Makapuku Forum

Makapuku Forum

Laquan McDonald: Afisa wa polisi mzungu Jason Van Dyke aliyemfyatulia risasi 16 kijana mweusi mwenye umri wa miaka 17, Laquan McDonald amepatwa na hatia ya mauaji ya kinyama.

Mauaji hayo yaliyofanyika Chicago Marekani mwaka wa 2014 yalisababisha machafuko na mabadiliko katika idara ya polisi na haki. Anakabiliwa na kati ya miaka 6-15 gerezani
Screenshot_20181007-081400.jpeg
 
Klabu ya Man Utd imesema taarifa kuwa mkufunzi wa klabu hiyo, Jose Mourinho atafukuzwa ni upuuzi.

Karibuni kumekuwa na shikizo kwa mkufunzi huyo kuondoka, kutokana na matokeo mabaya, pia kile kinachodaiwa kutokuwepo kwa uhusiano mzuri na baadhi ya wachezaji.
Screenshot_20181007-081559.jpeg
 
Wanafunzi 17 wa shule za sekondari wilayani Hai, Kilimanjaro wamekiri kulawitiwa, huku baadhi ya wazazi wakisema watoto hao walifanyiwa kitendo hicho Septemba 28, siku ya mkesha wa mwenge.

Tayari watu 12 wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuwalawiti wanafunzi hao.
Screenshot_20181007-081708.jpeg
 
Rais wa Interpol Meng Hongwei aliyeripotiwa kutoweka akiwa ziarani nchini mwake (China), anashikiliwa na mamlaka za nidhamu nchini humo kwa ajili ya mahojiano.

Alichukuliwa mara tu baada ya kuwasili nchini humo akitokea Ufaransa.
Haijafahamika sababu za kiongozi huyo kuhojiwa.
Screenshot_20181007-081808.jpeg
 
Jiji la Dar es Salaam linatajwa na wanasayansi kuwa, huenda likazama katika miaka 50 ijayo kutokana na kutokuwa na miinuko na kuwa karibu sana na bahari.

Tayari Tanzania imeshapoteza visiwa viwili, kimoja wilayani Pangani, Tanga na kingine Fungu la Nyani, wilayani Rufiji.
Screenshot_20181007-081922.jpeg
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema, Morani nane waliojeruhiwa baada ya kushambuliwa na Simba wapo chini ya ulinzi kwani ushahidi wa kimazingira unaonesha walikuwa wakiwinda.

Morani hao wamedai walikuwa wakichimba maji, ghafla mnyama huyo akatokea na kuwashambulia.
Screenshot_20181007-082103.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom