Makapuku Forum

Makapuku Forum

NUKUU NO 1#

Asilimia 90% ya wanasiasa ndio wanaosababisha wanasiasa wenzao ambao ni 10% iliyosalia, kuporoka kwa hadhi zao mbele ya Jamii.

Maneno haya yalisemwa na Henry Alfred Kissinger.
Kissinger alizaliwa Mei 27,1923. Ni mwanadiplomasia wa Marekani na mtaalamu wa siasa.
Amewahi kuitumikia nchi kwa wadhifa wa mshauri wa masuala ya ulinzi na usalama na baadaye, waziri wa mambo ya nje wa Marekani katika tawala za Rais Richard Nixon na Gerald Ford.
Ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa Marekani kuondoa vikosi vyake nchini Vietnam na kuzawadiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1973
Huyo ndio shujaa sasa!....najua amlishakufa R.I.P
 
1996 - Tupac Amar Shakur anafariki Dunia.

Alikuwa ni rapa wa muziki wa Hiphop toka nchini Marekani.

Anachukuliwa kama mmoja kati ya rapa mwenye ushawishi na bora wa wakati wote.

Ni miongoni mwa watu wachache ambao wameendelea kuwa maarufu hata baada ya miaka mingi kupita baada ya vifo vyao kando ya Mwanamapinduzi Ernesto Che Guevara na mwanamuziki wa regge Bob Marley.

Tupac aka Makaveli alifariki baada ya kupigwa risasi kadhaa wiki moja baadae ndio anafariki baada ya kiasi kikubwa sana cha damu kuvuja ndani ya mwili.

Pamoja na yote hayo kuna wanaoamini Tupac hajafa, Alifeki kifo chake ili apunguze kufatiliwa.


Kwa wale wanaoamini kuwa Tupac amefariki wanaamini Big ndio aliyemuua baada ya kutoelewana kisa Tupac alitembea na mwanamke wa Big Notorius aliyitwa Faith Evans.

Pia kuna wanaoamini Tupac aliuwawa na bosi wake na mmiliki wa Death row Inc. ambaye ni Suge Knight.

Baba wa ubatizo wa Tupac alifariki na kuzikwa Tanzania, alijulikana kama Geronimo Pratt.

Leo ni miaka 20 toka 2pac afe bado anabaki kama rapa bora wa wakati wote.

Pumzika amani 2pac.
Rest in peace king pac...

Makaveli the don
 
NUKUU NO 4#

Katika Tanganyika tunaamini kwamba ni shetani peke yake,
Mtu asiye mcha Mungu ndiye anayeweza kutumia rangi ya ngozi ya mtu kama kigezo cha kuamua kumlahisishia anapata haki zake za msingi

Haya yalisemwa na Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alitamka maneno hayo wakati akihutubia mbele ya Gavana wa kikoloni wa Uingereza, Richard Gordon Turnbull, wakati wa mkutano wa baraza la kutunga sheria (Legco) kabla hajakasimiwa madaraka waziri mkuu wa Tanganyika, mwaka 1960.
Huyu mzee popote alipo abarikiwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom