BlessedHope
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 7,988
- 32,649
EZEKIELI 37;3Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa
mikavu, lisikieni neno la BWANA.
*_Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi._*
Roho wa Bwana akamchukua Ezekieli katika bonde lenye mifupa mikavu ,akauulizwa je mifupa mikavu inaweza kuishi?
Ezekieli alipoitazama ile mifupa akaona hakuna uhai,haiwezi kuishi tena maana akiitazama mifupa imekuwa mikavu wala haina nyama,akaona ni jambo gumu sana mifupa kupata uhai tena,hivyo alipoulizwa juu ya lile tatizo kuwa linaweza tatulika akamjibu Mungu mimi sijui wewe ndo unajua...
*Katika mapito magumu huwa tunalitazama tatizo bila kutazama ukuu wa Mungu.Mungu ndo anajua yote wacha kulitazama tatizo kuwa ni kubwa kuliko MUNGU wako,ktk mambo magumu yale usiyoyaweza yaliyofika ktk upeo wa akili zako ndipo Mungu anakuonyesha ukuu wake..Ezekieli aliona lile tatizo la mifupa kupata uhai ni jambo gumu sana ila akiwa ktk bonde la mifupa mikavu alipewa NENO la Mungu juu ya mifupa na pia hakuwa peke yake kulikuwa na ROHO ya Bwana iliyomchukua na kumpeleka katika hilo bonde.*
Unapokuwa ktk bonde lenye mifupa mikavu hakikisha ROHO mtakatifu yupo pamoja na wewe pia hakikisha umepewa NENO la Mungu juu ya hiyo mifupa,USIENDE KTK BONDE LA MIFUPA MIKAVU UNGALI HUNA NENO LA KUITABIRIA HIYO MIFUPA.
*_Kwani kama hauna NENO na ROHO mtakatifu hapo hakuna UHAI.Neno na Roho mtakatifu vinakamilisha uumbaji na kuleta uhai..Neno likitamkwa Roho anaingia kazini analipulizia pumzi ya uhai nalo neno linafanyika mwili._*
Ezekieli aliambiwa atamke NENO ,aseme na mifupa mikavu
.'''Enyi mifupa mikavu lisikieni neno la Bwana.''...Na ile mifupa ilisikia sauti ya Bwana ikajikusanya mfupa kwa mfupa ikaingiwa na mishipa na ngozi,akatabiria upepo uwapulizie hao waliouawa wapate kuishi,pumzi ikawaingia wakasimama kwa miguu yao wakawa jeshi kubwa mno.
Je mifupa mikavu yako ni nini?
Inawezekana mifupa mikavu ni ndoto zako za kusoma,kuoa/kuolewa zimekufa,matumaini yako yamekufa,basi leo sema na hiyo mifupa mikavu isikie neno la Bwana ipate uhai,tamka neno juu ya hiyo mifupa ili iweze kupata uhai maana mauti na uzima vipo ktk nguvu ya ulimi..
Unapotamka neno la baraka katika ndoa iliyokufa au biashara iliyokufa huwa unajitabiria mema navyo vinakuwa hai tena..Roho mtakatifu yupo katika maneno yako mazuri ya baraka,akija analeta uhai katika hivyo ulivyovinenea..
Unapokuwa katika bonde lenye mifupa mikavu unapoitazama hiyo mifupa unaingiwa na hofu na kukata tamaa kuona haiwezekani kupata uhai tena ?
Au unakuwa na neno la Mungu ili kutoa unabii juu ya hiyo mifupa iweze kuishi?
*UBARIKIWE NA BWANA*

