Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

hakuna uongo hapo! hakuna ulicho kitunga vyote vimeandikwa kwenye vitabu vya dini.

watu wanahofu kutokana na jinsi dini zao zinavyowaaminisha.Lakini kiuharisia haya mambo ya dini probability kama ni ya kweli ni ndogo sana.
bado siwalaumu waanzisha dini waliona mbali sana walijua hiyo ndio njia ya kuleta amani na ustaarabu ktk jamii .

Mimi na wewe tunajukumu la kusupport dini kuendelea ili jamii isiwe na maovu.Binafsi najiita na dini fulani hata wanangu nitawaambia hivyo ingawaje akilini mwangu najua mimi ni mpagani nafanya yote hyo ili kutaka kujenga maadili mema kwa familia na jamii,ila mambo ya moto,pepo,shetani nk ni hamasa na vitisho ili watu wakae kwenye mstari, binadamu wengine hawana kabisa selfdispline hawawezi kujiongoza wenyewe.
Hebu tutumie akili kidogo kupima huo mtazamo wako.

Kuna dini ambazo zina adhabu zake kwa makosa mbalimbali kama vile kuuwa,kuiba,kuzini na mengine mengi tu. Hayo yote yanafanyika hapa hapa na si kwamba ukiiba unaachiwa kwa kutishwa kwa kuwa kuna moto kwa Mungu,sasa wewe unaposema watu wametunga tu hayo mambo ya moto ili kuwatisha watu kufanya maovu,labda ungeeleza ni maovu yapi hayo?
 
Jaribu kuelezea uwepo wa Mungu pasipo wewe kuwepo. Ukishindwa, ujue wewe ndiye mwanzo na mwisho, Alpha na Omega.

Uwepo wako ndio uwepo wa kila kitu. Hakuna JF bila Mimi kuwepo. Hakuna Mungu bila Mimi kuwepo. Hakukaa kuwepo na hatakaa awepo nje ya uwepo wangu.

Sikuwepo, na hivyo hakukuwa na uwepo katika kutokuwepo kwangu. Nipo ndio maana kuna uwepo. Kabla ya kuwepo, sikuwaza kuhusu uwepo. Sikuwa huru kuchagua namna ya kuwepo au kuwasiliana na uwepo au kuamua kutokuwepo.

Mama mjamzito yupo kwa kuwa kuna kiumbe hai tumboni. Wazazi wapo kwa kuwa kuna watoto n.k n.k Mungu yupo au hayupo kwa kuwa tupo. Usipokuwepo, hakuna kilichopo.
Usipokuwepo wapi sasa? maana kiuhalisia kabla ya wewe kuwepo kuna watu walikuwepo na ndiyo chanzo cha wewe kuwepo,sasa utasemaje usipokuwepo na hakuna kilichopo?
 
Hebu tutumie akili kidogo kupima huo mtazamo wako.

Kuna dini ambazo zina adhabu zake kwa makosa mbalimbali kama vile kuuwa,kuiba,kuzini na mengine mengi tu. Hayo yote yanafanyika hapa hapa na si kwamba ukiiba unaachiwa kwa kutishwa kwa kuwa kuna moto kwa Mungu,sasa wewe unaposema watu wametunga tu hayo mambo ya moto ili kuwatisha watu kufanya maovu,labda ungeeleza ni maovu yapi hayo?

unamaanisha kwamba kitisho pekee ambacho nimekiieleza ni moto Siku ya mwisho? au nimeelewa vibaya? (nifafanulie swali lako kama nimeelewa bibaya)

ila kama nitakuwa nimekuekewa vizuri acha nikujibu kama ifuatavyo "hata hizo adhabu za direct zinazotolewa na binadamu wenzetu ni moja ya vitisho ili watu wasifanye maovu kama kuiba,kuzini na kuua." ukifuatilia post yangu vizuri utaona nimekuwekea kifupi 'nk' nikimaanisha na kadharika.
maovu hayo kama yangefanyika katika jamii kwa kuwa akuna kipingamizi basi dunia isingekuwa salama sana.
 
Nyie mnaopinga uwepo wa Mungu salama yenu mpinge tu bila kuleta dharau na kashfa dhidi Yake vinginevyo "to hell".

Kuna mgiriki mmoja alikuwepo Kilosa (Morogoro) miaka ya nyuma 70s au 80s, yeye alikuwa anasumbuliwa sana na mafuriko sehemu moja ya shamba lake, siku moja akaamua kufanya ukarabati na kuweka daraja kuyadhibiti maji na akaweka tuta kubwa sana kwa gharama kubwa na alipomaliza akatamba hadharani kwamba:- "hata akija Mungu na mjomba wake hawawezi kung'oa hilo tuta na daraja".

Kesho yake tu ikanyesha mvua kubwa na ikasomba kila kitu na hali ilikuwa mbaya mno kuliko ilivyokuwa siku zote hapo katika mafuriko ya awali,

Watu wakamkebehi yule mgiriki, wakamwambia huyo aliyefanya gharika hiyo ni "mjomba wa Mungu" na Yeye mwenyewe bado hajaanza gharika lake.

Tahadhari:- mnapokanusha uwepo wa Mungu hiyo ni hatua ya awali ya kuelekea kumdhihaki na hapo ndipo mtakapo tambua kwamba Yeye yupo.
Bado nashindwa kukutofautisha na mwenzako nilom quote wote mmebez kwenye vitisho kuliko kutoa majibu ya mleta mada nadhani ukileta majibu itapendeza zaidi
 
unamaanisha kwamba kitisho pekee ambacho nimekiieleza ni moto Siku ya mwisho? au nimeelewa vibaya? (nifafanulie swali lako kama nimeelewa bibaya)

ila kama nitakuwa nimekuekewa vizuri acha nikujibu kama ifuatavyo "hata hizo adhabu za direct zinazotolewa na binadamu wenzetu ni moja ya vitisho ili watu wasifanye maovu kama kuiba,kuzini na kuua." ukifuatilia post yangu vizuri utaona nimekuwekea kifupi 'nk' nikimaanisha na kadharika.
maovu hayo kama yangefanyika katika jamii kwa kuwa akuna kipingamizi basi dunia isingekuwa salama sana.
Nimetaja moto ni kwa sababu ni jambo la kiimani,suala la kwamba waliyofanya maovu watakuja kuchomwa moto na Mungu ni jambo la imani ambalo linaelezwa kwenye dini.

Nakunukuu: "watu wanahofu kutokana na jinsi dini zao zinavyowaaminisha.Lakini kiuharisia haya mambo ya dini probability kama ni ya kweli ni ndogo sana."

Maana ni kwamba watu wametunga tu watu waogope kufanya mabaya ili tuishi vizuri.
Sasa kama lengo la kutunga habari za moto lilikuwa ni kuwafanya watu wakae njia sahihi kwa kuwaogopesha na huo moto wa imani, basi kusingekuwa na hizo adhabu za moja kwa moja hapa hapa kwa wenye kufanya maovu.
 
Bado nashindwa kukutofautisha na mwenzako nilom quote wote mmebez kwenye vitisho kuliko kutoa majibu ya mleta mada nadhani ukileta majibu itapendeza zaidi

Mbona ni kitu rahisi tu kwani ukisoma mazingira tunayoishi na viumbe vyote vilivyomo inatosha kabisa kutambua kwamba yupo muumbaji wa vitu hivyo weka mbali sisi wenyewe watu.

Kila kitu kina makusudio yake ya kuwepo kwake, mfano wote tunajua makusudio ya mimea na miti, makusudio ya wanyama, makusudio ya ardhi, hewa, maji, mwanga, usiku, mchana, vyakula nk, vitu vyote hivyo vyenye makusudio maalum iweje vitokee tu kwa bahati nasibu??

Sasa tuje kwa mtu, makusudio ya mtu hapa duniani ni yapi??, je alikuja kwa hiyari yake??, ilikuaje akatokea huku akiwa na akili ya kujitambua (concious mind)??.

Kama baadhi ya vitu na wanyama vinayo sababu ya manufaa kuwepo, vipi mtu akose sababu ya kuwepo kwake hapa duniani ukizingatia kwamba hakuna kitu chichote kilikuja kwa hiyari yake hapa duniani.

Hivyo kutokana na hali hiyo ninasema kuna nguvu yenye hekima iliyotenda na kusababisha watu na na hivyo vitu vikapatikana na nguvu hiyo ndiyo tunasema ni Mungu.

Kama unataka kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa kumuona kwa Macho hiyo ni kinyume kabisa na sifa yake kwani utendaji na shughuli zake zinatosha kwa mwenye akili kutambua Yeye yupo.

Mfano sote tunakubali kwamba nguvu za uvutano zipo lakini nani amepata kuziona??, tunakubali zipo kwa sababu tunaona zinavyotenda kazi.
 
kisicho kuwepo hakithibitiki huwezi kukithibitisha kwa kuwa hakipo wewe unayesema kipo ndio unayetakiwa ukithibitishe kama kipo
Unajua kusema hauwezi kuthibitisha kisichokuwepo kwa sababu hakipo,ni sawa na kusema haina haja ya kuthibitisha kuwepo kwa kitu kwa sababu teyali kipo?
 
Usipokuwepo wapi sasa? maana kiuhalisia kabla ya wewe kuwepo kuna watu walikuwepo na ndiyo chanzo cha wewe kuwepo,sasa utasemaje usipokuwepo na hakuna kilichopo?
Huwezi kujua kuwa watu na vitu vilikuwepo kabla ya kuwepo kwako. Hata mzazi haitwi mama au baba hadi awepo (mtoto) wa kumwita hivyo.
 
Huwezi kujua kuwa watu na vitu vilikuwepo kabla ya kuwepo kwako. Hata mzazi haitwi mama au baba hadi awepo (mtoto) wa kumwita hivyo.
Kiuhalisia ili apatikane huyo mtoto lazima kwanza mwanamke na mwanaume wafanye tendo la ndoa na mimba iingie,kama ni hivyo basi lazima ukubali kuwa watu walikuwepo kabla yetu sie.

Baba yupo kazini hajui chochote kuhusu nyumbani,ila hiyo haifanyi kuwa hakuna kilichopo au kinachoendelea nyumbani kwake hadi kwamba yeye awepo.
 
kisicho kuwepo hakithibitiki huwezi kukithibitisha kwa kuwa hakipo wewe unayesema kipo ndio unayetakiwa ukithibitishe kama kipo

Yawezekana understanding yako ikawa ndogo, au umetia kufuli akili yako kisiingie chochote kinachothibitisha uwepo wa Mungu,in that case however hard someone tries to make you understand the concept of God existence you will never ever grasp it deliberately. Mark the words of wisdom 👇🏻

"Huwezi kumuamsha mtu aliyejifanya kulala, lakini unaweza kumuamsha mtu aliyelala kiukweli".

Mnakazania tu:- " thibitisha kama Mungu yupo"----- ilhali ukiulizwa toa sababu ya wewe kuwepo hapa duniani jibu ni sufuri halafu mnakimbila maswali yaliyojuu ya akili zenu na hata mkijibiwa mnashindwa kuelewa majibu.

Kama huna jibu la sababu gani wewe upo hapa duniani basi huna tofauti na Mbuzi, Ng'ombe nk, kwa sababu wanyama hawajitambui, they are driven by instincts and not conscious mind. Wewe ulisikia wapi Mbuzi au Mbwa anazungumza juu ya kuwepo kwa Mungu?. Sasa hatuwezi kuishi kama Mbuzi nk.
 
Kitendo cha kuwepo understand yangu ndogo ndio kunazidi kuonyesha mungu hayupo

Kwanini mungu mwenye busara na hekima aumbe watu wengine awape understanding kubwa na wengine awape understanding ndogo
 
Kama ambavyo wewe ulivyoshindwa kueleza tu ni vp akili iwe na power ya ku control watu,ila bado unaamini hadithi za kwamba et akili ina power.

Sijashindwa kukuelezea ila nilitaka kukuonyesha kuwa ukitaka kuelewa vizuri nikupe reference za ukweli uchambue hapa tunapeana njia hatuwezi kujifunza au kueleza yote humu
 
Sijashindwa kukuelezea ila nilitaka kukuonyesha kuwa ukitaka kuelewa vizuri nikupe reference za ukweli uchambue hapa tunapeana njia hatuwezi kujifunza au kueleza yote humu
Na watu wa dini nao wangekuwa wanasema kama unadhani kungekuwepo hata hii mijadala?

Maana kila mtu angeishia kutaja vitabu vya akasome mwenyewe.
 
Namaanisha kuna mmoja kati hivyo vitu viwili anamtegemea mwenzake kuwepo kwake yaan hawezi kukaa pekee yake

Ngoja nukupe mfano ili tuelewane vizuri nini maana ya giza
Unajua kwanza kuwa hakuna mwenye kutaka mthibitishe kitu ambacho hakipo bali mnatakiwa mthibitishe kutokuwepo kwa hicho kitu? Unaposema haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo kwa sababu hakipo,huwa unakusudia kuonesha kitu ambacho hakipo na ndiyo maana unasema haiwezekani.

Na hata mie nakubaliana na hilo,ila hapa watu hawajataka hivyo bali wanataka mthibitishe kutokuwepo kwa hicho kitu.
 
Back
Top Bottom