Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe leo amefanya mkutano na Waandishi wa Habari Mwanza na kusema Chama hicho kinalaani Polisi kuvunja kongamano la BAVICHA kuhusu Katiba mpya juzi na kusema wameamua kama Chama kwamba wataendelea kufanya kongamano hilo wiki hii hapohapo Mwanza kwakuwa ni haki yao na kama Polisi wakitaka wamkamate yeye.

“Jumatano tuna kongamano la Katiba walete vikosi kila sehemu, baada ya Kongamano tutaanza mikutano ya hadhara Nchi nzima hatutasubiri vibali”———MBOWE
Screenshot_20210719-150955_GBInsta.jpg
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe leo ameongea na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza kuhusu Polisi kuzuia kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana CHADEMA kuhusu hitaji la Katiba Mpya ambapo pia mambo mengine aliyoyazungumza ni swala la utoaji wa chanjo ya covid-19 kwa Watanzania akimuomba Rais Samia afanye swala la chanjo hiyo kuwa lazima na sio hiyari.

“Serikali inasema chanjo ya Covid-19 ni hiari ya Mtu..... Mtu akatayependa ndiye apewe, huu sio utaratibu wa WHO, Nchi za Wenzetu chanjo ni lazima, tunamuomba Mama Samia aweke utaratibu wa chanjo kuwa lazima na inapaswa itolewe kwa kila Mtu, huu ugonjwa unaua”

”Mgonjwa wa Covid-19 ukilazwa gharama ni zaidi ya Tsh. Milioni 10 kwa wiki mbili, nimeuguza Ndugu yangu Hospitali pale Moshi gharama ni kubwa, kwa siku anatumia mitungi minne kila mtungi ni Elfu 30, ni Watanzania wangapi wanamudu?, gharama zinapaswa kubebwa na Serikali kwakuwa WHO imetangaza kuwa huu ugonjwa ni janga la Taifa” ——— Freeman Mbowe.
Screenshot_20210719-203300_GBInsta.jpg
 
Baada ya miezi 16 ya Night Clubs kufungwa kutokana na corona Nchini Uingereza, hatimaye zimefunguliwa na hizi ni picha za Jumapili usiku watu wakila raha.

Hii imetokana na Serikali ya Uingereza kutangaza kuondoa masharti yote ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona ambapo hata hivyo uamuzi huu umepingwa na Wanasayansi na Vyama vya Upinzani wakisema kuwa itaiweka Nchi hatarini.

Kuanzia saa sita usiku Night Clubs ziliruhusiwa kufunguliwa tena huku kanuni za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kama kuvaa barakoa, kuweka umbali wa mita moja na nusu baina ya Watu na kufanya kazi kutoka nyumbani zote zimeondolewa.

Waziri Mkuu Boris Johnson ameutetea uamuzi wa Serikali yake na kusema———“Ikiwa hatutafanya sasa, basi tutakuja kufungua miezi ya msimu wa baridi wakati virusi vitakapokuwa vinasambaa kwa kasi zaidi”

Licha ya kuondolewa vikwazo Waziri Mkuu Johnson amewataka Wananchi wa Uingereza kuendelea kuwa waangalifu.
Screenshot_20210719-203801_GBInsta.jpg
 
Wakati aina mpya ya kirusi cha corona kiitwacho Delta ikiripotiwa nchini Rwanda, Serikali ya Nchi hiyo imeanza mkakati wa kuwapima Raia wake kuanzia vijijini hadi mjini.

Sambamba na hilo pia Serikali ya Rwanda inakusudia kutoa vyakula kwa familia zilizoathiriwa na agizo la kubaki majumbani ambalo limewekwa kwa muda wa siku kumi kuanzia Jumamosi iliyopita ili kukabiliana na corona.

Serikali ya Rwanda imesema licha ya kuweka agizo la kutotoka nje kwa muda wa siku kumi katika mji mkuu Kigali na katika Wilaya nyingine nane zenye maambukizo mengi, bado zoezi la kuwapima Wananchi wengi kadri inavyowezekana litasaidia kubaini ni kwa kiwango gani virusi vya Corona vimesambaa nchini humo.
Screenshot_20210719-203953_GBInsta.jpg
 
Baada ya uamuzi wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wa kutaka tozo za miamala ya simu kuangaliwa upya, CCM imeishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia namna gani zitafanya mapitio upya ya Sera na sheria za kodi ili kuliweka vyema jambo hilo.

Akizungumza leo Jumatatu Julai 19, 2021 Katibu wa Itikadi siasa na Uenezi Shaka wa CCM, Hamdu Shaka amesema kwa mara nyingine Rais Samia amedhirisha hekima, usikivu wake, uzalendo, umakini katika utendaji wake.
Screenshot_20210719-204425_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Amos Makalla amesema toka janga la moto lilipotokea kwenye Soko la Kariakoo jumla ya wafanyabiashara 2,054 wamehamishwa na kupelekwa katika masoko mengine ikiwemo Kisutu na Machinga Complex.
Screenshot_20210719-204648_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom