Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210720-093851_Instagram%20Lite.jpg
 
“Hayati Magufuli alikuwa anafanya kazi sana, alikuwa analala akiwa na usingizi tu kama hana basi alikuwa halali na asipolala hata Sisi hatuwezi kulala"

“Hayati Magufuli ni Mtu alipenda sana Vijana aliwaamini na sio tu sisi tuliokuwa pale ofisini, nyie Clouds Mashahidi mnafahamu namna alivyokuwa anawapenda, alikuwa Mlezi, Rafiki, Mtani sana, Mimi Mkinga yule Msukuma na ni watani, mkimaliza kazi anakutania sana”———Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kwenye Clouds360 ya clouds tv
Screenshot_20210720-125244_GBInsta.jpg
 
“Ile tozo ambayo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anaiita 'Tozo za Mshikamano' dhamira yake ilikuwa Serikali kuanza safari ya kujenga Barabara za lami Vijijini hili jambo ukikaa huku Dar es Salaam unaweza kuliona kama dogo lakini Vijijini huko hakuna Barabara”

“Songea kuna kijiji ambacho kuna sehemu hakuna mawasiliano ya Barabara TANROADS waliweka lami ya kawaida sana tena sehemu korofi, huwezi amini inapofika Saa 11 jioni wanakijiji wote wanakaa pale ndio sehemu yenye staha, ndio sehemu yao ya kutalii"

“Serikali imeamua kuanza kujenga Barabara za lami vijijini, wakaamua kuweka tozo ya mshikamano ili kupanua wigo wa tozo kwahiyo hii tozo imelenga kwenye eneo hilo"

“Serikali ilikusudia kwenye tozo ya miamala na ile ya laini za simu palikuwa panatarajiwa karibu Trilioni 1.6 na Trilion 1 zilikuwa zinatakiwa zitoke kwenye miamala, hizi tozo zilitakiwa ziende zikajenge Barabara na vituo vya afya vijijini”———Msemaji Mkuu wa Serikali
Screenshot_20210720-125546_GBInsta.jpg
 
“Rais Samia anafanya kazi sana, ukiona anapanda ndege anashuka unaweza ukahisi ni maisha mazuri lakini hapumziki, tuna bahati ya kuwa na Viongozi wanaojitoa kwa ajili ya Watanzania, Wachapakazi, Wacha Mungu, wanawapenda Wananchi wao na wanafikiria kuhusu Watanzania"

“Ndoto za Hayati JPM kuhakikisha kila kata ina maji, vituo vya afya, barabara zinatimizwa, hakuna kazi iliyosimama, Bil 23.8 kwa ajili ya elimu bure zinaendelea kutolewa na hakuna Mtoto aliyeendelea kutozwa ada hata baada ya JPM kufariki"———Msemaji Mkuu wa Serikali
Screenshot_20210720-125707_GBInsta.jpg
 
“Hayati JPM aliacha miradi ambayo Rais Samia alisema lazima imalizike na mingine ianze, mfano Hayati JPM alianza mradi wa kujenga reli Dar hadi Morogoro na ilifika 86% ila sasa mradi umefika zaidi ya 92% na mwezi November treni ya umeme itafanyiwa majaribio"

“Ujenzi wa SGR umefikia 92% na mwezi November,2021 treni ya majaribio itatoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na kutoka Morogoro kwenda Singida ambako ujenzi wake umefikia 65 %”

“Reli kutoka Mwanza - Isaka fedha ya awali TZS Bilioni 372 imeshatolewa na kazi inaendelea, Rais Samia amewaagiza TRC kuanza maandalizi ya kutafuta Wakandarasi wa kuanza kujenga kutoka Makutupora - Tabora - Isaka - Kigoma - Kaliua - Mpanda- Kalema”———Msemaji Mkuu wa Serikali
Screenshot_20210720-125822_GBInsta.jpg
 
“Idara ya Habari MAELEZO ipo kwenye michakato ya awali ya kuanzisha Chaneli ya Televisheni na Kituo cha Redio ambazo zitakuwa zinatoa taarifa za Serikali tu, hii itawafanya Wananchi kupata taarifa za Serikali muda wote, najua mtaniambia TBC, TBC inafanya majukumu ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali”———-Msemaji Mkuu wa Serikali
Screenshot_20210720-130036_GBInsta.jpg
 
Wiki moja baada ya bilionea Richard Branson wa Virgin Atlantic kwenda space, bilionea mwenzake Jeff Bezos wa Amazon naye anakwenda space kwa kutumia roketi yake.

Bezos anakwenda space leo Jumanne, Julai 20, 2021 kwa roketi yake iliyotengenezwa na kampuni yake binafsi ya space iitwayo Blue Origin.

Bezos atafuatana na kaka yake na abiria wengine wawili mwanamama Wall Funk (85) ambaye anadhihirisha kuwa wanawake wanaweza kufika space na kijana wa miaka 18 Oliver Daemen ambaye anakuwa mtu mwenye umri mdogo kufika space.
Screenshot_20210720-130240_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom