Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Mtoa hoja mwanzoni nilishangaa kichaga "Yesu Maria na Yosefu " ila ukiangalia kwa makini Mungu wa kweli hawezi kuandaa moto wa kuchoma watoto wake .Hayo mambo yalitungwa ili tuogope tupokee dini zao
Mungu wa kweli unamjuaje?ni nani aliyeeleza jinsi Mungu wa kweli anapaswa awe? Kama watu waliweza kutunga mambo kuhusu Mungu ili tu muogope na kufuata dini zao,je ni maelezo ya nani tutayakubali kuwa hayajatungwa kuhusu Mungu?
 
Soma Comment ya Kiranga niliyokutage hapo chini uelewe hoja yake vizuri

Msingi wa hoja ya Kiranga ipo hivi;-

"Kama Mungu mwenye upole,huruma,muweza wa kila kitu yupo, mbona kuna shida na taabu na majanga yanawaandama watu kwanini asiyaondoe tuishi kwa raha??. Na akajenga hoja kwamba kwakuwa hizo shida zipo basi Mungu hayupo"

👆🏻Huo ndiyo msingi mkuu wa yeye kumkanusha Mungu kama kuna chochote alichoongeza basi hakijavunja huo msingi anao uamini.

JIBU LA HIYO HOJA YAKE👇🏻

Yeye kaangalia upande mmoja tu wa shilingi upande wa shida lakini hajaangali upande wa pili wa shillingi upande wa raha na sterehe, kulingana na hoja yake,kama Mungu hayupo kutokana na Shida na taabu za watu vipi Mungu asiwepo kutokana na raha na starehe za watu??.

👆🏻Hapo utaona hoja yake ikifa kifo cha kawaida kabisa na hataweza kuitetea.

Hoja yake unaweza kuiwekea mfano huu hapa;-

" kwakuwa usiku hakuna mwanga basi hakuna jua" huku anasahau "counter argument" kwamba kwakuwa mwanga upo mchana basi jua lipo". Basi kulingana na hoja ya kuwepo na kutokuwepo jua mtu mwenye akili atajua tu kuwa jua lipo mchana na usiku isipokuwa mwanga wake unakosekana wakati fulani (usiku) na unapatikana wakati fulani (mchana).

Basi kiranga ajifunze hapo ili aone jinsi hoja yake ilivyokuwa baseless.

Bado hajajibu maswali yanaweza kumsaidia kujua uwepo wa Mungu, maswali yenyewe ni:-

(1) Ulikuja duniani kwa amri ya kutoka wapi?
(2) Ulijua ungekuja lini ?
(3) Umekuja kufanya nini?
(4) Hiyo jinsia uliyonayo nani kakuchagulia?
(5) Kwa nini hukuwa nyani au mende?
(6) Umejuaje kama tsunami na kipindupindu ni taabu na shida ,je mende anajua kuwa hizo ni shida?
(7) nk, nk, nk.

Hatoi majibu, yeye anashikilia tu "thibitisha kama Mungu yupo!!"😁😁😁 , maskini wala hata hiyo nguvu ya kukanusha hajui imetokea wapi!!!.
 
Kuna mtu kathibitisha Mungu yupo?

Au longolongo za kila siku tu?
Kama uthibitisho ingekuwa ndio hoja ya msingi kuonesha hakuna Mungu basi isingewezekana kwa atheits kuja kukubali uwepo wa Mungu.

Tafakari.
 
KWELI NECTA WANAPATA KAZI KWENYE USAHIHISHAJI WA MITIHANI, NIMEAMINI.MTU UNAULIZWA MASWALI THEN UNAANZA KULAUMU NA KUHUKUMU....SASA NIMEELEWA NI KINA NANI WANAOANDIKA HIP HOP NA MATUSI KWENYE MITIHANI...MASWALI YAPO 10, SOMA YOTE THEN UTOE MAJIBU, KAMA HUJUI SUBIRI WANAO FAHAMU WATUJULISHE...TOFAUTI NA HAPO KAA KIMYA!!!
Nimechekaaaaa
 
HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA.

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la muziki the beatles. Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.

Kwa wale wanaotaka kujua mengi, wafungue GOOGLE na kisha kusearch haya "People who mocked GOD and died" Utasoma mengi tu.

*Watumie ujumbe huu ndugu na jamaa,ujumbee huu utawasidia kumuheshimu Mungu na kumtii.

Hali ya kumcha Mungu iongezeke ndani yako na kama nikuuliza maswali basi yafaa kuuliza kwa lengo la kujifunza na siyo kutengeneza ubishi usio na lazima.
Amina
Mkuu hapo mbn umeweka vitisho,,,juzi Hapo raisi wa philipino alisikika akisema "kwa yeyote atakae nithibitishia kua mungu yupo kwa kupiga selfie na mungu niko niko tayali kujiuzuru" but nothing happened to him alaf kwenye hiyo hoja yako ya namba nne huyo aliyetengeneza titanic mungu alichukia kwa maneno ya dhihaka akaamua kuzamisha meli na kuua watu wengine kwa ajili ya dhihaka ya mtengeneza meli yani nisawa namm niwe na ugomvi na ww alafu nije nilete vurugu hadi kwa watoto zako wasio na hatia
 
Msingi wa hoja ya Kiranga ipo hivi;-

"Kama Mungu mwenye upole,huruma,muweza wa kila kitu yupo, mbona kuna shida na taabu na majanga yanawaandama watu kwanini asiyaondoe tuishi kwa raha??. Na akajenga hoja kwamba kwakuwa hizo shida zipo basi Mungu hayupo"

👆🏻Huo ndiyo msingi mkuu wa yeye kumkanusha Mungu kama kuna chochote alichoongeza basi hakijavunja huo msingi anao uamini.

JIBU LA HIYO HOJA YAKE👇🏻

Yeye kaangalia upande mmoja tu wa shilingi upande wa shida lakini hajaangali upande wa pili wa shillingi upande wa raha na sterehe, kulingana na hoja yake,kama Mungu hayupo kutokana na Shida na taabu za watu vipi Mungu asiwepo kutokana na raha na starehe za watu??.

👆🏻Hapo utaona hoja yake ikifa kifo cha kawaida kabisa na hataweza kuitetea.

Hoja yake unaweza kuiwekea mfano huu hapa;-

" kwakuwa usiku hakuna mwanga basi hakuna jua" huku anasahau "counter argument" kwamba kwakuwa mwanga upo mchana basi jua lipo". Basi kulingana na hoja ya kuwepo na kutokuwepo jua mtu mwenye akili atajua tu kuwa jua lipo mchana na usiku isipokuwa mwanga wake unakosekana wakati fulani (usiku) na unapatikana wakati fulani (mchana).

Basi kiranga ajifunze hapo ili aone jinsi hoja yake ilivyokuwa baseless.

Bado hajajibu maswali yanaweza kumsaidia kujua uwepo wa Mungu, maswali yenyewe ni:-

(1) Ulikuja duniani kwa amri ya kutoka wapi?
(2) Ulijua ungekuja lini ?
(3) Umekuja kufanya nini?
(4) Hiyo jinsia uliyonayo nani kakuchagulia?
(5) Kwa nini hukuwa nyani au mende?
(6) Umejuaje kama tsunami na kipindupindu ni taabu na shida ,je mende anajua kuwa hizo ni shida?
(7) nk, nk, nk.

Hatoi majibu, yeye anashikilia tu "thibitisha kama Mungu yupo!!"😁😁😁 , maskini wala hata hiyo nguvu ya kukanusha hajui imetokea wapi!!!.
Umejitahidi kujibu hoja za Kiranga lakin hoja zako ni absotute BASELESS
 
Du majibu tutayapata tutakapo kutana na naye. Kuwa mpole jomba lai. Ninachojua yeye Anatupenda. Pia hana Upendeleo ila Esau alimchukia na Yakobo alimpenda. Mwombe teye akupe uwelewa wa maneno yake. Ninachojua tu nilikuwa Mgonjwa yeye kaniponya
 
Umejitahidi kujibu hoja za Kiranga lakin hoja zako ni absotute BASELESS

Hutaki kukiri kwamba hiyo hoja yake ya msingi kupinga uwepo wa Mungu ndiyo baseless, kwa sababu kama shida na taabu ni kigezo cha kutokuwepo Mungu, sasa utasema nini juu ya raha na starehe zilizopo??, bila shaka, kulingana na msingi wa hoja yake Mungu atakuwepo kwa sababu ya raha na starehe zilizopo!!, na ndiyo maana nasema yeye amekurupuka tu bila kufanya tathmini ya kina kabla hajatoa hiyo hoja kwa sababu hata mwenye akili ndogo ataona hiyo hoja ikijipinga yenyewe kabla haijapingwa na mtu. (THE SELF CONTRADICTORY ARGUMENT).

Tafuteni hoja zingine na kamwe hamtapata kwa sababu hamjui mpo hapa duniani kwa sababu ipi na nani kawaleta?, na wala hamkuja kwa hiyari yenu halafu leo mnakuwa washindani na wajuvi kana kwamba mmejiumba wenyewe.
😁😁😁😁

🍒NANI KAMA MUNGU?🍒
 
Mkuu hapo mbn umeweka vitisho,,,juzi Hapo raisi wa philipino alisikika akisema "kwa yeyote atakae nithibitishia kua mungu yupo kwa kupiga selfie na mungu niko niko tayali kujiuzuru" but nothing happened to him alaf kwenye hiyo hoja yako ya namba nne huyo aliyetengeneza titanic mungu alichukia kwa maneno ya dhihaka akaamua kuzamisha meli na kuua watu wengine kwa ajili ya dhihaka ya mtengeneza meli yani nisawa namm niwe na ugomvi na ww alafu nije nilete vurugu hadi kwa watoto zako wasio na hatia

Nyie mnaopinga uwepo wa Mungu salama yenu mpinge tu bila kuleta dharau na kashfa dhidi Yake vinginevyo "to hell".

Kuna mgiriki mmoja alikuwepo Kilosa (Morogoro) miaka ya nyuma 70s au 80s, yeye alikuwa anasumbuliwa sana na mafuriko sehemu moja ya shamba lake, siku moja akaamua kufanya ukarabati na kuweka daraja kuyadhibiti maji na akaweka tuta kubwa sana kwa gharama kubwa na alipomaliza akatamba hadharani kwamba:- "hata akija Mungu na mjomba wake hawawezi kung'oa hilo tuta na daraja".

Kesho yake tu ikanyesha mvua kubwa na ikasomba kila kitu na hali ilikuwa mbaya mno kuliko ilivyokuwa siku zote hapo katika mafuriko ya awali,

Watu wakamkebehi yule mgiriki, wakamwambia huyo aliyefanya gharika hiyo ni "mjomba wa Mungu" na Yeye mwenyewe bado hajaanza gharika lake.

Tahadhari:- mnapokanusha uwepo wa Mungu hiyo ni hatua ya awali ya kuelekea kumdhihaki na hapo ndipo mtakapo tambua kwamba Yeye yupo.
 
Kama uthibitisho ingekuwa ndio hoja ya msingi kuonesha hakuna Mungu basi isingewezekana kwa atheits kuja kukubali uwepo wa Mungu.

Tafakari.
Atheist yupi?

Mbona mimi atheist, siamini kuwepo Mungu, na sijawahi kuthibitishiwa kuwepo Mungu?

Unakubali kwamba huwezi kuthibitisha Mungu yupo?

Kwa nini huyo Mungu wenu anajificha ficha hivyo hajioneshi wazi ajulikane na wote bila utata?

Aanaogopa kudaiwa kodi?
 
Sijamdhihaki nimesema kweli. Kwani kuna uongo hapo??

hakuna uongo hapo! hakuna ulicho kitunga vyote vimeandikwa kwenye vitabu vya dini.

watu wanahofu kutokana na jinsi dini zao zinavyowaaminisha.Lakini kiuharisia haya mambo ya dini probability kama ni ya kweli ni ndogo sana.
bado siwalaumu waanzisha dini waliona mbali sana walijua hiyo ndio njia ya kuleta amani na ustaarabu ktk jamii .

Mimi na wewe tunajukumu la kusupport dini kuendelea ili jamii isiwe na maovu.Binafsi najiita na dini fulani hata wanangu nitawaambia hivyo ingawaje akilini mwangu najua mimi ni mpagani nafanya yote hyo ili kutaka kujenga maadili mema kwa familia na jamii,ila mambo ya moto,pepo,shetani nk ni hamasa na vitisho ili watu wakae kwenye mstari, binadamu wengine hawana kabisa selfdispline hawawezi kujiongoza wenyewe.
 
Jaribu kuelezea uwepo wa Mungu pasipo wewe kuwepo. Ukishindwa, ujue wewe ndiye mwanzo na mwisho, Alpha na Omega.

Uwepo wako ndio uwepo wa kila kitu. Hakuna JF bila Mimi kuwepo. Hakuna Mungu bila Mimi kuwepo. Hakukaa kuwepo na hatakaa awepo nje ya uwepo wangu.

Sikuwepo, na hivyo hakukuwa na uwepo katika kutokuwepo kwangu. Nipo ndio maana kuna uwepo. Kabla ya kuwepo, sikuwaza kuhusu uwepo. Sikuwa huru kuchagua namna ya kuwepo au kuwasiliana na uwepo au kuamua kutokuwepo.

Mama mjamzito yupo kwa kuwa kuna kiumbe hai tumboni. Wazazi wapo kwa kuwa kuna watoto n.k n.k Mungu yupo au hayupo kwa kuwa tupo. Usipokuwepo, hakuna kilichopo.
 
Atheist yupi?

Mbona mimi atheist, siamini kuwepo Mungu, na sijawahi kuthibitishiwa kuwepo Mungu?

Unakubali kwamba huwezi kuthibitisha Mungu yupo?

Kwa nini huyo Mungu wenu anajificha ficha hivyo hajioneshi wazi ajulikane na wote bila utata?

Aanaogopa kudaiwa kodi?
Wapo atheists kibao tu ambao wamekubali uwepo wa Mungu,si jambo la ajabu(kama hili nalo la kubisha sema niweke list) ila cha kutafakari hapa,ni kwamba kama uthibitisho ndio ingekuwa ni hoja ya msingi kwa basi hili jambo lisingewezekana.

Na ndiyo maana mara zote nakwambia kuwa suala la uwepo wa Mungu ni imani ndiyo ipo hivyo na si kwamba watu wameamua tu waamini kwa kukosa uthibitisho,hivyo hizo hoja za kwamba amejificha sijui hakuna uthibitisho zinakuja baada ya kuliondoa suala la uwepo wa Mungu kwenye sehemu yake husika.

Kama unaona hakuna lolote lenye kukufanya hadi uamini kuwa kuna Mungu,basi hapo ndio kwenye hoja ya msingi lakini sio kuja kutumbia kuwa hakuna uthibitisho.
 
Aleluya kwa wingi na kukesha , siku ya mwisho ukaambiwa ulikuwa unapoteza mda wa kujifunza na kuijua dunia utafanyaje ?ambao hatujawahi hata kutaja neno Mungu tukapongezwa kwa kutokuamini vitu ambavyo havionekani utashangaa !!
 
Back
Top Bottom