Hatakiwi kuvumilia mwanamke juu ya madhira na mahudhi ya mwanaume mshenzi ambae hajali familia yake wala hana mapenzi na mke wake. Kuwa mwanaume ni hadhi kubwa pia ni ujemadari wa hali ya juu sio rahisi kama wengi tunavyofikiria. Mwanaume anatakiwa awe na busara,heshima na ukereketwa wa dhati na familia yake wakati wote. Mwanaume ambae hana heshima wala huruma na familia yake huyo hana hadhi ya kuitwa mwanaume kamili. Tafsiri ya mwanaume inatakiwa ivae uhalisia wa hakika kwa kujituma na kijiumiza ilimladi tu familia yako ipate ahuweni ya maisha. Ulevi siku zote huwa unampa mtu tafsiri mbaya kwa Mungu na hata kwa watu wanaomzunguka. Maisha ya kuitesa familia na njaa na kutokuwapa mahitaji yao muhimu kwa kuthamini pole na uzinzi huu ni ujinga ngazi ya Phd. Mwanaume timamu na mwenye seli hai za kiume kamwe hawezi kufanya unyanyasaji na ukatili kiasi hichi. Yani unadiriki kumtukana mke wako na watoto wako kwasababu ya kuendekeza ulevi na marafiki wanaokubomoa fikra zako. Watoto wanahitaji mahitaji muhimu ya shule na ya kimaisha, lakini kutokana na uzwazwa wako hela unawanunulia marafiki pombe wakati huku familia yako inaumia kwa mateso yanayotokana na mkono wako. Mke hana nguo nzuri wala mpya, na si kuwa uwezo wa kumnunulia huna hapana, ila wenye haki ya kununuliwa na wewe ni wahudumu wa bar na sehemu za kujiuza. Inasikitisha sana kuona kuna familia zina wanaume wa aina hii. Ila kumbuka mateso yako unayowapiyitishia familia yako leo, kesho yatarudi mikononi mwako. TAFAKARI KWA KINA Mwanaume ni hekima sio kujaza mwili na vyuma