Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakazi wa Jiji la Dar es salaam na Wakazi wa Jiji la Mwanza hawatoboreka weekend hii sababu wanayo sehemu ya kwenda, sababu wanae wa kwenda kumuona baada ya miaka mingi bila kumuona na kuishia kumtazama kwenye TV tu.

Sasa ni rasmi kwamba Mwimbaji Staa mzaliwa wa Congo Fally Ipupa atatumbuiza Jijini Dar es salaam Ijumaa hii July 23 kwenye Hoteli ya Serena na kisha jumamosi July 24 atatumbuiza Mwanza kwenye venue ya Elevate iliyopo Malaika Beach Resort.

Screenshot_20210720-143207_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amepiga marufuku mikusanyiko yoyote ambayo sio ya lazima mkoani humo katika jitihada za kudhibiti ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

RC Gabriel amesema wataruhusu misiba tu na ibada lakini mikusanyiko mengine yote haitoruhusiwa bila kuwa na kibali maalum.
Screenshot_20210720-203916_GBInsta.jpg
 
Twenzetu Kigoma ndio maneno mawili ya mwanzo yanayotumika sana kwa sasa kuelekea mechi ya Simba vs Yanga itakayochezwa July 25 2021 Lake Tanganyika Stadium Kigoma, wanasema raha ya kwenda 89.3 Kigoma sio ndege wala basi, raha uende na Treni.... ujionee uzuri wa Tanzania na ushibe experience ya kusafiri umbali mrefu kwa treni ndani ya ardhi ya Tanzania.

Hata wenye magari yao binafsi hawatoyatumia kusafiri kwenda Kigoma, Shirika la Reli Tanzania limesema tickets zinanunulika kwa wingi "imagine uko treni moja, behewa moja na Watu wako mkila na kunywa, ndani ya Treni kuna Bar, usalama wa kutosha, clubs, perfomances kutoka kwa DJ's, Chege, Juma Nature, G Nako, Profesa J, Sholo Mwamba, Madee, Linah, Luludiva, Aslay na wengine"

TRC ambayo imeshirikiana CLOUDS MEDIA GROUP kwenye safari hii, imesema tickets bado zinaendelea kuuzwa kwa 100000 kwa daraja la tatu, laki na elfu ishirini kwa daraja la pili kukaa na shilingi laki moja na elfu hamsini kwa daraja la pili lenye sehemu ya kulala ambapo unaweza kununua ticket yako kwenye booking.trc.co.tz au fika Stesheni Dar es salaam Kamata, Dodoma, Morogoro na Tabora.

Safari itaanza Ijumaa tarehe 23 July na kufika Kigoma July 24 na itageuza baada ya mechi hiyo July 25.
Screenshot_20210720-204034_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Polisi nchini limesema katika kipindi cha miezi miwili ya May na June mwaka huu limefanikiwa kuwakamata Wahalifu 5429 waliohusika kutenda uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo mauaji.

“Waliokamatwa kwa kujihusisha na mauaji ni 275 kati yao waliokamatwa kutokana na mauaji ya wivu wa kimapenzi ni 21, imani za kishirikina ni 23 na 231 ni kutokanana na sababu mbalimbali ikiwa na pamoja na kujitafutia kipato kwa njia za uhalifu”
Screenshot_20210720-204140_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom