Kuwa na afya bora haitokani na kula nyama , pilau, chips , biriani , soseji, bugger, n.k, mafanikio ya afya bora inatokana na vitu vifuatavyo.
1.Angalia afya ya akili , kimwili na kiroho.
kuwa mwenye afya bora ni rahisi sana kuliko unavyofikiria wewe, haikuchukulii muda mwingi wala pesa nyingi , mfano usafi wako mwenyewe kimwili, usafi wa mazingira yako, mahusiano yako , ndoa yako ina amani, na je mahusiano yako na Mungu yakoje,
kuna watu hata kuoga wao wanaona kama adhabu , eti akiwa ameoga asubuhi , basi hata usiku haogi anaenda kulala hivyo hivyo, nguo nazo hata hafui anavaa mara mbili au tatu eti mpaka aone imechafuka. haendi kucheki hata kama anaumwa bali anameza dawa kwa kuwa tu ana maumivu ya kichwa . unaongeza sumu mwilini.