Makapuku Forum

Makapuku Forum

Umewahi kuhisi unaachwa na mtu unayetarajia kumwoa au kuolewa nae? Umewahi kutamani kuwa na 'access' na simu au barua pepe ya mwenzi wako ili angalau ujisikie kutulia moyoni? Umewahi kujisikia vibaya mwenzi wako akizungumza na mtu mwingine hata kama hukuwa na ujasiri wa kumwambia? Umewahi kumchukia mtu na hata kupambana nae kwa siri au wazi sababu tu umehisi anahatarisha uhusiano wako? Kama lolote kati ya hilo linaelezea hali yako, basi makala haya yanakuhusu.
 
Najua wapo, tena wengi tu, wanaoamini ni vigumu kutenganisha hisia za wivu na mapenzi. Wanaamini huwezi kumpenda mtu bila kumwonea wivu. Kwamba kiasi kidogo cha wivu kinathibitisha upendo kwa unayempenda. Lakini ni hisia hizo hizo za wivu ndio zimekuwa chanzo cha maumivu ya moyo, majeraha, talaka na hata vifo vya watu tunaoambiwa ni 'wapenzi'. Haya hayawezi kuwa matokeo ya upendo hata kidogo.
 
Wivu umesababisha watu wasiwe na amani na mahusiano yao. Wivu umesababisha watu wawe na hasira, ghadhabu na uchungu, wakati mwingi, kwa mambo yasiyokuwepo. Wapo waliofikia kugombana na watu wasiohusika kwa sababu tu wanahisi kuingiliwa kwenye mahusiano. Wivu si hisia zinazoweza kuleta faida hata kama wengi tumekuwa tukiamini hivyo.
 
Wivu ni ugonjwa wa nafsi isiyojiamini

Kuhisi mtu unayempenda anaweza kuwa na hisia za kimapenzi na mtu mwingine sio jambo la kujivunia. Kutokumwamini mpenzi uliyenaye na kuhisi kuna mtu mwingine anahatarisha, threaten, uhusiano wenu haiwezi kuwa afya ya mahusiano. Ni ugonjwa unaohitaji tiba.
 
Ingawa wakati mwingine hisia hizi huwa sahihi, wakati mwingi huwa ni hisia tu zisizokuwepo. Ni hisia za kutokujisikia salama na kutokujiamini. Ninapokuwa na hisia za wivu, mara nyingi hili ni tatizo langu kuliko linavyoweza kuwa la huyo ninayeugua kwa ajili yake. Mahusiano yenye tishio la wivu, kuhisiana, kupekuana, na kadhalika, hutegemea na namna gani mtu aliye kwenye mahusiano asivyojiamini kwa maana ya kuwa na nafsi isiyotulia kumwezesha kujiamini na kuwaamini wengine.
 
Malezi ndio msingi wa kutokujiamini. Si kazi nyepesi kwa mwenzi aliyekuzwa bila kujiamini kujisikia salama nafsini. Hajiamini na hawaamini wengine. Na hii hujidhihirisha sana kwa watoto wa miaka kati ya mwili na sita. Kwa sababu bado wanakuwa hawajajifunza kushindana, watoto wa umri huu huwa ni wepesi kujisikia kutishwa, threatened mzazi anapomsifia au kumwonesha upendo mtoto mwingine.
 
Huwa hawajajenga uwezo wa kujiamini na hivyo hushindana na chochote kinachofikiriwa kuhatarisha umiliki wao. Wasiposaidiwa kujiamini kadri wanavyokua, watoto hawa huwa hawabadiliki. Hukua na hisia hizo hizo za ubinafsi na hofu ya mahusiano. Wanapoingia kwenye mahusiano, ndio hawa ambao hushindwa kuamini kwamba wanaweza kupendwa kama watu wengine. Na hata wanapopendwa, huhisi lolote linaweza kutokea wakati wowote. Hujenga mahusiano yaliyojaa hofu. Kwa hiyo tunaweza kusema kutokujiamini ndio hasa wivu wenyewe.
 
Watafiti wengine wanakubaliana kwamba wivu ni matokeo ya imani batili kuhusu mapenzi na mahusiano. Wivu ni imani. Umewahi kusikia watu wanasema, "Hakuna mwanaume anaweza kuwa mwaminifu! Hawa wanaume waangalie tu!" "Hawa wanawake waone hivi...hata ufanyeje hawawezi kutulia kwenye ndoa!" Haya ni matokeo ya imani zilizojikita kwenye akili ya mtu na ndizo zinazopalilia hisia za kutokujiamini, na hivyo kujenga taswira isiyokuwepo.
 
Ukweli ni kwamba unapoamini hakuna mtu anaweza kuwa mwaminifu kwenye ndoa hata ufanyeje, unajenga matarajio yanayoweza kutengeneza uhalisia usiokuwepo. Imani kuwa hakuna mtu anayeweza kuwa mwaminifu huathiri mtazamo wako na hivyo huwezi kumwamini mkeo anaposafiri kikazi kwa siku kadhaa. Unajenga hofu unaposikia mumeo anakwenda kazini kwa zamu ya usiku.
 
Na ubaya wa imani hizi zinazojengeka kwenye ufahamu humtafuna mtu ndani kwa ndani hivyo hata usiposema ulivyo na wasiwasi, lakini unajua unavyopata tabu moyoni kwa kujua lolote linawezekana kutokea. Hakuna uhusiano wowote unaweza kuleta utimilifu wa furaha inayotarajiwa katika mazingira haya ya hofu na mashaka.
 
No body can stop REGGAE Wapenzi wa muziki wa Reggae mpo ?
Reggae imewekwa katika orodha ya kumbu kumbu ya utamaduni ambao unastahili kutunzwa kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa.

Muziki huo ambao chimbuko lake ni Jamaica ulianza miaka ya 1960 kutokana na juhudi ya wasanii kama vile Toots na the Maytals, Peter Tosh na Bob Marley, umeongezwa katika orodha hiyo kutokana "urithi wa utamaduni usioonekana".View attachment 951439
Sawa
 
Wivu na mapenzi haviendi pamoja

Hisia za wivu zikishakomaa ndani kwa ndani huhamia kwenye hatua inayoweza kuonekana wazi. Hapa tunasema hisia zinahama kutoka kuwa mtazamo na imani hasi na kuwa tabia. Katika hatua hii mtu huanza kuchukua hatua za kujihami katika kukabiliana na tishio linalohisiwa. Hapa tunazungumzia mbinu za kuanza kuchunguza mwenendo wa mwenzako kwa siri. Kuanza kumfuatilia kujua mambo yake ya faragha. Kuanza kuonesha wasiwasi wako waziwazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom