Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Mthibitishie kuwa Mungu yupo na sio kumhubiria!

Mungu muumba wa vyote, mwenye upendo, muweza wa yote na mjuzi wa yote yupo kweli au ni hadithi tu?
Kiranga, hoja zako za kumkanusha Mungu ni nyepesi mno ndiyo maana unatakiwa "u have to exercise and fine tune your intellect".

Nikikuangalia, japo sikuoni!!, unaonekana ni mtu mwenye jazba iliyoziba uelewa wako kutokana na "preconceived mind set" kwamba Mungu hayupo.

Sisi sote hapa duniani hatuna hiyari ya kumpangia Mungu kwa sababu hatukuja kwa amri yetu kwa minajili hiyo tunatakiwa kutafakari hekima (philosophy) ya uumbaji na matukio yote yanayotukabili hapa duniani, hivyo jambo la kwanza kabisa ni kutafuta HEKIMA YA SISI KUWEPO DUNIANI BILA HIYARI YETU baada ya kupata majibu ndipo hatua nyingine ifuate na siyo kupinga tu "blindly" kwa tamaa za ufahamu wako finyu juu ya mambo ya kimbingu na mbaya zaidi unataka kupotosha UMMA kwamba Mungu hayupo!!.

Hivi sasa umeumbwa na upo katika hali hiyo je, kama ungeweza kujiumba mwenyewe ingekuaje ??
 
Kutokujua chanzo chako isiwe kigezo cha kusema Mungu yupo.

Kiujumla maswali anayouliza Kiranga yamekuzidi upeo
Shida yako unataka uthibitishiwe kuwa Mungu yupo katika njia unayoitaka wewe (preconceived way). Mtu akikuthibitishia kinyume cha hivyo unavyotaka unashindwa kumuelewa/hutaki kumuelewa.

Na jambo la muhimu ni kwamba thibitisha wewe mwenyewe umetoka wapi? na baada ya hapo ndipo uulize mambo mengine kama yanayohusu uwepo wa Mungu nk.

Au ulitaka umuone Mungu akiwa na ofisi yake amekaa kitini na juu ya meza kuna mafaili mbalimbali, pembeni kukiwa Mihuri, kompyuta,simu ya mezani,jokofu lililojaa vinywaji baridi na meza ndogo juu yake kuna chupa ya chai nk, hapo ndipo ungeamini kuwa YEYE yupo!!!??. A Very, very absurd notion.
 
Mthibitishie kuwa Mungu yupo na sio kumhubiria!

Mungu muumba wa vyote, mwenye upendo, muweza wa yote na mjuzi wa yote yupo kweli au ni hadithi tu?



Wewe unadhani ni leo ndiyo nimeanza naye kumthibitishia uwepo wa Mungu!!,

Na isitoshe ni lazima mtu apate (mahubiri) au maelezo, vyovyote utakavyoyata, yatakayo mtosheleza ili aepukane na "ugonjwa" wa kupinga uwepo wa Mungu.

Tiba ya kwanza kabisa ni kujitambua wewe nani?, umekujaje hapa duniani? na je ulikuja kwa hiyari yako? na ulikuja kwa sababu ipi??, ukisha jibu hayo maswali ndipo unakwenda hatua yoyote inayofuata.

Hayo maswali nilikwisha muuliza huyo Kiranga mwanzoni kabisa alipoleta thread inayofanana na hiyo na hakujibu hata swali moja ikionyesha kwamba hajitambui na ndiyo maana anapinga kuwepo kwa mungu huku akiabudu na kunyenyekea sayansi kana kwamba Sayansi kwake ndiyo kila kitu.

Na isitoshe alipata kusema kwamba alipokuwa chuoni alizawadiwa (rewarded) A+ credit na prof, wake wa falsafa kwa kutoa hoja za kupinga uwepo wa Mungu, hoja zilizo konga akili za huyo prof, ambapo akamwambia asifanye mtihani wa falsafa kwani hoja zake zipo juu ya upeo wao!!


👆🏻Sasa huyo ndiye kiranga anaye sema hakuna Mungu na hayo ndiyo maelezo yake, mimi nilitaka kumjua huyo Prof, na chuo alichosoma ili tuone kama anasema kweli na hadi hii leo hajaleta huo ushahidi.

Kwa upande mmoja huyo prof,kamuharibu huyo ndugu yetu na ame "mbrain wash" sasa mzigo upo kwetu kumnusuru na kasumba hiyo ya kutoamini uwepo wa Mungu, nadhani kama ni kweli huyo prof, atakuwa mzungu??!!. Kwasababu wazungu wengine wanawazimu inayoweza kuambukiza Waafrika.
 
Mtoa hoja mwanzoni nilishangaa kichaga "Yesu Maria na Yosefu " ila ukiangalia kwa makini Mungu wa kweli hawezi kuandaa moto wa kuchoma watoto wake .Hayo mambo yalitungwa ili tuogope tupokee dini zao
 
Kutokujua chanzo chako isiwe kigezo cha kusema Mungu yupo.

Kiujumla maswali anayouliza Kiranga yamekuzidi upeo


Chanzo chako Mungu ndiyo kakitengeneza hivyo Yeye kimsingi ndiye aliyekuumba na Yupo ndiyo maana katuandalia kila kitu ili kusastain maisha yetu kwa muda fulani hapa duniani.


Hoja yake kuwa Mungu hayupo ni kutokana na shida na taabu zetu zinazo tukabili hapa duniani na anasema huyo Mungu mwenye huruma hayupo!!, sasa angalia hiyo point na muulize kwani duniani kuna shida na taabu pekee??, je, hakuna raha na starehe??, point ni hii kama kutokana na shida na taabu hakuna Mungu basi kutokana na raha na starehe Mungu atakuwepo.

Hoja yake hiyo ni "self contradictory" katika suala hilo na ni ya kupuuzwa.
 
Kwa wingi wa rehema nakuandikia maswali ambayo yanaulizwa mara nyingi na majibu yake kutoka kwangu.

1.Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu ndiye anaaminiwa na watu wengi kabisa kuwa yupo. Quran, Biblia, dini nyingi, falsafa zinamtaja huyu.

2. Mungu huyu yupo kweli?

Tukiangalia kimatiki, dhana ya Mungu huyu kuwapo ina tatizo la kimantiki, kubwa sana.

3.Tatizo gani la kimantiki?

Tatizo hilo ni kwamba, dhana ya kuwepo Mungu huyu inajipinga yenyewe.
.
4. Dhana hii inajipingaje?

Dhana hii inajipinga kwa sababu tunaambiwa, upande mmoja, Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, hana sababu ya kimantiki kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo, dhambi inawezekana kuwepo, matetemeko ya ardhi yanawezekana kuwepo, magonjwa yanawezekana kuwepo, kifo kinawezekana kuwepo, tsunami linawezekana kuwepo n.k, halafu upande wa pili tunaambiwa Mungu kauumba ulimwengu uwe unaruhusu mabaya hayo.

Huku ni kujipinga kusiko kwa kiungu. Ni kama mtu anakwambia kwamba katika jometri ya Euclid, duara haliwezi kuwa pembetatu, halafu akakuambia kuna pembetatu iliyo duara.

Ama amaekosea kusema pembetatu haiwezi kuwa duara, ama amekosea kusema kwamba kuna duara iliyo pembetatu.

Hawezi kuwa sawa pote.

5. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu hakutaka ulimwengu uwe na mabaya, ila shetani, uasi, dhambi ndizo zilifanya dunia iwe na mabaya?

Hilo litamaanisha Mungu aliumba ulimwengu unaoruhusu uasi, dhambi, ubaya kuwea kuwepo, kwa nini?

6. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu aliruhusu ubaya uweze kuwepo ili watu wawe na uchaguzi na uhuru?

Kwanza kabisa kwa nini uhuru na uchaguzi uwe muhimu kuliko kutokuwepo kwa mabaya?
Ukiwa na mtoto mchanga ambaye hana ujuzi sana, utampa maziwa na sumu ili tu awe na uhuru wa kuchagua? Hapana, utampa maziwa na kuficha sumu asiweze kuifikia. Sasa kwa nini Mungu katuachia watoto wake tuifikie sumu? Kwa nini hakuificha?

Pili, si kweli kwamba tuna uhuru wa kuchagua. Hatuchagui wazazi wetu, hatuchagui kabila letu, hatuchagui tutazaliwa wapi, hatuchagui tutazaliwa lini, hatuchagui tutakuwa na genes gani, hatuchagui tutakufa lini, hatuchagui tuzaliwe au tusizaliwe.

Hii habari ya kwamba tuna uhuru wa kuchagua mema na mabaya ni uongo. Kuna mengine yana mizizi katika genes, mengine ni sehemu ya socioeconomic background.

Tatu, kuna mabaya mengi hayahusiani kabisa na habari za uchaguzi wa mazuri na mabaya, mabaya kama majanga ya kiasili hayana uhusiano wowote na uchaguzi wa mazuri na mabaya.

7. Vipi kuhusu maandiko matakatifu yanayosema Mungu yupo?

Maandiko matakatifu ni jitihada za watu tu kujipangia maisha yao kwa namna inayoeleweka kwao, mengi yana mafundisho mazuri, lakini sehemu nyingi tunaona yanajipinga, yanatetea mabaya, yanaonesha kwamba yameandikwa na watu tu, kuhusu Mungu ambaye hayupo

8. Mbona watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu?

Kwanza kabisa, habari ya kwamba watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu ina mushkeli. Watu wengi wangeamini kweli kuwepo kwa huyu Mungu, ujambazi, uuaji, wizi, utapeli, dhambi nyingi sana zisingekuwepo. Kuwepo kwa mabaya haya kwa sana duniani kunaonesha watu wanapenda kujinadi kwamba wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini ndani kabisa, ama wanakubali kwamba hawajui vizuri habari hii au wanaikataa kabisa.

Pili, ulimwengu unatoka katika zama za ujinga na kwenda kwenye zama za elimu na maenddeleo ya habari.Kitu kuaminiwa na watu wengi hakuoneshi kitu hicho ni kweli. Kuna wakati watu waliamini jua linazunguka dunia, lakini sasa watu wengi wamejua dunia ndiyo inazunguka jua. Kwa hiyo kitu kuaminiwa na watu wengi hakumaanishi kuwa kitu hicho ni kweli.

9. Kama Mungu hayupo, ulimwengu umeanzaje? Unaweza kujibu swali hili ili kuonesha kwamba Mungu hayupo?

Sijui. Habari iliyo karibu zaidi kutueleza kuhusu mwanzo wa ulimwengu ni kuunganisha Albert Einstein's Relativity na Quantum Theory kupata theory mpya ya Quantum Gravity. Kwa sasa hatujaweza kupata mahesabu ya kuweza kuondoa singularities fulani.

Lakini hata kama naishia kusema tu sijui jibu la swali hili kimsingi, kutokujua huko hakuna maana kwamba sitajua jibu la uongo.

Nikijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, mtu akiniambia square root ya 2 ni 10 (ambayo ni kubwa kuliko 2), nitajua 10 si square root ya 2 hata kama sijui square root ya 2 ni nini.

Kijana wa miaka 20 akiwa hamjui mama yake mzazi, akajua mama yake mzazi ni lazima awe na umri wa zaidi ya miaka 20 (ili aweze kuwa amemzaa) halafu akaoneshwa mtoto kike wa miezi mitatu, akaambiwa huyu ndiye mama yako mzazi, atajua huyu si mama yake mzazi, bila hata kumjua mama yake mzazi ni yupi.

Kukubali Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye aliyeumba ulimwengu huu wenye kuweza kuwa na mabaya ni sawa na kukubali mtoto wa miezi mitatu ni mama mzazi wa mtu mwenye miaka 20

10. Sasa tufanye nini?

Tujifunze zaidi, tuchunguze zaidi, tutafute ukweli bila kupenda majibu rahisi rahisi. Tukubali majibu ya kweli hata kama hatuyapendi.

Majibu ya uongo ambayo ni wazi kabisa hayana logical consistency, tuyakatae.

*Angalizo, hapa naongelea umuhimu wa ujuzi, kwa misingi ya mantiki na ukweli. Sizungumzii imani per se. Imani ni sehemu muhimu ya utu na watu wanaruhusiwa kuamini wanavyotaka. Katiba ya nchi na mazimio ya kimataifa yanaruhusu uhuru wa kuabudu.
@mokaze kama kweli kuna sehemu umejibu maswali ya Kiranga, njoo tolea ufafanuzi hii Comment maana Kiranga kafafanua vizuri

Mungu wa namna hii aweza kuwepo kweli?
 
Soma Comment ya Kiranga niliyokutage hapo chini uelewe hoja yake vizuri
Chanzo chako Mungu ndiyo kakitengeneza hivyo Yeye kimsingi ndiye aliyekuumba na Yupo ndiyo maana katuandalia kila kitu ili kusastain maisha yetu kwa muda fulani hapa duniani.


Hoja yake kuwa Mungu hayupo ni kutokana na shida na taabu zetu zinazo tukabili hapa duniani na anasema huyo Mungu mwenye huruma hayupo!!, sasa angalia hiyo point na muulize kwani duniani kuna shida na taabu pekee??, je, hakuna raha na starehe??, point ni hii kama kutokana na shida na taabu hakuna Mungu basi kutokana na raha na starehe Mungu atakuwepo.

Hoja yake hiyo ni "self contradictory" katika suala hilo na ni ya kupuuzwa.
 
Huyo profesa hakumharibu Kiranga bali aliona uzito wa hoja zake ndio maana akampa hadi zawadi

Pia inaonesha ni jinsi gani alivuka viwango vya kufikiri na ujasiri wa kuuliza ndio maana profesa mwenyewe akaona hata mtihani aliotakiwa kufanya ni kama kumfundisha mtu mzima namna ya kutembea

Wewe unadhani ni leo ndiyo nimeanza naye kumthibitishia uwepo wa Mungu!!,

Na isitoshe ni lazima mtu apate (mahubiri) au maelezo, vyovyote utakavyoyata, yatakayo mtosheleza ili aepukane na "ugonjwa" wa kupinga uwepo wa Mungu.

Tiba ya kwanza kabisa ni kujitambua wewe nani?, umekujaje hapa duniani? na je ulikuja kwa hiyari yako? na ulikuja kwa sababu ipi??, ukisha jibu hayo maswali ndipo unakwenda hatua yoyote inayofuata.

Hayo maswali nilikwisha muuliza huyo Kiranga mwanzoni kabisa alipoleta thread inayofanana na hiyo na hakujibu hata swali moja ikionyesha kwamba hajitambui na ndiyo maana anapinga kuwepo kwa mungu huku akiabudu na kunyenyekea sayansi kana kwamba Sayansi kwake ndiyo kila kitu.

Na isitoshe alipata kusema kwamba alipokuwa chuoni alizawadiwa (rewarded) A+ credit na prof, wake wa falsafa kwa kutoa hoja za kupinga uwepo wa Mungu, hoja zilizo konga akili za huyo prof, ambapo akamwambia asifanye mtihani wa falsafa kwani hoja zake zipo juu ya upeo wao!!


Sasa huyo ndiye kiranga anaye sema hakuna Mungu na hayo ndiyo maelezo yake, mimi nilitaka kumjua huyo Prof, na chuo alichosoma ili tuone kama anasema kweli na hadi hii leo hajaleta huo ushahidi.

Kwa upande mmoja huyo prof,kamuharibu huyo ndugu yetu na ame "mbrain wash" sasa mzigo upo kwetu kumnusuru na kasumba hiyo ya kutoamini uwepo wa Mungu, nadhani kama ni kweli huyo prof, atakuwa mzungu??!!. Kwasababu wazungu wengine wanawazimu inayoweza kuambukiza Waafrika.
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
,wewe jamaa hatari sana
 
Sasa wewe unataka kumfundisha mungu? Mungu ni wahuruma na wafadhili ndio maana mpuuzi kama wewe uliekufuru kwa kiasi hichi na bado upo hao na hovyo hovyo shetani kaachwa kama wewe ,then kuhusu Abraham na uzao wake ebu kaesabu nyota zen chukua idadi ya waisraeli na waarabu +wakushi (waethiopia na baadhi ya jamii za Africa mashariki zenye nasaba zao Ethiopia ) according to rastafarian kuwa malkia wa Sheba alizaa na mfalme Solomon niambie kuwa watu hao ni wachache? Je unajua idadi ya nyota na hao watu?
 
Mtoa hoja mwanzoni nilishangaa kichaga "Yesu Maria na Yosefu " ila ukiangalia kwa makini Mungu wa kweli hawezi kuandaa moto wa kuchoma watoto wake .Hayo mambo yalitungwa ili tuogope tupokee dini zao
Swali dogo tuu kwako
Ukivuna mahidi, mabua huwa unayafanyia nini?
Tupo kwenye chumba cha mtihani, jipange mkuu, achakujipa matumaini yasiyokuwepo..muabudu Mungu mmoja acha ujanja ujanja..
 
Kushiba ni kubaya sana!!!......Wewe kijana unamdhihaki Mungu kisa unakula na kushiba vizuri na una afya njema ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii????
Kudhihaki Mungu sio kuuliza swali ambalo haulijui na kutaka watu wakusaidie kujua.
Hivi wewe unajua neno Dhihaka?
Usimjaze Mungu upupu.
Jamaa anauliza baadhi ya maswali ambayo yamemshinda kuelewa kwa Mungu wetu.
Unatakiwa kumjibu ili ajue zaidi atoke kwenye giza kama hili.
 
Huyo profesa hakumharibu Kiranga bali aliona uzito wa hoja zake ndio maana akampa hadi zawadi

Pia inaonesha ni jinsi gani alivuka viwango vya kufikiri na ujasiri wa kuuliza ndio maana profesa mwenyewe akaona hata mtihani aliotakiwa kufanya ni kama kumfundisha mtu mzima namna ya kutembea




Sisi sote tumepitia vyuo, hicho alichosema Kiranga ni uongo mkubwa kuliko, hata mtu ambaye hajaenda shule kabisa hawezi kukubali sembuse wana jf humu ndani!!😁😁, hata kama huyo prof, angalikuwa mjomba wake asingeweza kufanya hivyo kulinda hadhi na heshima yakee kitaaluma pia hadhi ya chuo kitaaluma (academic ethics), vipi tukio hilo kwa wanafunzi wenzake??, kuna maswali mengi mno katika tukio hilo kuliko majibu.

Huo ni uongo mkubwa katika njia ya kujitukuza na kujsifu mbele ya umma wa jf. eti mtu azawadiwe A+ nje ya chumba cha mtihani kwa kukanusha uwepo wa Mungu na anaambiwa asifanye mtihani kwa sababu hiyo tu!!!😁😁 vipi hiyo siyo dhuluma kwa wanafunzi wenzake??. Tafuteni uongo mwingine huo ume "backfire".
 
Back
Top Bottom