Makapuku Forum

Makapuku Forum

1992 - Thibaut Courtois anazaliwa.

Kipa namba 1 wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji.
cbeed171403b321befcca1af0216713f.jpg
6bddd109333c7f5a2a23c04b4d3112e4.jpg
3b75e4c87a1cd39179fcb3c11ca31b08.jpg

Ndiye aliyemfukuza Prtr Cech pale daraja ni baada ya kungara Atletico Madrid alipopelekwa kwa mkopo hivyo kurudisha
Pia anamsugulisha benchi Simon Mignolet wa Liverpool timu ya Taifa Ubelgiji
...
..
 
1981 - Mwanamuziki mashuhuri wa Regge na Mwanaharakati kutoka Jamaica, Robert Nesta ' Bob ' Marley anafariki Dunia.

Mmoja kati ya watu maarufu katika karne ya 20.

Alifariki kutokana na kansa. Aliacha watoto 13 kutoka kwa mama watatu.

Alizikwa kitaifa siku 10 baadae huko Kingston, Jamaica.

Alifariki akiwa na miaka 36, na kuwa mmoja kati ya watu maarufu kufariki kabla ya kufikisha miaka 50.

Pamoja na kwamba leo ni miaka 36 toka afariki lakini bado amebakia kuwa maarufu utadhani amefariki mwaka jana.
7b57da4a75a912fa00cac9b5ae41120d.jpg
92d587c653c7736b94cee5a65f3ecacd.jpg
a67ad66366cee1213c9cf2d374184b55.jpg

Kansa yake ilisababishwa na kidole cha mguuni alichoumia wakati akicheza soka
Madaktari walimshauri akubali kufanyiwa operesheni kukiondoa lakini akakataa kutokana na Imani yake ya Urastafarah matokeo yake kansa ikasambaa na kusababisha kifo chake
"I'll shoot a Shariff"
.........
 
Ishi na watu kwa wema utafurahia muziki

Najua tumekuwa na wakti mzuri na tunapoenda kuimaliza Jumatano hii basi kama kawaida Makapuku nawakaribisha katika ka-kipengele haka ka ala za muziki na hasa tukijikita katika udonoaji na wadonoaji wa gitaa.

Kwa wapenzi wa muziki wa dansi miaka 20 nyuma, na wanaofuatilia miziki ya bakulutu, bendi ya Maquis Original ni bendi yenye umaarufu mkubwa hapa nchini ikiundwa na wanamuziki wengi toka Kongo na mmoja wao ni mpiga gitaa maarufu Dekula Kahanga almaarufu Vumbi. Mitindo kama Zembwela na Sendema haiwezi kukutoka kiurahisi.

Sikiza vibao cha Ngalula, Mayanga, Makumbele, Karubandika na vingine vingi katika mitindo ya Sendemaa na Zembwela. Gitaa utakalosikia linamuongoza muimbaji awe ni Tshimanga Assossa au Kasaloo basi ni la nguli Dekula Kahanga.

Bado yupo na anafanya muziki wake nchini Sweden akiwa na band yake ya Dekula Band.

Hapa nakuwekea baadhi ya nyimbo alizoweza kuzicharaza na kuzifanya zikavutia zaidi.

FYI: Upigaji wake mzuri umechangiwa zaidi na kufuatisha mipigo ya Nguza Viking (yupo jela sasa akitumikia adhabu ya maisha gerezani)

Dekula anaamini katika kuishi vizuri na watu, kwani huwezi kujua maisha yatakupeleka wapi.

hapa najiuliza nikuache na Ngalula au nitupie clip ya YouTube ambayo anacharaza baadhi ya nyimbo zake, isiwe ishu, nakuacha na zote mbili, suala la kukumalizia MB zako mpenzi msomaji liko nje ya uwezo wangu (joke)





 
Hakuna kitu kinacholeta faraja na furaha kama kusaidia wahitaji hata kama huna kitu,kushare kidogo ulichonacho na wale ambao hawana kabisa imagine unaenda hospital kumtembelea ndugu yako amelazwa mnajikuta mko 20 mmezunguka kitanda ,lakini next bed kuna mtu kapata referal kuja muhimbili hana ndugu hebu sogea tumia muda nae,ongea nae mpe kidogo ulichonacho aaah huwezi amini utakuwa unatafuta safari a kutembelea watu wa aina hii na hutapungukiwa,nauli,cha kuwapa hata neno la kuwatia moyo .hata majumbani wapo wengi wanahitaji faraja ,kutiwa moyo,kusikilizwa pata muda wa kuwaona watu hawa wapo wengi sana Mungu atutie nguvu

Nehemia 8

10b....furaha ya BWANA ni nguvu zenu.

Haleuiya

MATENDO YA MITUME 20

35.Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge,na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu ,jinsi alivyosema mwenyewe. Ni heri kutoa kuliko kupokea
Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom