Wapo atheists kibao tu ambao wamekubali uwepo wa Mungu,
Kuwa atheist nikukataa uwepo wa Mungu, sasa atheist anayekubali uwepo wa Mungu ni contradiction.
Ni kama mke wa mtu ambaye hajaolewa, ni kama pembetatu iliyoduara.
Zaidi, watu kukubali dhana fulani si jambo lakulifanya jambo hilo kuwa kweli. Kuna watu wengi waliamini jua linazungukadunia, lakini hilo halikufanya jua lizunguke dunia.
Tuongee hoja, si watu.
Kuna msemo "small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas". Ukitoka kwenye ku discuss ideas, uka discuss watu, bila muktadha, unakwenda kwenye small minds
si jambo la ajabu(kama hili nalo la kubisha sema niweke list) ila cha kutafakari hapa,ni kwamba kama uthibitisho ndio ingekuwa ni hoja ya msingi kwa basi hili jambo lisingewezekana.
Uandishi wako mtu anayesoma neno bada ya neno anapata shida kukuelewa.
Your diction is jumbled, you are not conveying.
Unapoandika " ila cha kutafakari hapa,ni kwamba kama uthibitisho ndio ingekuwa ni hoja ya msingi kwa basi hili jambo lisingewezekana" hapo una maana gani? Sentensi imekaa ovyo kiasi kwamba hata kuijadili zaidi siwezi
Na ndiyo maana mara zote nakwambia kuwa suala la uwepo wa Mungu ni imani ndiyo ipo hivyo na si kwamba watu wameamua tu waamini kwa kukosa uthibitisho,
Unaweza kuthibitisha hili?
hivyo hizo hoja za kwamba amejificha sijui hakuna uthibitisho zinakuja baada ya kuliondoa suala la uwepo wa Mungu kwenye sehemu yake husika.
Kama unaongelea imani, huna haja ya kubishana na mtu.
Ukishabishana na mtu, maana yake umejitoa kwenye imani umeingia katika uthibitisho.
Sasa wewe huku haupo na wala kule haupo.
Kwenye imani haupo (kwa sababu unabishana na mimi jambo la imani, ukianza kubishana kuhusu jambo la imani umejiondoa kwenye iamni, unajiweka kwenye uthibitisho)
Kwenye imani haupo.
Kwenye uthibitisho nako hutaki, unasema hili ni jambo la imani.
Haupo kote, kwenye imani wala uthibitisho.
Unawayawaya kama popo aliyeondolewa uwezo wa kujua njia!
Hujui unaenda au unarudi.
Kama unaona hakuna lolote lenye kukufanya hadi uamini kuwa kuna Mungu,basi hapo ndio kwenye hoja ya msingi lakini sio kuja kutumbia kuwa hakuna uthibitisho.
Sitaki kuamini, nataka kujua.
Kama unaweza kuthibitisha Mungu yupo, thibitisha.
Kama unasema Mungu nisuala la imani na halihitaji uthibitisho, usiingie katika mjadala wa kutaka uthibitisho wa kuwepo Mungu.