema hivyo.
Mimi nataka nitoe mfano hai.
Mwaka wa masomo kwa shule za msingi una siku kati ya 192 hadi 197. Mwaka huu wa 2021 una siku 192.
Mihtasari ya masomo ya darasa la saba ina uzito sawa au kuzidi ile ya darasa la sita. LAKINI WAKATI MIHTASARI YA DARASA LA SITA IKIWA NA NAFASI YA KUTEKELEZWA KWA KWA SIKU 192-197 MIHTASARI YA DARASA LA SABA INATAKIWA KUTEKELEZWA KWA SIKU CHACHE ZAIDI KWA SABABU HUWA WANAHITIMU MWEZI WA TISA. (Hali hiyo ni kwa madarasa yote ya mitihani. Mitihani huwa inafanyika mapema).
MTOA MADA NIKUKUMBUSHE JAMBO:
Wakati wewe unalalamikia hilo, wazazi wengi ndio wanataka watoto waspend muda mwingi shuleni.
USHAURI WANGU KWA MTOA MADA.
Jitahidi kuhudhuria vikao vya wazazi ili utoe maoni yako, Pia usikilize hoja za uongozi wa shule yako. Kamati ya shule na Mkutano wa wazazi ndio chombo kikuu cha maamuzi ya uendedhaji wa shule. Kuhudhuria na kutoa maoni yako ndio njia sahihi ya kutatua na kujenga shule bora kwa watoto wetu. SHULE NI MALI YA WATOTO WETU AMBAO SISI NDIO WASIMAMIZI WAO.
PIA MTOA MADA USIWE MBINAFSI SANA. USIMHURUMIE MWANAO TU WAHURUMIE NA WALIMU WA MWANAO. HAWA WALIMU NAO WANAHITAJI MAPUMZIKO.
Mambo ni mengi nimechoka kuandika.