Makapuku Forum

Makapuku Forum

7b57da4a75a912fa00cac9b5ae41120d.jpg
92d587c653c7736b94cee5a65f3ecacd.jpg
a67ad66366cee1213c9cf2d374184b55.jpg

Kansa yake ilisababishwa na kidole cha mguuni alichoumia wakati akicheza soka
Madaktari walimshauri akubali kufanyiwa operesheni kukiondoa lakini akakataa kutokana na Imani yake ya Urastafarah matokeo yake kansa ikasambaa na kusababisha kifo chake
"I'll shoot a tariff"
.........
Kansa mbaya sana,Mungu amuweke mahali pema
 
Mama Mchungaji. Umegusia Falsafa kabisa ya maisha yangu. Kwa vile nimeshafanikiwa kuacha kunywa pombe sasa bajeti yangu ina nidhamu sana. Lile fungu la 10 mimi hulitumia katika kusaidia wenzangu wenye shida moja kwa moja.

Ukienda huko mahospitalini ndo utaona bahati uliyonayo kwamba ungali na afya. Kuna binadamu huko wana magonjwa sugu na wengine wameshakata tamaa. Wengine ni masikini kabisa na wameshatelekezwa na familia zao. Wako huko mahospitalini wanasubiri kufa. Hawa hata ukimpa elfu moja unamuona anatoa machozi. Ukimpelekea matunda, sabuni, blanketi na hata mafuta ya kujipaka tu anakuona kama malaika. Na cha muhimu zaidi ni maongezi na upendo wa kibinadamu. Kuonyesha kuwa unawajali. Kuwapa matumaini kuwa Mungu bado Anawapenda. Kwamba waweke matumaini katika Yeye Aliyewafia. Kwamba kila kitu kitakuwa sawa.

Ninayo mifano mingi ya watu hawa na kusema kweli ndiyo wamebadilisha mtazamo wangu kuhusu maisha. Kuwasaidia hawa wenye shida kusema kweli ndiyo dini ya kweli.

Halafu mwalimu wangu mmoja hapa alitusisitiza sana kuwa kila siku angalau tufanye tendo moja jema kwa mtu mwingine - random act of kindness. Hii yaweza kuwa maneno ya kutia moyo, kusali pamoja na/au pesa kidogo. Mfano upo kwenye daladala na nyuma yako amekaa bibi kizee. Basi unamlipia nauli kwa siri. Na akifikiwa konda akimwambia bibi wewe nauli yako kuna mtu huko mbele kakulipia. Kitendo kidogo hiki lakini kinaweza kubadilisha siku ya mtu kabisa. Siku moja pale posta mpya kwenye matope mzee mmoja akakatikiwa na kandambili zake. Kwa pembeni pale kulikuwa na machinga anauza open shoes za ngozi. Basi nikamwambia mzee yule achague open shoes za ngozi imara. Alipigwa na butwaa na hakuamini mpaka akaanza kulia. Alichagua viatu imara, mimi nikamlipa yule mmachinga nikaondoka zangu. Ni matendo madogo madogo kama haya yanayotendwa kwa moyo mweupe bila kutegemea malipo wala fadhila ndiyo yanaweza kuuonyesha upendo wa Mungu kwa binadamu wenzetu. Na kupitia kwayo ndiyo tunaweza kupata ridhiko la kweli na thamani halisi ya maisha yetu. Asante sana mama Mchungaji kwa kutukumbusha wajibu huu mtakatifu. Mungu na Atusaidie tupunguze ubinafsi na kiburi cha kibinadamu. Good night!
Somo Kubwa.....thanks Shimba
 
Inaonekana uko makini sana katika kukosoa miili ya watu. It seems you are physically perfect Mr. Nyagei

Ni binti tu mjasiriamali na ana duka lake la nguo mtandaoni. Kuna picha amevaa bikini anauza. Kama ni toy kusema kweli sijui ila ni kibonge wa wastani mweupe na mrembo ajabu (at least kwangu). Ni mwanamke aliyekamilika. Mwanamke wa ndoto zangu. Shunie njoo unisaidie kumtetea huyu binti huku...
 
1984 - Andres Iniesta anazaliwa.

Kiungo mshambuliaji Barcelona na timu ya taifa ya Spain.

Mmoja kati ya viungo bora kabisa kuwahi kutokea katika uso wa Dunia. Kombinesheni yake na Xavi Hernandez ilikuwa ya kusisimua na iliyowaacha wapinzani wasijue wamkabe yupi wamuache yupi.

Ni mfungaji wa goli pekee lililoipa Spain kombe la Dunia mwaka 2010 pale Afrika ya Kusini.

Ni mmoja kati ya wachezaji wachache duniani ambao wameshinda kila kombe kwa ngazi ya vilabi na timu ya taifa.
happy birthday Andres iniesta
 
1981 - Mwanamuziki mashuhuri wa Regge na Mwanaharakati kutoka Jamaica, Robert Nesta ' Bob ' Marley anafariki Dunia.

Mmoja kati ya watu maarufu katika karne ya 20.

Alifariki kutokana na kansa. Aliacha watoto 13 kutoka kwa mama watatu.

Alizikwa kitaifa siku 10 baadae huko Kingston, Jamaica.

Alifariki akiwa na miaka 36, na kuwa mmoja kati ya watu maarufu kufariki kabla ya kufikisha miaka 50.

Pamoja na kwamba leo ni miaka 36 toka afariki lakini bado amebakia kuwa maarufu utadhani amefariki mwaka jana.
R.i.p Bob marley
 
1984 - Andres Iniesta anazaliwa.

Kiungo mshambuliaji Barcelona na timu ya taifa ya Spain.

Mmoja kati ya viungo bora kabisa kuwahi kutokea katika uso wa Dunia. Kombinesheni yake na Xavi Hernandez ilikuwa ya kusisimua na iliyowaacha wapinzani wasijue wamkabe yupi wamuache yupi.

Ni mfungaji wa goli pekee lililoipa Spain kombe la Dunia mwaka 2010 pale Afrika ya Kusini.

Ni mmoja kati ya wachezaji wachache duniani ambao wameshinda kila kombe kwa ngazi ya vilabi na timu ya taifa.
Happybirthday Iniesta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom