Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Mpito wa Mali, Assim Goita ameshambuliwa na Wanaume wawili mmoja akiwa amebeba kisu baada ya kumaliza Ibada ya Sikukuu ya Eid Al-Adha Msikitini, Bamako.

Ikulu ya Mali imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Rais yupo salama na Watu hao walidhibitiwa na Walinzi wa Rais na kwamba uchunguzi unaendelea.

Mashuhuda wanasema wameona damu kwenye eneo la tukio lakini bado haijajulikana damu hiyo ni ya nani.
Screenshot_20210720-204244_GBInsta.jpg
 
Wananchi wa eneo la Lusanga kata ya Kwamagome wilayani Handeni mkoani Tanga wameandamana na kuzuia msafara wa Mkuu wa Wilaya wakati anaelekea mgodi wa dhahabu wa Mamgambazi ili kushinikiza kupatiwa eneo kwajili ya kujenga shule na kufunguliwa njia ya mifugo.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi ambapo zaidi ya wananchi 150 walijitokeza na kufunga barabara ya kuelekea Morogoro kuzuia msafara wa Mkuu wa Wilaya na kueleza kuwa shida yao ni kupatiwa eneo kwaajili ya ujenzi wa shule lakini pia kufunguliwa njia ya mifugo kwenye eneo ambalo amepewa muwekezaji bila wao kushirikishwa.

Mmoja wa wananchi hao Rashid Rajabu amesema mpaka sasa wameidhinishiwa heka 10 baada ya aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo, Godwin Gondwe kukaa kikao baina ya wananchi, mwekezaji na wao kuhusu kutafuta ufumbuzi ila wao hawahitaji heka hizo wanachohitaji ni kuangaliwa upya mipaka.

Ameongeza kuwa heka 10 haziwatoshi kujenga majengo ya shule kwani kuna madarasa, nyumba za walimu, mashamba na viwanja vya mpira hivyo kwa kuwa wanaamini eneo lao halijauzwa kihalali wanalihitaji kwaajili ya shughuli hizo.
Screenshot_20210720-204419_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom