Makapuku Forum

Makapuku Forum

Manchester City watahitji kuvunja rekodi yao ya kusaini wachezaji kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele baada ya klabu hiyo ya ufaransa kumwekea thamani ya pauni milion 70 mchezaji huyo wa miaka 21 mwezi Januari. (Star)
 
Manchester United wamemuambia Paul Pogba kuwa hatauzwa mwezi Januari licha ya mfaransa huyo wa maiak 25 kuripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Barcelona baada ya wao kuonyeha nia ya kumsaini. (Mail)
 
Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 31, hatarajiwi kujadili mkataba mpya na huenda akaondoka wakamti mkataba wake utakwisha mismu wa joto akitarajia kuhamia China au mashariki ya Kati. (Sun)
 
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 37, ambaye sasa anaichezea LA Galaxy yuko tayari kuzungumza na AC Milan kuhusu kurejea kwake kwa mujibu wa ajenti wake Mino Raiola. (Sun)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom