Makapuku Forum

Makapuku Forum

FAHAMU MAISHA YA KUUZA MUUZA MADAWA YA KULEVYA NGULI PABLO ESCOBAR

Dawa za Kulevya ni moja ya ulevi unaopigwa vita mno karibu mataifa yote dunianiZipo aina mbalimbali za dawa za kulevya lakini dawa aina ya Cocaine ni dawa hatari mno ambayo ukiianza ni vigumu kuacha kutokana na kuathiri haraka mfumo mzima wa binadamu.

Pengine unajiuliza ni nani haswa muanzilishi wa uraibu huu? Basi fahamu kuwa Pablo Escober ndie muanzilishi wa uraibu huu.

Nathubutu kusema asingekuwepo Pablo Escober duniani basi kusingekuwepo na dawa za kulevya aina ya cocaine. mfahamu Pablo Escober na namna alivyowekeza kwenye biashara hii
 
FAHAMU MAISHA YA KUUZA MUUZA MADAWA YA KULEVYA NGULI PABLO ESCOBAR

Dawa za Kulevya ni moja ya ulevi unaopigwa vita mno karibu mataifa yote dunianiZipo aina mbalimbali za dawa za kulevya lakini dawa aina ya Cocaine ni dawa hatari mno ambayo ukiianza ni vigumu kuacha kutokana na kuathiri haraka mfumo mzima wa binadamu.

Pengine unajiuliza ni nani haswa muanzilishi wa uraibu huu? Basi fahamu kuwa Pablo Escober ndie muanzilishi wa uraibu huu.

Nathubutu kusema asingekuwepo Pablo Escober duniani basi kusingekuwepo na dawa za kulevya aina ya cocaine. mfahamu Pablo Escober na namna alivyowekeza kwenye biashara hii
Pablo alikuwa mafia sanaaaa
 
PABLO NI NANI?

Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa colombia

Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza makubwa ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe.
Screenshot_20181007-083626.jpeg
 
Kama hii haitoshi kwenye gereza hilo pia kulikuwa na chumba maalumu cha michezo ya watoto maalumu kwa ajili ya watoto wa mfungwa huyo pindi akitembelewa na familia yake.

Na pia ndani ya gereza kuliwekwa darubini kali (Telescope) ya kumuwezesha mfungwa huyo kuangalia katika mji wa Medellín ambako familia ya mfungwa huyu iliishi na kila siku jioni walitoka nje kibarazani kuongea naye kwenye simu huku akiwatazama kwa darubini.

Gereza hili lilijulikana kama La Catedral (the cathedral) na lilimuhifadhi mfungwa muhimu zaidi duniani na binadamu aliyeifinyanga na kuifanya biashara ya mihadarati iwe jinsi ilivyo hivi leo.

Marafiki zake wa karibu walipenda kumuita El Patrón (The Boss) au El Zar de la Cocaína (The Tsar of Cocaine) lakini alipozaliwa wazazi wake walimuita Pablo Emilio Escober Gaviria au kwa kifupi Pablo Escobar kama ulimwengu wote ulivyomtambua.

Akiwa mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto saba ambapo baba yake alikuwa ni mkulima na mama yeke mwalimu wa shule ya chekechea, Pablo Escobar alikuwa ni mwenye kutamani mambo mazito na mwenye maono makubwa tangu angali mtoto.

Akiwa bado kwenye umri wa makumi (teenage) Pablo mara kwa mara aliwaambia ndugu zake na marafiki zake kuwa anataka awe na utajiri wa kiasi cha Peso Milioni 1 za Colombia (COL$ 1 Million) atakapofikisha umri wa miaka 22.

Pamoja na biashara hiyo pia Pablo alijihusisha na kusambaza mizigo ya sigara zilizokuwa haziruhusiwi nchini Colombia (Marlboro), pia alifanya kazi kama mlinzi binafsi (bodyguard) pamoja na wizi wa magari.

Moja ya matukio muhimu ya ujana wa Pablo yaliyochangia kuamsha ari ndani yake na kumfanya atamani kuwa moja wa manguli wa biashara haramu lilikuwa ni tukio ambalo alipofikisha miaka 26 alifanikiwa kuweka benki (Cash Deposit) kiasi cha Peso Millioni 100 za Colombia (COL$ 100 Million).

Mafanikio haya yaliwasha taa ndani yake na kuamsha ari ya kutaka kuwa ‘Papa’ katika ‘Dunia’ ya siri ya ulimwengu wa biashara haramu.

Katika miaka ya 1970 mamlaka ya kupambana na matumizi mabaya ya madawa nchini marekani (US Drug Enforcement Agency) waliwahi kutangaza kuwa wamewekeza zaidi rasilimali zao kupambana na matumizi na uingizaji wa dawa aina ya Heroin nchini marekani na kwa maoni yao walisema kuwa wanadhani madawa aina ya Cocaine hayakuwa na uwezo wa kuleta uteja (addiction) au kufanya mtumiaji kuwa muhalifu tofauti na dawa aina ya Heroin.

Hivyo basi walielekeza nguvu zao zote na rasilimali kupambana na biashara ya usafirishaji wa Heroin kama kipaumbele cha kazi zao.

Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa upande wao. Kwani kijana Pablo aliona mwanya huu na udhaifu huu upande wa DEA au pengine tusema kwamba Pablo alifahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa mihadarati kuliko DEA.

Kitu kikubwa ambacho Pablo alikiona na watu wakiwemo DEA hawakukiona ilikuwa ni uwezekano (potential) ya kuifanya Cocaine kuwa moja ya madawa yenye soko zaidi Amerika ya Kaskazini.

Katika kipindi hiki kulikuwa na watumiaji wachache sana wa Cocaine nchini marekani lakini Pablo aliona fursa ya kuifanya mihadarati hiyo kuwa moja ya madawa yenye kuhitajika sana nchini marekani na ulimwenguni kiujumla.

Kutokana na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu, Pablo aligundua kuwa zao la Coca linalimwa nchini Bolivia ambalo linatumika kutengeneza Cocaine ni bora zaidi kuliko Coca inayolimwa nchini kwake Colombia.

Hivyo basi Pablo akadhamiria kuwa kama anaingia kwenye biashara hii ya kusafirisha Cocaine ni lazima mihadarati yake iwe tofauti na bora zaidi kuliko Cocaine nyingine watu waliyozoea kutumia.

Akadhamiria kufanya Cocaine yake iwe daraja la kwanza ili kuvutia watumiaji na kufanya soko likue kwa haraka.
Kama sehemu ya mkakati wake wa kuingia rasmi kwenye biashara ya kusafirisha mihadarati aina ya Cocaine, mwaka 1975 kijana Pablo alisafiri mpaka nchini Bolivia kukutana na Roberto Suaréz Goméz ambaye marafiki zake walipenda kumuita El Padrino (The Godfather) kiongozi wa Genge lililoitwa La Corparacíon (The Corporation).

Suaréz alikuwa ndiye mtu pekee anayeendesha na kuratibu uzalishaji wa zao la Coca katika nchi ya Bolivia na Peru. Kipindi hiki Suaréz tayari alikuwa na mtandao mkubwa katika America ya kusini na alikuwa na jina kubwa, ushawishi na nguvu ya kijeshi hivyo haikuwa kazi rahisi kwa kijana Pablo kumshawishi

Suaréz akubali kufanya naye biashara.
Itaendelea.......!!

Dawa za Kulevya ni moja ya ulevi unaopigwa vita mno karibu mataifa yote duniani.

Zipo aina mbalimbali za dawa za kulevya lakini dawa aina ya Cocaine ni dawa hatari mno ambayo ukiianza ni vigumu kuacha kutokana na kuathiri haraka mfumo mzima wa binadamu.
 
Fahamu Maisha Ya Muuza Madawa Ya Kulevya Nguli, Pablo Escobar......Part 2

Huyu bwana Suaréz alikuwa na nguvu kiasi kwamba alikuwa na jeshi lake binafsi la anga (Air force) na wanajeshi wa miguu 1,500 ambao walipatiwa mafunzo nchini libya.

Pablo alitumia uwezo wake wa kujieleza na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu kumshawishi Suaréz na kumueleza kuhusu mkakati wake wa kuiteka biashara ya mihadarati ya Cocaine nchini marekani na akamdadavulia jinsi ambavyo yeye Suaréz atapata utajiri wa kupindukia kama atakubali kufanya nae biashara.

Pia Pablo alimpa wazo Suaréz kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini (Suaréz alikuwa amefanikiwa kumpenyeza Mdogo wake serikalini na kuwa Waziri wa mambo ya ndani) ahakikishe wanakutana na kiongozi wa Cuba Fidel Castro ili wamuombe kuwa mshirika wao katika mambo kadhaa.

Suala hili lilifanikiwa kwani Pablo na Suaréz walipata fursa adhimu na wakakutana na Fidel Castro na ombi lao kubwa kwake lilikuwa ni kuwaruhusu kupitisha mizigo yao nchini kwake Cuba na nchi za jirani pasipo bugudha.

Pia walimuomba aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanma vya ndege vya Cuba na kujaza mafuta pale inapobidi kufanya hivyo.
Screenshot_20181007-084721.jpeg
 
Castro akawakubalia kwa masharti mawili, moja ni kwamba atakuwa anawachaji mamilioni ya dola za marekani kwa huduma hizo na pili mihadarati hiyo isiuzwe ndani ya Amerika ya Kusini bali isafirishwe na kuuzwa Marekani ambapo Fidel Castro alisisitiza kuwa atafurahi akiona vijana wa Mabepari wakiharibika na mihadarati.

Masharti yote mawili haya yakakubaliwa na Pablo na Suaréz kisha wakarejea Bolivia . Baada ya kufanya mazungumzo juu ya namna watakavyo fanya biashara hatimae Pablo na Suaréz walifikia muafaka na kwa mzigo wake wa kwanza alioununua nchini Bolivia kutoka kwa Suaréz ulikuwa ni kilo 14 za unga gafi za Cocaine.

Baada ya unga gafi kufikishwa nchini Colombia kwenye mji wa Medellín, Pablo alikuwa ameandaa jengo maalum la ghorofa mbili ambalo alilitengeneza kuwa maabara maalumu ambapo Cocaine gafi kutoka Bolivia ilichanganywa na maligafi nyingine na kuboreshwa zaidi kikemia na hatimaye kupata Cocaine daraja la kwanza aliyoihitaji tayari kusafirishwa nchini Marekani kwa ‘walaji’.

Baada ya Cocaine kutoka kwa Pablo kuingia kwenye soko la Marekani uhitaji na biashara ya mihadarati ya Cocaine ilipaa kwa kasi ya ajabu na Pablo Escobar akaanzisha rasmi genge lake la biashara ya mihadarati na kuliita Medelline Cartel
 
Fahamu Maisha Ya Muuza Madawa Ya Kulevya Nguli, Pablo Escobar......Part 2

Huyu bwana Suaréz alikuwa na nguvu kiasi kwamba alikuwa na jeshi lake binafsi la anga (Air force) na wanajeshi wa miguu 1,500 ambao walipatiwa mafunzo nchini libya.

Pablo alitumia uwezo wake wa kujieleza na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu kumshawishi Suaréz na kumueleza kuhusu mkakati wake wa kuiteka biashara ya mihadarati ya Cocaine nchini marekani na akamdadavulia jinsi ambavyo yeye Suaréz atapata utajiri wa kupindukia kama atakubali kufanya nae biashara.

Pia Pablo alimpa wazo Suaréz kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini (Suaréz alikuwa amefanikiwa kumpenyeza Mdogo wake serikalini na kuwa Waziri wa mambo ya ndani) ahakikishe wanakutana na kiongozi wa Cuba Fidel Castro ili wamuombe kuwa mshirika wao katika mambo kadhaa.

Suala hili lilifanikiwa kwani Pablo na Suaréz walipata fursa adhimu na wakakutana na Fidel Castro na ombi lao kubwa kwake lilikuwa ni kuwaruhusu kupitisha mizigo yao nchini kwake Cuba na nchi za jirani pasipo bugudha.

Pia walimuomba aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanma vya ndege vya Cuba na kujaza mafuta pale inapobidi kufanya hivyo. View attachment 889187
Huyu jamaa yuko responsible kwa vifo vya watu dunia nzima kwa overdosage....maana yeye ndo muhasisi wa Poda...daah.
 
Pablo akatengeneza mtandao madhubuti wa wasambazaji wa mihadarati yake katika miji ya Florida na California pamoja na majimbo mengine ya Marekani.

Pia akabuni njia mpya ya kupitisha mihadarati kupitia Bahamasi katika kisiwa cha Norman’s Cay takribani kilomita 350 kusini mashariki mwa pwani ya Florida.

Ili kufanikisha zaidi azma yake Pablo Escobar alinunua nusu ya ardhi ya kisiwa cha Norman’s Cay na nusu nyingine ikanunuliwa na swahiba wake wa kimarekani aliyeitwa Robert Vesco ambaye pia alikuwa ndiye anashughulikia masuala yake ya kibenki na uhasibu.

Katika Kisiwa hiki Pablo alitengeneza uwanja wa ndege, bandari, hoteli, nyumba za kuishi pamoja na ghala kubwa la jokofu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mizigo ya Cocaine kabla ya kuisafirisha kwenda marekani. Kwa kifupi hapa ndipo kilikuwa kitovu cha kibiashara cha Genge lake la Medellíne Cartel.

Pablo Escobar alikuwa amepania haswa kuliteka soko la Cocaine Amerika ya Kaskazini na hii ilijidhihirisha kutokana na juhudi zake alizozifanya kibiashara ili mda wote awe hatua kadhaa mbele tofauti na washindani wenzake kibiashara.
 
Ili kufanikisha usafirishaji wa mizigo yake kwa ufasaha na uhakika Pablo alinunua ndege za mizigo 15 za ukubwa wa kati na helikopta 6.

Pia alinunua Nyambizi ndogo mbili (submarines) kwa ajili ya kusafirisha mizigo mikubwa ya mihadarati.

Hadi kufikia mwaka 1985 Pablo alikuwa anasafirisha takribani tani 70 mpaka 80 za Cocaine kwa mwezi na alikuwa ameshikilia asilimia 80 (80%) ya soko la mihadarati la Marekani.

Na katika kipindi hiki Genge lake la Medellíne Cartel lilikuwa linaingiza kipato cha cha Dola Milioni 70 kwa siku (Shilingi Bilioni 140 za Kitanzania) na mapato yao kwa mwaka mzima yalifikia Dola Bilioni 21.9. (Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania).

Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.
 
Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).

Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw.

Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.

ITAENDELEAA.........
 
Huyu jamaa yuko responsible kwa vifo vya watu dunia nzima kwa overdosage....maana yeye ndo muhasisi wa Poda...daah.
Haya mambo uyasikie tu kama hauna ndugu anayetumia

Nina mjomba yangu ni teja acha tu tumpeleke sobar hataki tumpeleke akanywe hata dawa zao za methadone hataki anasema tusimlazimishe

Tumuache eti akiamua mwenyewe atafanya lini sasa gari linazidi kuwaka tu haya mambo narudia uyasikie tu kama hauna ndugu yako wa karibu anayetumia
 
Haya mambo uyasikie tu kama hauna ndugu anayetumia

Nina mjomba yangu ni teja acha tu tumpeleke sobar hataki tumpeleke akanywe hata dada zao za methadone hataki anasema tusimlazimishe

Tumuache eti akiamua mwenyewe atafanya lini sasa gari linazidi kuwaka tu haya mambo narudia uyasikie tu kama hauna ndugu yako wa karibu anayetumia
Shunie, nna ndugu yangu alitumia ila yeye alifanya Heroine, yani tangu akiwa Shuleni Uganda....yeye alimix bangi na Heroine....alikuja kuwa chizii balaa, vikao vikakaa wakampeleka Tanga kuna institution flan hv ipo Lushoto huko Lutindi miliman huko yani bila hivyo tungempoteza maana hatua aliyofikia ni ile akikosa arosto yake sasa hadi anatetemeka mwili mzima, aliacha kutumia ila mpaka leo ana hali flan hv ya kuzubaa bado hajatengemaa vizuri.
 
Mm mjomba angu huwa akiwa anavuta najifungia chumbani kwake na sio peke yake yupo na washkaji zake kuna siku walibaki washkaji zake nikawachungulia

Wanachukua unga wanaweka juu ya zile karatasi sijui za sigara zile kwa chini zina usilver chini ya ule usilver wanawasha moto halafu sasa ndio wanavuta puani

Hiyo ya kutetemeka ni alosto akikosa unga mbona sisi mjomba wetu akifikia hivyo tunajua anataka kufa tunamchulua tumpeleke hospital yaani tunachanganyikiwa sana siku ya kwanza tunataka tumpeleke hospital akakataa akasema mm siumwi ugonjwa wa hospital uko mnanipeleka mnaenda kunia

Tukamtazama unaumwa nn sasa mbona unasikia baridi ndio kutuambia arosto ya unga akasema tumpe elf 2 sijui elf 5 amtume rafiki yake amletee unga atakaa sawa mbona tulitoa hela na kweli alivyovuta akarudi kwenye hali yake

Yaan ikimtokea hiyo arosto kama hana hela hatuna jinsi tunamnunulia
Shunie, nna ndugu yangu alitumia ila yeye alifanya Heroine, yani tangu akiwa Shuleni Uganda....yeye alimix bangi na Heroine....alikuja kuwa chizii balaa, vikao vikakaa wakampeleka Tanga kuna institution flan hv ipo Lushoto huko Lutindi miliman huko yani bila hivyo tungempoteza maana hatua aliyofikia ni ile akikosa arosto yake sasa hadi anatetemeka mwili mzima, aliacha kutumia ila mpaka leo ana hali flan hv ya kuzubaa bado hajatengemaa vizuri.
 
Kapata wakili mzuri tu, huku Tz angeangalia Miaka isiyopungua 30 au kifo tu ashukuru hata hiyo miaka 15.
Ishu hapo siyo wakili bali aina ya sheria /hukumu
Kwa Bongo kosa la mauaji ni kifungo cha maisha(life imprisonment) na kuua bila kukusudia adhabu inaweza kuwa miaka miwili na kuendelea
Nchi zinatofautiana sheria hivyo Tz ukipatikana na hatia ya mauaji(murdsr) hata utetewe na Kibatala adhabu ni hiyohiyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom