Makapuku Forum

Makapuku Forum

MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 18

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Simulizi hii inakujia kwa udhamini mkubwa wa #km_music

#KM _MUSIC INAWAKARIBISHA WASANII WOTE KUFANYA KAZI NAO NA WANAFANYA AINA ZOTE ZA MUZIKI.PIA KAMA UKO MKOANI NA UNAHITAJI BEAT KALI WASILIANA NAO KWA SIMU NA +255743761268

#kmmusic____
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"yaani kitoto kimo hiki, sema urefu umemseidia"
"lakini ulisema mwenyewe"
"ndio ila huyo kazini afu istoshe sijampenda yaani namchukia"
"wewe mwai, wenzio wanazitafuta ndoa kama hizo hawazipati"
"I know but huyo mume wangu bwege tu"
Mwai alikuwa akimsema kijana sheby huku wakicheka sana
"kwahio ni jinga jinga tu"
"yaani halina hata akili, lipo lipo lipoleee halipendi kutoka out, yaani ni yeye na kazi tu muda wote"
"heheheeeeeeeee halooooooo bibie unalo ilooo"
Rose alicheka huku wakigongesheana mikono kwa umbea, wakati huo mary yupo bize na laptop yake, alikuwa anachati
"sasa hivi shost una laptop ni kuchat mwanzo mwisho"
"we acha tu... Hapa kuchati tuu"
"weweeeeee.... Halooooo"
"mary, umesikia mwai anavyosema kuhusu mumewe"
"nimesikia... "
"mmmhhhh lakini mwai, uyo mi mumeo tu usimfanyie hivyo"
Aliongea rose huku akicheka kwa unafiki wa hali ya juu tena wakati huo mikono inagongana haswa kwa umbea
"tena hilo ni dogo, sasa nakwambia kuna kitendo namfanyia mpaka leo hana hata raha yani"
Aliongea mwai huku rose akitega skio kujua hicho kitendo...
"Enheeee umemfanyia nini tena"
Aliuliza rose huku akitamani sana kujua, na mwai bila hiana akaanza kuropoka siri za ndoa yake..
"huezi amini rose,.. Yule mtoto wa kiume....

Ndoa ina mambo mengi sana ya kuficha tena kwa asilimia 90 hutakiwi kuongelea mambo ya ndoa,.. Mwanamke ulie tayari kuolewa kitu cha kwanza ambacho hata kwenye vitabu vya dini vimeandika usiri wa ndoa, tunza ndoa yako kwa kila njia unayoijua lakini usitoke nje ya ndoa usimsemee mume au mke vibaya,.. Uimara wa ndoa huja pale mnapofichiana siri zenu mpaka kifo kiwatenganishe,...

"Enheeee umemfanyia nini tena"
Aliuliza rose huku akitamani sana kujua, na mwai bila hiana akaanza kuropoka siri za ndoa yake..
"huezi amini rose,.. Yule mtoto wa kiume toka anioe sijawahi kumpa tendo la ndoa hata siku moja mpaka leo hii tuna zaidi ya miezi miwili naa.. Lakini hajui uchi wangu upoje"
Aliongea mwai huku akijisifu sana kwa kitendo hicho cha kutompa mumewe tendo la ndoa,..
"we mwai umezidi uongo sasa mmmhhh"
"mi nakuambia sasa,.. Yaani mimi wa kunila ni jemsi peke yake na sio haka kasambaa ka kijinga"
"he he he he he HaaaaLoooooooo laaake ilooo"
Mwai na rose walikuwa wakicheka sana na hata mary alikuwa akisapoti kiasi ila yeye sio kivile na mambo ya umbea,... Mary hua anapenda kujiepusha na umbea umbea wa hapa na pale,
"nakwambia shost kweli umepata mume bwege"
"tena sio bwege wa kawaida, ni bwege haswa"
Aliongea mwai huku akitoa pochi na kuangusha vinywaji maalum kwa wanawake,.. Walianza kunywa huku stori kwa wingi zikiendelea...

Tukija huku kwa kijana sheby akiwa ndio anatoka na wakati huo kagiza kameshaingia tayari yeye ndio anatoka ofisini kuelekea nyumbani kwake
"boss leo kazi zimekubana sana ee"
Aliuliza mlinzi wao huku akiambatanisha na kicheko
"aahhh si unajua kazi zetu hizi, yaani ni ngumu sana kiukweli"
"pole sana boss"
"Ahsante sana"
Basi kijana huyo alitoka na kuelekea nyumbani kwake, lakini hua hapiti mbali na hoteli fulani na kula kabisa, inashangaza mwanaume ana mke lakini anakula hotelini, ni kitendo cha ajabu sana,
"Samahani nitengenezee chipsi moja safi sana takeaway"
Aliongea sheby kwa kumtaka muhudumu afanye hivyo,...
"sawa boss"
Muda ulisogea na sasa ni saa mbili usiku sheby akiwa nje ya geti la Nyumba yake, kama unakumbuka walizawadiwa nyumba ya kifahari na wazazi wake,..
"aahhhh boss karibu sana boss"
Alikuwa ni mlinzi wa jengo hilo akimkaribisha boss wake aingie ndani, lakini sheby alishtuka kufika kwenye paking haoni gari ya mke wake...
"john... John"
Alimuita mlinzi na kumuuliza
"yes boss"
"gari ya shemeji yako ipo wapi"
"ametoka nayo mwenyewe boss"
Kijana huyo alijiskia vibaya sana kwa kuskia mke wake katoka afu mbaya zaidi sasa ni saa mbili hii usiku, afu mke wa mtu bado hajarudi nyumbani,.Ilimuuma roho japo matukio hayo hutokea kila siku, ...
"ametoka saa ngapi"
Aliuliza kijana huyo huki akitoa zawadi nyingi tu alizoleta
"kama saa 12 hivi kasoro"
"duuuuuuu toka saa hio"
Ghafla honi ya gari imelia kwa nje, sheby akajua ndio yeye mana honi anaijua, sasa sheby hakutaka kuendelea kukaa hapo aliondoka zake na kuingia ndani,...
Mlinzi alifungua geti kisha mama mwenye nyumba kaingia, wakati huo kijana sheby yupo ndani kajituliza kwenye sofa huku akijifanya kaja muda mrefu, kumbe kaja muda huo huo...
"weeee amerudi saa ngapi"
Mwai alimuuliza mlinzi kuwa sheby kaja saa ngapi,..
"muda sio mrefu, kama dakika tano hivi"
"ok poa"
Mwai aliingia ndani na kumkuta mume wake kaweka mguu juu, sheby alikuwa akijifariji tu na masofa kwa kuweka mguu juuuu.... Lakini mwai alipoingia aliutoa ule mguu na kukaa yeye,
"mume wa mtu, unarudi saa hizi nyumbani, ulikuwa wapi"
Aliongea mwai huku akiwa kavinyoosha vidole vyake kama vile anasuta mtu,...
"sasa mke wangu, mi na wewe nani wa kumuuliza mwenzie? mimi nilikuwa kazini, haya na wewe je"
"hio haikuusu, zawadi zangu zipo wapi"
"hizo hapo"
Haya ndio maisha wanayoishi wanandoa hao, yaani sheby anaumia moyo wake sana, yaani hatamani hata kuitwa mume, na hata hio hadhi ya mume hapewi kama mume,...
"kila siku chipsi mayai kila siku chipsi mayai, kwani mi mwanafunzi"
Maskini kijana sheby alikuwa kimya, yaani kama kuna wanaomchukia kijana huyo basi kwa hapo alipo watakuwa wanafurahia sana,..
"lakini mke wangu"
"Eh eeeeeeee, hilo neno mke wangu nilishakwambia lisiwe wimbo mdomoni mwako sawa eee"
"sawa, lakini wewe ulisema lete zawadi yeyote"
"kwahio yeyote ndio umeona chipsi"
Sheby hakutaka malumbano, alikumhuka siku anaonywa na baba yake kuwa
#"haruhusiwi kumpiga, wala hutakiwi kumchukiza"#
#"mzee, nitakaaje na mke asioadhibiwa"#
#"nimeshasema... Naomba utii amri"#
Sheby alipomaliza kukumbuka maneno ya baba yake, aliamka katika sofa na kuingia zake chumbani,.. Aliingia bafuni na kuoga kisha akatoka na kujilaza zake kitandani..
Nyumba hio haijawahi kupikwa hata siku moja, mwanamke kila siku anakula vitu vya kununua tu, na ndio mana hqta sheby kala kule kule hotelini mana anajua torati ya mke wake hua hapikagi na ndio mana sheby akirudi anakuja na chipsi kuku au chipsi mayai,...

BAADA YA SIKU HIO KUPITA

Leo kijana sheby kapata muda kidogo wa kutembelea kule uswahilini kwa mchumba wake, sheby akiwa na mkokoteni wake uliojaa viazi vya chipsi,..
"haya kula kiazi cha leo leo ichooo"
Alikuwa ni kijana sheby akiwa anauza viazi, lakini sisi tunajua sio kazi yake
"unamsikia bwege wako uyo, kila siku anakuletea viazi uchemshe, we una upungufu wa madini ya wanga mwilini wewe?... Kazi kula hela zangu tu nakuambia kila siku husikiii"
Aliongea shadi huku akiamka... Wakati huo zai kanyamaza kimya hana neno na mtu yeye anampenda sheby wake hata kama ni muuza viazi
"karibu kaka sheby"
Shadi alimkaribisha huku upole wake ukiwa umerudi, maskini ya mungu kijana sheby ana balaa tupu, yaani ana balaa sio kidogo.. Shadi alikuwa mpole kama ilivyo kawaida ya upole wake, lakini sheby akiondoka tu, shadi anavaa nguo fupi na kutoka muda wowote ule..
"Ahsante sana dada shadi"
"waaaooo baby mambo"
Alikuja zai kwa furaha na kumsalimia mpenzi wake,...
"poa nambie"
"safi tu, nimekumiss mie"
"muongo zai"
Basi sheby akaacha mkokoteni wa viazi hapo nje na kuingia ndani,...
"siku hizi unazidi kunenepa tu vipi mwenzangu"
"mmmhhh shida zangu tu wala hakuna jipya"
Sheby alijikuta anamtamani zai, ukumbuke toka aoe, hajawahi kupewa haki ya ndoa na mke wake, sasa leo kamkuta zai kavaa kanga alioifunga kifuani, sheby alimsogelea kimatamanio huku akitaka kumnyonya denda, maskini yaani hata huyu zai pia ana kiapo nae na kuvunja kiapo ni kitu kibaya sana, tena mbaya zaidi ni kwamba aliapa mbele ya mama mkwe wake kuwa hatokaa kumgusa mpaka pale atakapokuwa mke wake, lakini mpaka sasa sheby kesha oa, ana mke sasa sijui kama kiapo bado kipo au kimevunjika,...
Wakati huo shadi kaingia chumbani kwake katulia kimyaa kitandani kwake, kama unavyoujua upole wa shadya ni adimu kwa kila mwanamke lakini huezi amini hapo alipo kavaa ngozi ya kondoo wakati ni chui...
Hata zai alikuwa na hamu ya mapenzi toka kwa mchumba wake huyo, ila hajui kama mwenzie keshaoa kwa lazima bila kupenda, mambo ya wazazi hao....
Wawili hao waliweza kukutanisha midomo yao na kuanza kunyonyana denda, hapo sheby kaacha mkokoteni wa viazi hapo nje, mikono ya zai ilianza kumpapasa sheby huku sheby nae akiyajibu mapigo toka kwa zai,.. Kutokana na zai kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi, hivyo kila alipoguswa kwake ilikuwa ni kelele tu,...
"aaaiiiii"
Vilio vilivyokuwa vya kichokozi kwa kijana huyo,
"uuuuuuwiiiiiiiiiii shebiiiiiiiii usiachie please"
Aliongea zai huku macho yake yakiwa yamejifumba, chuchu zake zilikuwa kero kwa kijana sheby, kwani kila akizigusa sheby lazima afumbe macho yake huku akijibu mapigo ya sauti
"assisisiiiiiiii"
"sheby nini sasa, mimi nilie hata wewe pia"
"kwani mi sina hisia... Ukiona silii basi ujue umbo lako halinifai"
Zai kuskia hivyo alitamani kuvua hata chupi kabisa mana ni maneno yaliompa furaha katika moyo wake,.. Zai aliitupa ile kanga na kubaki na chupi huku akimrukia sheby na kumnyonya katika shingo...

Sasa huku kwa shadi kumbe hata shadi alikuwa akizisikia hizo sauti za akina sheby na zai...
Huezi amini nae alikua akijitomasa katika kifua chake... Sasa swali linakuja hivi, Kama shadi ni malaya, sasa mbona anazishangaa sana na kuzifurahia sauti hizo, kana kwamba hajawahi hata kuzisikia wala kukutana nazo, na wakati yeye ni malaya.... Mi sijui twendeni mbele

Tukirudi huku katika chumba cha akina sheby na zai,.. Sheby alisitisha denda kwanza na kuanza kuongea mambo ya ndoa yao, mana zai ndio kaanza
"we sheby umeamua kuvunja kiapo, lakini sawa tu kwani kuna nini"
Hapo ndipo sheby akasitisha kumnyonya mate mpenzi wake
"aaahhhh nisamehe zai"
"No, mi nipo tayari kama utataka"
"zai... Kuna kitu nataka kukuambia ila sjui kama utakasirika"
"we bwana kama wataka mapenzi ina haja gani uniambie, we nisukumie kitandani nipe vyangu, mi ni mkeo mtarajiwa huna haja ya kusema nataka.. We nivute ule vyako jamani sheby"
"sio hilo"
"nini kwani.... Au umeanza tabia mbaya, mana nyie wanaume wa siku hizi manpenda sana tabia mbaya..."
"tabia gani tena sisi tunaipenda"
"si kurukana hovyo hovyo... Mi naomba hilo lisikupate mme wangu"
"zai.... Mi mwenzio nimeoa"
Zai ana macho makubwa yaliompendeza kutokana na umbo lake, lakini kwa maneno hayo alioyaongea sheby, macho ya zai yamekuwa makubwa zaidi... Mpaka sheby aliogopa huenda yakapasuka..
Lakini sasa kumbe......

Je? Nini Kitaendelea??....
Tuendelee jaman husna
 
Ni mwendo wa Movie tu leo

bde5cdd3b6d4d5c845bfccdc1fb3469f.jpg



Ipi Kali hapo
 
With all this extra stressin'
The question I wonder is after death, after my last breath
When will I finally get to rest through this oppression?
They punish the people that's askin' questions
And those that possess steal from the ones without possessions
The message I stress: to make it stop, study your lessons
Don't settle for less, even the genius asks his questions
Be grateful for blessings
Don't ever change, keep your essence
The power is in the people and politics we address
Always do your best, don't let the pressure make you panic
And when you get stranded
And things don't go the way you planned it
Dreamin' of riches, in a position of makin' a difference
Politicians are hypocrites, they don't wanna listen
If I'm insane, it's the fame made a brother change
It wasn't nothin' like the game; it's just me against the world
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom