Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210721-070239_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210721-070253_Opera%20Mini.jpg
 
Waandaaji Prime Time Promotions, Clouds Media Group pamoja na Management ya Mwimbaji Staa wa Congo DR. Fally Ipupa wametoa taarifa rasmi ya ahirisho la show za Fally Ipupa zilizokua zifanyike weekend hii Jijini Dar es salaam Ijumaa July 23 na Jumamosi July 24 Jijini Mwanza, taarifa hiyo imesema ni kutokana na changamoto zilizoshindwa kuepukika.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Edward Lusala ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi imesema "Wapenzi, Jamaa, Marafiki na Mashabiki tunachukua nafasi hii kuomba radhi kwa wale wote ambao walitenga ratiba yao ili kuwa sehemu ya matukio haya, tarehe mpya za show zitatangazwa baadae, utaratibu wa walionunua tiketi na kufanya booking ya meza utafafanuliwa kwa mawasiliano kati yao na kamati husika"

Bora walivyosogeza mbele
Screenshot_20210721-173443_GBInsta.jpg
Screenshot_20210721-173605_GBInsta.jpg
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema tayari chanjo ya Covid 19 ipo Tanzania hivyo anayetaka kuchanjwa ni ruksa kwenda kupata chanjo hiyo ili apate kinga na zimsaidie kusafiri kwenda kwenye Mataifa ambayo yanataka wanaokwenda wawe wamepata chanjo.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hii leo kwenye Baraza la Eid lililofanyika kwenye Msikiti wa Mtoro Jijini Dar es salaam ambapo AyoTV na millardayo.com zitakupatia maelekezo hivi karibuni kuhusu Hospitali zinakopatikana chanjo hizo.
Screenshot_20210721-173927_GBInsta.jpg
 
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema tayari Tanzania imepokea chanjo za aina mbili au tatu za corona ili Watanzania ambao wamekwama kusafiri kwenda kwenye Nchi zenye masharti ya kwenda ukiwa umechanjwa chanjo ya corona.

"Serikali ilikaa chini na kutafakari na kugundua kwamba tuna Watanzania wengi ambao wana shughuli mbalimbali ikiwemo kwenda HIJA kwenye masharti ya kwenda ukiwa umechanjwa, kuna Watanzania wanafanya biashara na Nchi mbalimbali zenye masharti hayohayo, kuna wengine mna Ndugu mnataka kuwatembelea kwenye Nchi ambazo zinataka Watu waliochanjwa"

"Mh. Rais wetu Samia Suluhu Hassan alisema tukae pamoja tutafakari, hawa Watanzania wanaotaka kwenda kote huko wanakwendaje? basi maamuzi yakafikiwa kwamba basi tulete angalau chanjo kadhaa hapa Madaktari fanyeni utafiti wa chanjo nzuri ambayo wenzetu wamechanja hawajapata madhara maana tumesikia nyingine zinagandisha hela nyingine zinaleta madhara ndio tukazipata hizo chache za aina kama mbili au tatu tu kati ya zote"

"Tukasema tuzilete hapa Nchini anayetaka achanjwe, kama unaona mwakani ni muhimu kwenda Hija basi fursa unayo hapahapa ndani, pia kama una Watoto wanasoma huko nje una ndugu zako na Nchi hiyo inataka waliochanja basi fursa ipo ndani ya Nchi usihangaike, tunaambiwa wengine wanakimbilia Afrika Kusini, Dubai au China sasa tukasema tusiwatie gharama Watanzania" ———
Screenshot_20210721-174245_GBInsta.jpg
 
Club ya Azam FC imemsajili kiungo wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna akitokea Club ya Gor Mahia ya Kenya ambapo huu unakuwa usajili wa nne wa Azam FC kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa 2021/22, wengine waliosajiliwa ni Edward Manyama, Charles Zulu na Rodgers Kola.
Screenshot_20210721-174443_GBInsta.jpg
 
Hizi ni picha kutoka eneo la tukio leo Mwanza zikionesha Polisi na magari ya Polisi baada ya kufunga barabara ilipo Hoteli ambayo ukumbi wake ulipangwa kutumika leo kwa kongamano la Katiba Mpya lililoandaliwa na CHADEMA.

Polisi waliojihami pia wameizingira hoteli hiyo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na wengine 11 wamekamatwa, updates zaidi kukujia.
Screenshot_20210721-174629_GBInsta.jpg
Screenshot_20210721-174651_GBInsta.jpg
Screenshot_20210721-174708_GBInsta.jpg
Screenshot_20210721-174724_GBInsta.jpg
Screenshot_20210721-174740_GBInsta.jpg
 
Makampuni mengine sita ya Tanzania yamepata idhini ya kuuza Maharage ya Soya nchini China na hivyo kuifanya idadi ya Makampuni ya Tanzania yanayoruhusiwa kuuza maharage ya soya katika soko la China kufikia 72.

Itakumbukwa Mwezi June mwaka huu Ubalozi wa Tanzania nchini China ulitangaza Makampuni 16 ya Tanzania ambayo yalipewa kibali cha Serikali ya China kuuza maharage ya soya katika Soko la China na ikafanya idadi ya Makampuni ya Tanzania yenye idhini ya kuuza maharage ya soya China kufikia 65.
Screenshot_20210721-175022_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom