Malalamiko kwa Shule Binafsi: Wizara ya Elimu na Tamisemi waliangalie na kulitolea muongozo

Dogo langu yupo shule ya serikali ila kutokana na kuwa kidato Cha mtihani wanabaki shule kusoma

Sina doubt katika hili "Kama Elimu ni ghali jaribu ujinga"
 
Sasa mkuu kwa taarifa yako (kama haya mambo yamekupita pembeni kidogo) hakuna kitu muhimu kwenye ubongo wa binadamu yeyote kama mapumziko. Mapumziko maanake unatoka nje kidogo ya yale au utaratibu wa kila siku wa maisha uliouzoea. Ukirudi unarudi na nguvubya ajabu! Lakini watoto kuendelea na nazingira yaleyale mtihani ukifika hiyo sept. wanakuwa hoi ajili zimechoka! Matokeo yake hata performance katika mitihani inaweza kushuka!
Mkuu, utafiti unaonesha muda wa masaa nane hautoshi kuifikisha nchi kama Tanzania kwenye nchi ya asali na maziwa.

Tunahitaji sana kufanya kazi kwa muda zaidi ya huu wa sasa.

Turudi kwenye mada yako.

Kwanza jambo hili hujalifanyia utafiti wa kutosha, matokeo yake umeleta hoja ambayo kimsingi inachafua huduma nzima ya Elimu hasa kwa shule binafsi. Pengine na wewe unaweza kuwa unasadifu mapungufu ya mfumo wetu wa Elimu. (kwa kipindi fulani kama taifa tumekuwa na tabia ya kukurupuka. Watoa maoni tunakurupka, na viongozi wanakurupukia maoni, matokeo yake yanatolewa maamuzi mabaya ambayo hayana tija).

Huu utaratibu wa kuwabakiza watoto wa madarasa ya mitihani shuleni ni utaratibu ambao kwa miaka ya hivi karibuni unaratibiwa na mamlaka za elimu. Uratibu na utekelezaji wake hutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na malengo. Na kwa bahati nzuri au mbaya siku hizi shule zote za serikali na private zinalazimika kuwabakiza watoto wa madarasa ya nyakati za likizo kwa maelekezo ya viongozi. Na hata utoaji wa likizo kwa walimu wa serikali halmashauri unazingatia majukumu ya walimu wakati wa likizo. (Yaani walimu wengine wanapewa likizo mwezi June wengine wanapewa mwezi December) kwa hiyo baadhi ya Halmashauri walimu watakaobaki June watafundisha watoto darasa la saba na la nne. Wale watakaobaki Dec watafundisha darasa la sita na la tatu. Au baadhi ya Halmashauri katika mgawanyo wa vipindi shuleni wanazingatia mwaka huu usipofundisha darasa la mitihani mwaka kesho lazima upewe ili kubalance likizo. n.k n.k YAANI KWA KIFUPI SUALA LA ELIMU LIKO VERY COMPLICATED.

HOJA YAKO YA KUHUSU BINADAMU WANATAKIWA KUPUMZIKA.

Uzoefu wa huduma ya Elimu unaonesha kuwa mara nyingi watoto wanaporudi nyumbani bado wazazi wengi huwatafutia tuition. Kwa hiyo hata ile dhana ya KUPUMZIKA nayo inakosekana.
Pia Wataalam kule shuleni nako huwa wana mitazamo tofauti na tuition.

A. Shule nyingi huamini watoto wengi hujiingiza kwenye makundi yasiyofaa kupitia hizi tuition.

B. Wakati mwingine(mara nyingi kwa watoto wa shule za msingi), tuition pia huleta confusion kwa watoto kati ya kile kilichofundishwa shuleni na tuition. Walimu wetu wa tuition hawafanyi pre assessment kwa mtoto kabla ya kufundisha.

C. UONGOZI WA SHULE NA WALIMU NAO WANAZITAMANI HIZO HELA ZA TUITION ๐Ÿค‘๐Ÿค‘๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹. KWA HIYO WANAAMUA KUBUNI MBWINU YA KIHALALI YA KUZIPATA HIZO SHEKELI๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.

MORE IMPORTANTLY UZOEFU UNAONESHA WATOTO WETU WANAPORUDI SHULENI BAADA YA LIKIZO WANAKUWA WAMESAHA. YAANI WALIMU WANAANZA UPYAAAA (Hili angalau linatatulika) ๐Ÿ˜๐Ÿ˜
KUHUSU UTEKELEZAJI WA MTAALA.
Hili ni suala ambalo wengi tunajitia kulijua ila hata hatujui Changamoto za utekelezaji wa mtaala.
Nimeona mdau mmoja hapo juu amesema walimu watumie muda vizuri๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…. Ni rahisi kusema hivyo.

Mimi nataka nitoe mfano hai.

Mwaka wa masomo kwa shule za msingi una siku kati ya 192 hadi 197. Mwaka huu wa 2021 una siku 192.

Mihtasari ya masomo ya darasa la saba ina uzito sawa au kuzidi ile ya darasa la sita. LAKINI WAKATI MIHTASARI YA DARASA LA SITA IKIWA NA NAFASI YA KUTEKELEZWA KWA KWA SIKU 192-197 MIHTASARI YA DARASA LA SABA INATAKIWA KUTEKELEZWA KWA SIKU CHACHE ZAIDI KWA SABABU HUWA WANAHITIMU MWEZI WA TISA. (Hali hiyo ni kwa madarasa yote ya mitihani. Mitihani huwa inafanyika mapema).

MTOA MADA NIKUKUMBUSHE JAMBO:
Wakati wewe unalalamikia hilo, wazazi wengi ndio wanataka watoto waspend muda mwingi shuleni.

USHAURI WANGU KWA MTOA MADA.
Jitahidi kuhudhuria vikao vya wazazi ili utoe maoni yako, Pia usikilize hoja za uongozi wa shule yako. Kamati ya shule na Mkutano wa wazazi ndio chombo kikuu cha maamuzi ya uendedhaji wa shule. Kuhudhuria na kutoa maoni yako ndio njia sahihi ya kutatua na kujenga shule bora kwa watoto wetu. SHULE NI MALI YA WATOTO WETU AMBAO SISI NDIO WASIMAMIZI WAO.

PIA MTOA MADA USIWE MBINAFSI SANA. USIMHURUMIE MWANAO TU WAHURUMIE NA WALIMU WA MWANAO. HAWA WALIMU NAO WANAHITAJI MAPUMZIKO.

Mambo ni mengi nimechoka kuandika.
 
Tunaomba serikali na hasa Wizara ya Elimu na ike ya Tamisemi waliangalie sana hili na kulitolea muongozo mapema.

Malalamiko yenyewe ni kwamba kumekuwa na utaratibu kwa shule za binafsi hasa zile za English Medium kuzuia wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwenda likizo hasa ya mwezi wa sita.

Inajulikana kwamba utaratibu wa likizo upo duniani kote kwa binadamu wote wanaofanya kazi wakiwepo wanafunzi. Na hili linafanyika baada tafiti kuonesha kwamba binadamu hawawezi kufanya kazi mfululizo bila kupumzika kwani hilo linaadhiri ufanisi wao katika kazi.

Sasa inashangaza kuona shule hizi za msingi za binafsi zinawanyima wanafunzi wa darasa la nne na la sita kwenda mapumziko ya mwezi mmoja eti kisa wanawaandaa kwa mitihani ijayo.

Hawa ni watoto wadogo, wanasoma mfulilizo bila kupumzika kisa mitihani kweli hili ni sawa? Kaka na dada zao wa Form Two na Form Four wana mitihani mwishoni mwa mwaka huu lakini wapo likizo. Sasa iweje hawa wa form two na darasa la sita? Ni nini hasa so special kwa hawa wanafunzi wa English Medium schools.

Je, ni kweli kwamba muda uliopo hautoshi kuwaandaa hawa watoto kufanya vizuri kwenye mitihani yao?

Hao watalaam wa elimu na wanasaikolojia waliopendekeza utaratibu huo na ukakubalika pengi walikosea?

Isitoshe, kwa sasa kuna waraka wa serikali unaokataza shule za serikali kutofunga shule au kuongeza muda wa masomo kwa wanafunzi bila ruhusa ya mkurugenzi/serikali. Tena yamewekwa masharti na mambo ya kuzingatia kama shule itataka kutumia muda wa mapumziko wa wanafunzi kufundisha.

Je, Shule hizi za private hazifungwi na taratibu na secular hizo za serikali? Wanaruhusiwa kufanya mambo wanavyoona tu wao? Kiholela.

Tunaomba serikali na bunge waliangalie hili na liwekewe utaratibu mzuri kwa sababu linaleta usumbufu mkubwa kwa wazazi na kunyima haki ya watoto kupumzika "from daily routines za shule!"
Usimpeleke shule wakati wa likizo, baki naye nyumbani.
Wizara inahusika vp na utaratibu binafsi wa kupeleka watoto wasumbufu shuleni wakati wa likizo?
 
Utakuwa mkuu wa shule wewe! Asante kwa maoni yako Mwalimu Mkuu!
 
Hujui kwamba ndio utaratibu wa shule husika? Kuhusu watoto wasumbufu sijakuelewa! Unamaanisha watoto wote wa darsa la nne na la sita ni wasumbufu?
 
Tunaomba serikali na hasa Wizara ya Elimu na ike ya Tamisemi waliangalie sana hili na kulitolea muongozo mapema.

Malalamiko yenyewe ni kwamba kumekuwa na utaratibu kwa shule za binafsi hasa zile za English Medium kuzuia wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwenda likizo hasa ya mwezi wa sita.

Inajulikana kwamba utaratibu wa likizo upo duniani kote kwa binadamu wote wanaofanya kazi wakiwepo wanafunzi. Na hili linafanyika baada tafiti kuonesha kwamba binadamu hawawezi kufanya kazi mfululizo bila kupumzika kwani hilo linaadhiri ufanisi wao katika kazi.

Sasa inashangaza kuona shule hizi za msingi za binafsi zinawanyima wanafunzi wa darasa la nne na la sita kwenda mapumziko ya mwezi mmoja eti kisa wanawaandaa kwa mitihani ijayo.

Hawa ni watoto wadogo, wanasoma mfulilizo bila kupumzika kisa mitihani kweli hili ni sawa? Kaka na dada zao wa Form Two na Form Four wana mitihani mwishoni mwa mwaka huu lakini wapo likizo. Sasa iweje hawa wa form two na darasa la sita? Ni nini hasa so special kwa hawa wanafunzi wa English Medium schools.

Je, ni kweli kwamba muda uliopo hautoshi kuwaandaa hawa watoto kufanya vizuri kwenye mitihani yao?

Hao watalaam wa elimu na wanasaikolojia waliopendekeza utaratibu huo na ukakubalika pengi walikosea?

Isitoshe, kwa sasa kuna waraka wa serikali unaokataza shule za serikali kutofunga shule au kuongeza muda wa masomo kwa wanafunzi bila ruhusa ya mkurugenzi/serikali. Tena yamewekwa masharti na mambo ya kuzingatia kama shule itataka kutumia muda wa mapumziko wa wanafunzi kufundisha.

Je, Shule hizi za private hazifungwi na taratibu na secular hizo za serikali? Wanaruhusiwa kufanya mambo wanavyoona tu wao? Kiholela.

Tunaomba serikali na bunge waliangalie hili na liwekewe utaratibu mzuri kwa sababu linaleta usumbufu mkubwa kwa wazazi na kunyima haki ya watoto kupumzika "from daily routines za shule!"
Hilo la watoto kunyimwa kwenda likizo hata shule za serikali wanafanya.

vv
 
Ni darasa la nne na la saba. Halafu naamini hakuna wazazi waliolalamika, wewe usiye mzazi umetunga tu ili kutuvuta ndevu wazee wazima.
Ukome.
 
Utakuwa mkuu wa shule wewe! Asante kwa maoni yako Mwalimu Mkuu!
Kila unayejibu tofauti na matamanio yako unamwita mwalimu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ulianza na Mwalimu wa chekechea sasa hivi uko na Mwalimu Mkuu ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Unachotakiwa kufanya ni kuchambua, kutathimini hoja na kutoa maoni yako ili mjadala uwe mtamu.

Mambo ya kazi za watu hayatakusaidia.

Anyways binafsi ni mdau mkubwa sana wa Elimu ya wanangu. Linapokuja suala la Elimu sina mzaha kuanzia kwa Mwanangu, walimu wake hadi uongozi wa shule. KIKUBWA HUWA SIACHI KUWAPA MOTISHA WALIMU WA WANANGU KAMA NINAVYOFANYA KWA WANANGU. Taaluma ya ualimu nayo haikunipita kushoto.
 
yaani watanzania sisi ni wavivu sana tena sana mfano ni huu wa watoto kuwahurumia kipindi fulani ilikuwa sheria sikukuu ikiangukia jumapili unalipizia jumatatu watu wakafurahi sana huo ni kutokuwa na ufahamu kuwa unapunguza siku za uzalishaji uchumi unarudi nyuma kwaajili tu ya kupenda kukaa nyumbani kunakusaidia nini? kwa suala la watoto kuna usemi unasema ukiona elimu ni gharama jaribu ujinga ,

ukiuchukua mwaka unaweza ukauona mkubwa sana lakini ni muda mdogo sana ukianza kuugawanya ukumbuke kuna siku za sikukuu ambazo hawarudi wanakuwa shule lakini hawaingii darasani wakifungua january wanasomamapaka march wanafunga wikimbili wakifungua april hiyo hapowanasomamay tuwanafunga likizokubwa wanafungua july wanasoma september tena likizo wiki mbili wanafungu kidogo october hiyohapo november mwishoni wanafunga likizo kubwa hebu hesabu ni muda gani mwanao amesoma darasani na hesabu ni muda gani anakuwa hayuko darasani katika mwaka acheni watoto wawe busy na shule muda wanao kiaa nyumbani unatosha kabisa hata hivyo hizo likizo wanazobaki shuleni ni kwa madarasa yenye mitihani tu yaani waacheni watoto wasome KWANI HAO WANAFUNZI WENYEWE WANA SEMAJE?

kuna mzazi alishaambiwa na mtoto kuwa amechoka kusoma apumzike? tuacheni kuambukiza watoto uvivu tulionao
kwa hiyo twende hivyo hivyo tu na huo mfumo? Soma kwa makini michango mingine hapa utaelewa undani wa hili tatizo.
 
Kila unayejibu tofauti na matamanio yako unamwita mwalimu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ulianza na Mwalimu wa chekechea sasa hivi uko na Mwalimu Mkuu ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Unachotakiwa kufanya ni kuchambua, kutathimini hoja na kutoa maoni yako ili mjadala uwe mtamu.

Mambo ya kazi za watu hayatakusaidia.

Anyways binafsi ni mdau mkubwa sana wa Elimu ya wanangu. Linapokuja suala la Elimu sina mzaha kuanzia kwa Mwanangu, walimu wake hadi uongozi wa shule. KIKUBWA HUWA SIACHI KUWAPA MOTISHA WALIMU WA WANANGU KAMA NINAVYOFANYA KWA WANANGU. Taaluma ya ualimu nayo haikunipita kushoto.
Usijali ni katika kunogesha tu mjadala.
Kwa hiyo wewe unakubaliana na watoto wetu kubakizwa shuleni kukaririshwa mitihani? Kama mdau mkubwa wa elimu ulishayajaribu maarifa ya wanao kuona kama kuna chochote wanachopata zaidi ya kukariri maswali? Unajua kwanini baadhi ya watu hapa wanaungana mkono hoja ya walimu/shule kwamba watoto wakikaa nyumbani mwezi mzima wanasahau kila kitu? Kwa nini wasahau kila kitu? Moja ya sababu kubwa ni ufundishaji huo wa kukaririsha badala ya kuwapa watoto maarifa! Ni bahati mbaya kwamba wewe mdau mkubwa wa elimu ya watoto wako unakubaliana na huu utaratibu. Very unfortunate indeed!

Halafu kama wewe sio Mwalimu Mkuu basi ni mjumbe wa bodi ya shule.
 
Shida kubwa ya sisi watanzania, kujifunza/kusoma/elimu tunaona ni kama kazi na ndo maana wazazi wanaomba mapumziko ya vijana wao na vijana pia wanataman kupumzika na mara nyingine tunawasimamia vijana kusoma kama kusoma ni kubeba zege. Lakini ukweli elimu si kazi ni raha kama kutazama kulfi saa mbili usiku... wazaz, walim, walez tuwafanye watoto waone elimu ni sehemu ya starehe/raha.. mzazi atayetambua elimu ni sehem ya starehe atotaka mwanae abaki nyumban na pia kijana akichukulia elim n starehe hata matokeo yatakua mazur kwa sababu atasoma kwa mapenz hata bila kufundishwa.. na atakuomba kwenda shule hadi boxing day.
 
Sioni shida kwa watoto kwenda shule muda wote hasa kwa madarasa yenye mitihani. Watoto wana miezi mingi ya kucheza nyumbani baada ya kumaliza masomo.....binafsi sipendi kuona watoto wanang'aa macho nyumbani, waende huko.
 
Usijali ni katika kunogesha tu mjadala.
Kwa hiyo wewe unakubaliana na watoto wetu kubakizwa shuleni kukaririshwa mitihani? Kama mdau mkubwa wa elimu ulishayajaribu maarifa ya wanao kuona kama kuna chochote wanachopata zaidi ya kukariri maswali? Unajua kwanini baadhi ya watu hapa wanaungana mkono hoja ya walimu/shule kwamba watoto wakikaa nyumbani mwezi mzima wanasahau kila kitu? Kwa nini wasahau kila kitu? Moja ya sababu kubwa ni ufundishaji huo wa kukaririsha badala ya kuwapa watoto maarifa! Ni bahati mbaya kwamba wewe mdau mkubwa wa elimu ya watoto wako unakubaliana na huu utaratibu. Very unfortunate indeed!

Halafu kama wewe sio Mwalimu Mkuu basi ni mjumbe wa bodi ya shule.
Mkuu kabla sijakujibu hoja za msingi naomba nikwambie kitu kimoja, usitoe maoni yenye conclusion ndani yake ilhali wewe sio mtaalamu wa hii fani.

Just leave a room for the experts to chip in and make professional clarification. Kwa sababu kuna mambo wewe unayaona na unadhani ni makosa kumbe hata sio makosa au ni njia moja kati nyingi ya kufikia malengo.

Haya turudi kwenye hoja sasa.

Kwanza kwenye hoja (post) yako ya msingi kule juu haijaongelea suala la kukaririsha watoto mitihani. HOJA YAKO YA MSINGI ILIKUWA NI KUTOTOA FURSA KWA WATOTO WETU KUPUMZIKA WAKATI WA LIKIZO.

Kuwazuia watoto wasipumzike na kuwakaririsha watoto mitihani ni vitu viwili tofauti. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kubaki wakati wa likizo na kukaririsha. NINAMAANA KWAMBA KUKARIRISHA KUNAWEZA KUFANYIKA WAKATI WOWOTE WA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI. KWA MAANA NYINGINE RATIBA ZA LIKIZO ZINAWEZA KUZINGATIWA NA WATOTO BADO WAKAWA WANAKARIRISHWA.

KUHUSU KUKARIRISHWA MAARIFA.
Hili suala ni pana kidogo, ila kwa ufupi iko hivi:
Kabla ya mwaka 2016 mtaala wetu wa shule za msingi ulikuwa Content based curriculum. Mtaala huu ulikuwa unajikita kuona ni jinsi/kuasi gani mwanafunzi anajua vitu. Kwa kiasi fulani mtaala huu ulikuwa una support sana kukariri. Sasa hata walimu wetu bado ni zao la mtaala huo.

Sasa hivi tuna mtaala mpya unajulikana kama Competence based curriculum. Ni mtaala unaojikita na umahiri zaidi. Kwa kiasi kikubwa mtaala huu hauna uhuru wa kukaririsha kwa kiasi kikubwa. Mwaka huu (2021) ndio watoto wetu wanatahiniwa kwa mara ya kwanza kupitia mtaala huu mpya.

KUHUSU SUALA LA KUKARIRISHA MITIHANI.
Kwanza kabisa kwa darasa la saba mwaka huu hakuna cha kukaririsha mitihani kwa sababu hakuna rejea (mitihani) za kutosha kwa sababu huu ni mtihani wa kwanza wa mtaala mpya.

PILI: Ufundishaji huendana na upimaji. Na upimaji huwa una lengo la kujua kiwango cha ubora wa elimu.

Yaani sisi kama nchi tukitaka kujua kiwango cha ubora elimu yetu tunajuaje?? TUNAJUA KWA KUANGILIA KIWANGO CHA UFAULU KATIKA UPIMAJI NA MITIHANI YA KITAIFA.

ikumbukwe kuna aina nyingi za kupima kiwango cha ubora wa Elimu ila kwa Tanzania na nchi nyingine nyingi kama majirani zetu njia kuu tunayotumia ni hiyo niliyoitaja.

Ukirudi kwenye ngazi ya shule, Halmashauri na Mkoa hiyo ndio njia kuu inayotumika kujua kama malengo ya UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI yamefikiwa kikamilifu.

Hata Maafisa Elimu ngazi mbalimbali wanawajibishwa au kupongezwa kwa kugezo hicho.

Kwa siku hizi za karibuni mitihani mingi inaratibiwa kuanzia ngazi ya shule hadi mkoa. Siku hizi hadi majaribio ya mwezi unaweza kukuta yanafanyika kwa ngazi ya mkoa.

KUHUSU MAONI YANGU BINAFSI
Mimi siku zote huwa nawashauri kuwapeleka watoto kwenye shule zinazoeleweka.

Siku hizi kuna shule nyingi hazieleweki kabisa. Yaani wanakusanya tu fedha za wazazi. Shule inamaliza mwaka haijafanya hata kikao cha wazazi, shule haina Kamati ya shule, shule ukifuatilia kwa ndani unakuta hailipi hata walimu, shule inasimamiwa mke wa mwenye shule na wanae(yaaani family members ndio Alfa na Omega).

Ila bado kuna shule nyingi sana zinazoendesha mambo yake kwa weledi.

Pia kwa sasa serikali imetoa mwongozo wa kuwa na umoja wa walimu na wazazi(UWW). Pamoja na mambo mengine Umoja huu umewapa wazazi nguvu ya kuwawajibisha walimu kwa ufundishaji usiofaa.
 
Competence based curriculum ni jina tu ndugu. Ni empty vocabularies zisizokuwa na uhalisia. Ninafuatilia sana wanachofundishwa watoto na vitabu wanavyosoma, sijaona huo mtaala mpya ukiakisiwa kwenye vitabu na ufundishaji! Unapozungumzia competence based curiculum unazungumzia imparting knowledge and skills! Katika hili labda wanafanikiwa tu kwenye lugha ya kiingereza. Wanafunzi wengi wa English medium wanamudu kuisoma, kuandika ma kuzungumza kingereza vizuri. Masomo mengine sijana hiyo competence! Vitabu vyenyewe vya siku hizi viko so shallow. Lugha yenyewe iliyotumika utashangaa hivi vitabu vilipitishwaje visomwe nacwatoto wetu? Sasa sijui hiyo competence itatoka wapi? Ndio maana nikasema huu ni msamiati tu mtamu masikioni lakini hakuna dalili zozote za ufundishaji unaozingatia huo mtaala!

By the way, waalimu waliandaliwa vilivyo kufundisha kwa kuzingatia mtaala mpya?

Bado tuna safari ndefu!
 
Bado tuna changamoto ya utekelezaji wa mtaala mpya.

Ndio maana pale juu imesema walimu wetu bado ni zao la Content based curriculum.

Kwenye suala la mtaala, kuna mtaala wenyewe na kuna utekelezaji wa mtaala. Mtaala ukitekelezwa vibaya tatizo linakuwa ni la watekeleza mtaala na sio kwamba mtaala ndo unakuwa mbaya.

mfumo wetu wa Elimu unapitia changamoto kubwa ya utekelezaji wa mtaala kwa kiwango kikubwa sana.

Pia hii competence based curriculum inakuwa supplemented na format mpya ya mtihani. Mitihani ya sasa inapima zaidi competence kuliko contents.

KUHUSU VITABU
Suala vitabu ni tatizo kubwa. Na limekuwa ni tatizo hasa pale wataalam wetu walipoingia kwenye mtego wa siasa za kujipendekeza. Yaani taasisi za umma hata zile za kihuduma kutaka kufanya biashara. Na mwishowe tulikuwa tunawaona wakurugenzi mbele ya Kamera wanatoa gawio kwa serikali.๐Ÿค”๐Ÿค”

HAIWEZEKANI KITABU UKITUNGE MWENYEWE, UHARIRI MWENYEWE NA ITHIBATI UJIPE MWENYEWE ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.

Siku hizi TET wanauza hadi madaftari ya maandalio, maazimio, mahudhurio n.k๐Ÿ˜ฒ๐Ÿ˜ฒ๐Ÿ˜ฒ
 
Asante kwa kuendelea kutushirikisha utaalamnwako katika hili!
 
Nashukuru serikali imepata huu ujumbe na imeshachukua hatua tayari za kuwataka wahusika wajieleze kwa nini watoto hawajaenda likizo!
 
Back
Top Bottom