*_RUHUSU FAGIO LA ROHO MTAKATIFU LIFAGIE NA KUONDOA CHOCHOTE KISICHOFAA KWENYE MAISHA YAKO_*
Mungu akitaka akuinue na kukupeleka kwenye kiwango kingine cha Upenyo kwenye maisha yako, ni lazima kwanza aanze kufanya mabadiliko kwenye maisha yako.
Kwanza kabisa atahakikisha anashughulika na moyo wako ili anapokuinua KIBURI kisiinuke ndani yako na kukufanya umkufuru Mungu kama Nebukadreza.
*_Pili,atahakikisha anaondoa vizuizi vyote na visiki vyote vya mafanikio yako ili ukipata Upenyo, Upenyo wako usiambatane na huzuni.
Tatu, ataondoa watu wasiofaa kwenye maisha yako ili akikuinua wasije wakainuka na kusema," Ni sisi ndio tumemfikisha hapo alipo.Sisi ndio tumehusika kufanya maisha yake , huduma yake n.k ifike hapo.Bila sisi asingeweza."
Kumbuka Mungu anapomwinua mtu anataka UTUKUFU UMRUDIE YEYE.Maana Yeye ni Mungu mwenye Wivu (Isaya 42:8)
*_Unapoona Umemwomba Mungu kwa muda mrefu kwa habari ya Upenyo au umemwomba Mungu akutoe kwenye hatua uliyopo na kukupeleka kwenye kiwango kingine cha Upenyo;_* *_USISHANGAE kuona mambo yakibadilika kwenye maisha yako na kukwendea tofauti na matarajio yako kwa muda.Usianze kumhoji Mungu na kumwuliza KWA NINI nimeomba hiki na umejibu ndivyo sivyo?
Usishangae kuona vitu vinaibuka na vingine havina kichwa wala miguu.Usishangae kuona baadhi ya watu wanainuka na kukushambulia na hata hujawakosea au kuwatendea ubaya wowote.Hapo Mungu anakuwa anaweka ukuta wa moto mwenyewe.
Usishangae kuona shetani na mawakala aliokuwa amepenyeza kwenye maisha yako kwa siri wakianza kudhihirisha makucha yao waziwazi mbele ya macho yako na kuanza kukushambulia.
*_Badala ya kumhoji Mungu maswali na kuanza kupaniki;_* *_Mwambie Mungu_**_"BABA FAGIA CHOCHOTE KISICHOFAA_* *_KWENYE MAISHA YANGU_* na HATIMA yangu."
Kumbuka Mungu anajua maisha yako ya mbeleni.Anajua hata mioyo ya watu waliokuzunguka.Anajua kama hatafanya msako na kuwafagia wasiofaa kwenye maisha yako na hatima yako mbeleni watakuletea shida na utashindwa kufika kwenye nchi yako ya ahadi. Mpe muda asafishe njia yako ili baraka zako zinapoanza kumiminika....zimiminike bila kuzuiliwa.

Usimpangie Mungu utaratibu wa jinsi anavyopaswa kukuinua maana Mungu akiamua kumuinua mtu anaweza kuvunja hata protocal za kidunia kwani Yeye ni Mungu.

Mungu ndiye mwenye SIRI zote na kama Yeye ndiye aliyekuinua mwanzo atafanya juu chini kulinda Heshima Yake kwa kutengeneza mazingira ya Kukuinua tena bila msaada wa mtu. (Danieli 2:22)