Wadau mnazimalizaje Weekend zenu kistaarabu?

Namshakende

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
844
Reaction score
2,184
Habari za jioni wana-JF,

Nimeona nije hapa jukwaani kuandika haya machache, huenda kuna wanaopitia hali kama yangu au waliowahi kuivuka wakashare nami namna ya kukabiliana nayo.

Mimi ni mtu ninayependa sana kuwa busy na majukumu yangu. Kipindi cha nyuma, nilikuwa na vitu vingi vilivyonipa burudani na kunichangamsha; nilikuwa mpenzi mkubwa wa kusikiliza Music [emoji444], kuangalia filamu, na hata kutoka mara moja moja. Upande wa pombe nilishaamua kuacha kabisa huko nyuma.

Hata hivyo, siku hizi mambo yamebadilika kabisa. Kila Ijumaa inapoingia , kwangu inakuwa ni mwanzo wa stress na boredom ya hali ya juu.

Yale mambo yote yaliyokuwa yananipa furaha mwanzo (muziki, muvi, mitoko) sasa hivi vimepoteza ladha kabisa, nikijaribu kuvifanya nahisi upweke na muda hauendi.

Hata upande wa mahusiano umekuwa na changamoto sana, kwani imekuwa ngumu kukutana na watu wenye uelewa na ukomavu wa akili unaoenda sawa na mimi.

Kimbilio langu pekee limebaki kwenye kazi. Hamu yangu kubwa kila weekend inakuwa ni kutamani Jumatatu ifike haraka ili nirudi kwenye majukumu yangu ya kila siku, kwa sababu huko ndiko akili yangu inapotulia.
 
Duh! Hongera aisee
Hata niwe sina pa kwenda.. nitalala.. sijawahi kutamani j3 ifike mapema 😀😀
 
Ukishaanza kujihisi kuwa uko mpweke tu hapo Tatizo ndo linapoanzia, upweke unaumiza kihisia na unaweza kukufanya usione thamani ya maisha kabisa kama Hali ikiendelea hivyo ni hatari Sana...Binafsi muda wowote ule naweza nikatoka na kwenda kufurahi, napenda kutembea sehemu mbalimbali hasa nje ya eneo ninaloishi, nikitembea ndo namaliza mambo yangu huko huko.
 
Piga puli..
Joking mkuu,

Nini kinakufanya uwe workaholic? Unakwepa Nini hasa?
Mimi nilishakumbwa na hii issue. Ila baada ya kujua nilikua nakimbia kitu, nilianza kupona na kuanza ku feel alive tena.

Ongea na watu wa karibu, Anza ku journal, ingia mtandaoni angalia picha zako za nyuma, tafta rafiki mliyepotezana. Just remember who you were before everyone taught you how you should be.
 
Hata upande wa mahusiano umekuwa na changamoto sana, kwani imekuwa ngumu kukutana na watu wenye uelewa na ukomavu wa akili unaoenda sawa na mimi.

With all due respect.
Ni nani amekuambia kuwa ww una ukomavu wa akili?.
Kimbilio langu pekee limebaki kwenye kazi. Hamu yangu kubwa kila weekend inakuwa ni kutamani Jumatatu ifike haraka ili nirudi kwenye majukumu yangu ya kila siku, kwa sababu huko ndiko akili yangu inapotulia.

kwa upande wangu. Weekend hata zingekuwa ni siku 3 zisingetosha.

Mbona vitu ni ving vya kufanya,
mm hata huo muda wa kuangalia Movie siupati.
 
Kuna jirani yangu mmoja yeye kila weekend akilewa lazima apigwa, sasa mtu kama huyu anamalizaje weekend kistaarabu..🙄
 
With all due respect.
Ni nani amekuambia kuwa ww una ukomavu wa akili?.

kwa upande wangu. Weekend hata zingekuwa ni siku 3 zisingetosha.

Mbona vitu ni ving vya kufanya,
mm hata huo muda wa kuangalia Movie siupati.
Watu hawapandi hata mchisha? Wapalilie wkend? Aargh! Au ni waizi? Wanatamani sku za kazi zifike warudi kazini kuiba 😀
 
mm kesho niko free ila nina vi-ratiba viwili hiv. Nadhan jion ndio ntatulia.
Nikikaa bar jion kuangalia mpira bas siku ishaisha.

Jpili kanisan, then kurud home na kufanya kazi mbili tatu za kihome na kupumzika.

Sasa siku moja (hasa j2) yenye masaa machache ya free hivi haitoshi.

Waweke weekend ziwe 3 😊😊😊😊😊
 
Toka, nenda sehemu nunua nyama ya nguruwe na maji baridi, pawe na pisi unashangaa vichuguu
 
Habari za jioni wana-JF,

Nimeona nije hapa jukwaani kuandika haya machache, huenda kuna wanaopitia hali kama yangu au waliowahi kuivuka wakashare nami namna ya kukabiliana nayo.

Mimi ni mtu ninayependa sana kuwa busy na majukumu yangu. Kipindi cha nyuma, nilikuwa na vitu vingi vilivyonipa burudani na kunichangamsha; nilikuwa mpenzi mkubwa wa kusikiliza Music [emoji444], kuangalia filamu, na hata kutoka mara moja moja. Upande wa pombe nilishaamua kuacha kabisa huko nyuma.

Hata hivyo, siku hizi mambo yamebadilika kabisa. Kila Ijumaa inapoingia , kwangu inakuwa ni mwanzo wa stress na boredom ya hali ya juu.

Yale mambo yote yaliyokuwa yananipa furaha mwanzo (muziki, muvi, mitoko) sasa hivi vimepoteza ladha kabisa, nikijaribu kuvifanya nahisi upweke na muda hauendi.

Hata upande wa mahusiano umekuwa na changamoto sana, kwani imekuwa ngumu kukutana na watu wenye uelewa na ukomavu wa akili unaoenda sawa na mimi.

Kimbilio langu pekee limebaki kwenye kazi. Hamu yangu kubwa kila weekend inakuwa ni kutamani Jumatatu ifike haraka ili nirudi kwenye majukumu yangu ya kila siku, kwa sababu huko ndiko akili yangu inapotulia.
Nunua shamba uwe unaenda kulima weekend. Au fungua biashara uwe unaenda kupambana na wateja weekend. Jibu la tatizo lako ni tafuta cha kufanya. Kama umekamilika kiakili na kimwili huwezi kukosa ha kufanya. Yaani hata kuzurula huwezi? Kama una gari weekend drive mpaka Bagamoyo au Kibiti keshokutwa Kisarawe au Kimbiji.
 
Habari za jioni wana-JF,

Nimeona nije hapa jukwaani kuandika haya machache, huenda kuna wanaopitia hali kama yangu au waliowahi kuivuka wakashare nami namna ya kukabiliana nayo.

Mimi ni mtu ninayependa sana kuwa busy na majukumu yangu. Kipindi cha nyuma, nilikuwa na vitu vingi vilivyonipa burudani na kunichangamsha; nilikuwa mpenzi mkubwa wa kusikiliza Music [emoji444], kuangalia filamu, na hata kutoka mara moja moja. Upande wa pombe nilishaamua kuacha kabisa huko nyuma.

Hata hivyo, siku hizi mambo yamebadilika kabisa. Kila Ijumaa inapoingia , kwangu inakuwa ni mwanzo wa stress na boredom ya hali ya juu.

Yale mambo yote yaliyokuwa yananipa furaha mwanzo (muziki, muvi, mitoko) sasa hivi vimepoteza ladha kabisa, nikijaribu kuvifanya nahisi upweke na muda hauendi.

Hata upande wa mahusiano umekuwa na changamoto sana, kwani imekuwa ngumu kukutana na watu wenye uelewa na ukomavu wa akili unaoenda sawa na mimi.

Kimbilio langu pekee limebaki kwenye kazi. Hamu yangu kubwa kila weekend inakuwa ni kutamani Jumatatu ifike haraka ili nirudi kwenye majukumu yangu ya kila siku, kwa sababu huko ndiko akili yangu inapotulia.
At least umepata kusudi sio Kila kitu Kwa Kila mtu Kila mmoja anapata kusudi Kwa njia tofauti so don't stress wikiendi tumia kujifunza tu zaidi
 
Pombe umeacha sawa,
Madem akili bado sawa,
Music na move haumo hiyo ni fresh kabisaa na hongera kwa hiyo hatua..

Sa fanya hivi kesho amka saa mbili tafuta maji mengi fanya usafi ndani anza na kufuta kuta, deki kuanzia chumban had seblen futa hadi nje siku ya kesho imeisha. Jpili fua kuanzia mashuka, manguo, vitambaa vya makochi, mapazia uchoke ulale ukutane na hiyo jtatu unayoitamani maana wewe n mfanyakazi mzuri sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom