Makapuku Forum

Makapuku Forum

THE DOM

Sehemu Ya 17

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

Yaani kakauka mbaya mbovu, kisha akaandika X kwa hewani.. Mageneral wanaangaliana huku wakijiuliza kwanini sahi acheke,... Sasa baada ya sahi kicheka mara generally Nyange nae kacheka,... Sahi akizidi kushangaa kicheko cha General nyange, akashngaa kwa chini kuna wanajeshi walioshika mitutu, yaani generally kesha panga hata kumuondoa rais.... Na wakati huo ndege ndio inaruka juu kwa safari,..
"aisee, pita kulia mara moja"
Aliongea sahi baada ya kuona chini kuna hatari, Mheshimiwa kaona kila kitu, na akajua kiwa hata hapa jeshiwkuna jipu,... General nyange alishangaa kuonda ndege imepita kulia hivyo ipo mbali na mitego yake,.. Hivyo akawa ameshindwa kufanya jambo lake,...
Sasa huku ndani ya ndege, mzee GU kamgeukia sahi na kumwambia
"hata wewe ni jipu,... Utakaa miezi sita jela"
Sahi alitoa macho huku akiuliza
"ujipu wangu ni nini mkuu"
"utajua tu... Umeficha siri ukajua sintoijua??.... Rubani, tuelekee maweni prison jail"
Sahi haamini kama kweli anapelekwa jela, mbaya zaidi dom hajui ilipo... Maana yake imeshapotea....

ENDELEA........

Sahi akiwa juu ya ndege na Mheshimiwa GU, na wakati huo anashangaa kwa maneno ya Mheshimiwa kuwa nae ni jipu, hivyo ndege ielekee maweni prison jail, sahi analijua gereza hilo lilivyo machachari kwa wafungwa nguli, yaani wale wafungwa wasiosikia...

"tafadhali sana mkuu, kama ni kuhusu dom, mbona nina wiki moja mbele"
Aliongea sahi ili kujitetea kwa rais, mana alipewa mwezi mmoja ailete dom na sasa kumebaki wiki moja
"hilo sio tatizo linalokupeleka maweni, tatizo lako unanifichia mimi siri, nimekusomesha mwenyewe nje ya nchi leo ukipata jipu huniambii nilitumbue unakaa kimya, sasa hio kimya yako ndio inayo kupeleka maweni"
Sahi haamini kama mzee GU kajua kila kitu, yaani alitegemea hio ishu itakuwa siri lakini sasa imejulikana..
"labda ni siri gani unataka nikupe"
"mimi sichagui cha kunipa, nilikwambia kaa katika kitengo hicho unipe kila kitu unachokipata, lakini umekaa kimya"
"samahani mkuu, kwanza wacha nimalizie wiki yangu ya dom"
"kwanza kabla ya yote... Mtoto wangu Joseph jipu lake ni lipi"
"nae kushiriki kuiba dom"
"ati nini"
Mzee GU alishtuka kusikia mtoto wake ndie mshiriki mkuu katika ile dom inayotafutwa,...
"ni kweli mzee, na mshiriki wake mkuu ni... Lakini mzee wacha nimalize misheni yangu"
"nawe ni jipu, rubani, twende maweni"
"ah ah basi mzee... Hata General pia ni jipu"
"ati unasemaje... Huyu General tuliomuwcha punde pale kambini"
"ndio"
"enheee, ujipu wake"
"mi nadhani siri zite, nimeshakutumia leo kwenye Email yako, mpaka ya leo wanakwenda kuuza dom nimekutumia, siku anauza silaha nimekutumia, kwahi ki"
"subiri kwanza... Umesema wanauza nini"
Sasa kabla sahi hajajibu Mara simu yake ikaita, kuangalia mpigaji alikuwa ni Joseph,
"mzee, mtoto wako huyu ndie anaepiga"
Aliongea sahi huku akijiandaa kuipokea
"mpokelee usikilize anasema nini"
Sahi aliiipokea kisha akaweka laudi spika ili hata GU asikie
"ahahahahahahahaha, hatimae nimekujua rafiki yangu, yaani siamini macho yangu sheby, kumbe ni wewe mtoto wa General Nyange, umekuwa professional boy kwa kazi ulionayo"
Aliongea Joseph huku akiambatanisha na kicheko kikubwa sana, sahi alikata simu huku akimwambia mzee GU kuwa
"anaongelea nini"
"achana na hilo, tafuta dom ilipo"
"dom imeuzwa leo"
"naitaka... Ivi unajua thamani ya dom"
"hapana mzee, siifahamu"
"ile dom original ina thamani ya Shilingi Trillion 1000 za kitanzania, ni pesa nyingi sana ambayo inailisha Tanzania mwaka mzima... Tukajikamua na kuinunua, na hio ni siri hatakiwi mtu yeyote kujua bei ya dom,.. "
"khaaaaaaa, mzee, trilion buku unajua ni pesa ya kulisha nchi"
"tena sio kulisha tu, na maisha bora kwa kila Mtanzania"
Ndege ilitua mpaka Ikulu, sahi aliposhuka hakutaka kukaa, gari moja hapo Ikulu ilimchukuwa sahi mpaka TSS, aliingia huku akijifanya hajui chochote,... Alimkuta Joseph akiwa anazunguka katika kiti,...
"angejua baba yake kesha gundua kila kitu kuhusu yeye asinge zunguka na kiti hapa"
Aliongea sahi kimoyomoyo huku akimkaribia Joseph,
"aaahhhh sheby rafiki yangu, kwanini umekuja na staili yako ya sura mpya kumbe ni wewe, yaani siamini kama hukufa katika lile tukio"
"tukio gani"
"acha kunipumbaza akili wewe"
Joseph alitoa kitabu alichokikuta kule ndani kwa sahi
"hiki kitabu kinaelezea mambo ya plastic surgery, sasa kwani wewe kinakuhusu nini hiki"
"Joseph acha ukichaa, hiki si kitabu tu kama vitabu vingine"
"ni sawa, lakini kina maana gani kuwepo nyumbani kwako"
"mimi nilikipewa nikiwa narudi huku Tanzania na nilipewa kama kipeperushi tu.... Nipe dom yangu"
Aliongea sahi huku akinyoosha mkono,..
"dom gani sasa"
Sasa hivi Joseph hana utani tena na sahi baada ya kujua ni mtu aliosomea jeshi korea, tena kwa kufuzu mafunzo vizuri, na sio ujeshi tu sahi kujifunza mapigano aina yote kana kwamba hakuna pigano ambalo halijui katika hii dunia,
"wewe leo si ulikuwa nyumbani kwangu ukisachi, ata sijui ulikuwa unasachi upuuzi gani"
"sikiliza, kule kwako niliingia kwa kukuhofia na ni kweli, wewe ni mpelelezi wa serikali, na pia ni mwanajeshi,.. Kama sio kqenda kwako ningekujulia wapi, afu sasa nilichokikuta nyumbani kwako ni hard drive na vitu vingine, ukweli ni kwamba dom sijaikuta"
"Joseph, unajua unatafuta vita na mimi... Dom ipo katika kibegi changu, na sikutaka kwenda kuangalia kwasababu ulipo ongea na General nilisikia ukisema hakuna dom hapo ndani sasa nani kaichukuwa kama sio wewe"
Sahi alikuwa ni mpole kwasababu ya hio dom,
"sikiliza we sahi sijui ni sheby, sikiliza kwa makini sana... Sijakuta dom, nikudanganyie nini sasa kwani nakuogopa, una kipi cha kunitisha wewe mpaka nisikuambie ukweli, nakuogopea nini sasa acha ujinga wewe, tena angalia sana... Na sioni kama kuna haja ya wewe kuja hapa mana nimeshakujua... Usije hapa TSS, mwanzo na mwisho kukanyaga hapa"...
Sahi kusikia hivyo hakutaka kubishana, alitoka zake taratibu na kuichukuwa gari iliompeleka mpaka kwake,.. Alipofika kwanza alichangua vitu kuitafuta dom hapo ndani, alitumia masaa matatu kuitafuta katika chumba kimoja, akiangalia kile kibegi kilikuwa na Hard drive peke yake, waya waya zake zote zimechanguliwa na Joseph,.. Lakini sahi yote tisa... Sahi alichoka akili mpaka usingizi ukampitia papo hapo

Huku kambini sasa mzee General haamini kama sahi ni mtoto wake, mana kapewa taarifa wakati ndege ilisharuka, na licha ya kuambiwa na mwaju bado Joseph nae alimpigia..
"general Deo,... Yule kijana ni mtoto wangu"
"mmmhh unajua mimi siamini kama hata wewe pia unaotaga mchana, yule mtoto ni maji ya kunde, tena hafanani hata kidogo na mtoto wako, leo utasemaje ni mtoto wako"
"hahahahahaha... MTOTO WA RAIS GU mr Joseph John Kinywaji kanipigia simu kuwa kaona kitabu chenye maelezo ya plastic surgery,.. Na hicho ndicho kilichomfanya ajue kuwa ni mtoto wangu"
"kwahio unataka kusema mtoto wako kabadirishwa sura"
"haswaaa.... Na ile dom ataileta kwa njia moja tu"
"njia gani"
"utajua tu bwana deo"

Masaa kadhaa baadaye sahi anazinguka, lakini haamini kama kapoteza dom, na hajui imepoteaje, sahi aliumiza kichwa, huku akirudisha kumbukumbu nyuma kuwa ile dom mwisho alikuwa nayo wapi,... Kweli sahi alivuta kumbukumbu mpaka akajua kuwa siku ile aliingia nayo gest na yule mwanamke, lakini pia toka siku ile hakuitazama katika kibegi... Afu sasa kitu kilichompa wasiwasi ni pale alipo kumbuka kuwa mwanamke yule hakumlipaga na licha ya kutokumlipa pia hakuonana nae baada ya tendo...
"lakini yule ni changudoa tu, atawezaje kuiba, na istoshe ni mpole yule hawezi hata uizi yule"
Sahi alikuwa akijiuliza mengi sana juu ya hilo,
"lakini wacha Niende tu, ila uhakika sina"
Sahi aliona bora aende tu kule shivazi lakini hana uhakika,... Alinyanyuka kitandani na kuchukuwa gari yake aina ya VX limited yenye namba za kiserikali,...

Huku Ikulu kwa rais aliokuwa akifungua Email yake na kukuta video na sauti nyingi zikiwa zimetumwa,.. Sasa wacha turudi nyuma kule kambini jinsi sahi alivyo fanya juu ya kutuma hivyo vitu..

Wakati anajiandaa kutoka ili aje huku mjini baada ya kuona nyumba yake inasachiwa na TSS Group,.. Alikopi mafaili yote kwenye ile saa, unakumbuka nilikwambia ile saa ni over phone, saa iliokuwa na memory card kwa ndani ilitolewa na kuwekwa kwenye kompyuta kisha akanyonya data zote,.. Alipomaliza hapo alichukuwa simu nayo pia akanyonya data zote, sasa siri zote zikawa zipo katika saa, ila mpaka ujue saa hio ni simu, sio leo ni miaka...

Wakati sahi anazuiliwa getini na makamanda wasiopungua 50, general aliwahi kuchukuwa begi la sahi pamoja na simu, hivyo wakasahau kuchukuwa saa,.. Na hapo ndipo walipokosea... Sahi alitumbukizwa sero, wakati huo General na mtaalamu wake wanakagua laptop na simu zinawaandikia NO FILES, walishangaa mbona vyombo vyote havina data,... Sasa General alipokumbuka kuwa aliambiwa kuwa saa ya huyo kijana ina kamera na ni kama simu,.. Hio ni taarifa aliopolewa na lilr gaidi muuza silaha, mana kuna siku sahi aliwapiga picha kila mmoja kabla ya kuwauwa,... Sasa General baada ya kukumbuka hilo, akawa anakwenda kule sero kuchukuwa saa..
Sasa huku sero kumbe sahi nae machale yalimcheza, aliikunjua ile saa na ikawa katika mfumo wa simu, kisha akakusanya data zoote na kuzituma katika email ya PRESIDENT GU, sasa generally alipokuja alimkuta sahi anaongea na simu, na wakati huo tayari keshatuma muda tu tena hapo alikuwa anafuta vitu vingine,.. General alimnyang'anya saa hio na kuondoka nayo, walipofika walikuta data nyingi sana, walizifuta zoote, na kubaki na saa hio,..

Sasa wakati ule sahi anaondoka na raisi alicheka sanaaaa, maana yake ni kwamba wamefuta mafaili yote na wakati yeye alishayatuma, ndio pale sahi akacheka sana... Na mara ghafla na General nae akacheka sanaa, sasa kumbe maana ya kicheko cha General ni kwamba alijua ndege hio lazima ipite kushoto, hivyo walitega mitutu ya kulipua ndege,.. Lakini sahi aliiona kabla rubani hajapitia kushoto na uzuri ni kwamba ilikuwa ni ndege aina ya helikopta, hivyo ilizunguka papo hapo na kugeuza ili wapite kulia baada ya kuona mitutu inawaangalia,....

HIVYO NDIVYO ILIVYOKUWA KULE KAMBINI

Sasa sahi ndio anafika pale shivazi, ikiwa ni mida ya jioni jioni hivi,... Sahi alitega gari yake pembeni na kutulia, siku hio hakuwa hata na mudi ya mwanamke na pia hakuja kwa ajili ya mwanamke tena kaja kujaribu tu,..
Alikaa sana kama masaa matatu hivi, sasa akaona ngoja akanunue maji aondoke zake, mana kaja kufuatilia kitu ambacho hajui kilipotea vipi
Sasa wakati anashuka machangudoa wamemuona, saa ngapi wasimgombanie
"kaka, unanionaje jamani.."
"we kaka ona mie mlainii"
"jamani mkaka, mie ndio naanza leo"
"achana nao hao, mie bei nafuu usiku kucha"
Kelele zilikuwa nyingi sana na wakati huo anakumbatiwa na wanawake, wengine wanamshika shila nanii yake, yaani kila mtu anafanya juhudi na kazi yake.... Sahi alishikwa na hasira sema sasa sahi hasira kidogo huruma nyingi, aligundua sio kosa lao mana nao wanatafuta riziki,.. Hivyo haoni haja ya kuwakasirikia
"Samahanini jamani, leo sina mudi ya mwanamke kabisa yani"
Aliongea sahi kwa upolee
"mimi naweza kukufanya mpaka uwe na mudi ya mapenz"
Aliongea dada mmoja mzuri sana, yaani warembo wengi wapo kwenye kazi hizi, huyo mdada alikuwa ni mzuri sana
"najua unaweza, lakini leo sina mudi kabisa"
"sasa hapa umekuja kufanya nini,.. Au umekuja kutuchora tu"
"hapan.... Kuna dada mmoja hivi namtafuta"
"mmmmhhh kumbe kuna mtu unamtafuta.... Aisee tuondokeni kumbe hana lolote"
Aliongea dada huyo ambaye ni member wa kundi hilo,...
"lakini mdada huyo ni mtu wenu wa hapa hapa,.. Nitawalipa kama mtanionyesha huyo dada"
"yupoje yupoje huyo mdada"
Aliuliza yule mtoto wa kike,
"aahhh Kiukweli ni mdada mzuri, ana umbo zuri, mweupe hivi, nakumbuka siku ya kwanza alikuwa msumbufu kitandani"
"mmhhhh huyo atakuwa mgeni huyo, ila mimi sio msumbufu twende"
"kuwa siriasi dada angu, sikuja kufanya mapenzi hapa"
"hii ni sehemu ya kufanya mapenzi, na kama hujaletwa na hilo basi ondoka"
"nisikilizeni basi... Kwani shida yenu si pesa... Kwani mapenzi ni lazima"
"hela kwanza ndio uulize"
"nisipo walipa vunjeni kioo cha ile gari"
Sasa walipoangalia gari, waliona ina namba za serikali...
"jamani huyu atakuwa ni polisi,.. Oneni gari yake"
Aliongea dada mmoja na kuwafanya waote waogope na kuanza kukimbia huku sahi akisema
"kama ningelikuwa na nia ya kuwakamata ningeshawakamata muda mrefu tu,.. Ila shida yangu ni huyo mschana tu"
"sikiliza we kaka, usitake kutuingiza majaribuni,... Sisi hatumjui huyo mtu"
Sasa sahi akakumbuka alimuulizaga jina yule dada siku ileee,
"enheeee, huyo mdada anaitwa sauda"
Sasa waliposikia jina la sauda, wenyewe walisikitika sana tena sana.
"we leah?? Sauda si yule mgeni wenu cha uvivu"
"ndio yeye, na siku anayo ongelea huyu kaka ndio siku ya kwanza sauda anaingia kazini"
Sasa huyu huyu leah ndio alikuwa anaishi na sauda, je atamjuaje kama huyu ndio aliokuwa anaishi nae
"pole sana kaka yangu kwa nitakayokwambia kuhusu huyo mdada unaemtafuta"
Aliongea leah huku akisikitika sana
"kwani kafanya nini???... Kaacha kazi ya kujiuza au??"
"bora hata angeacha kazi na kubaki mjini.. Lakini sasa, pole mwaya kaka, kama ni huyo umemkosa"
"we leah??... Usimwambie ukweli bwana hata sisi ni wanawake tunahitaji wanaume..... We kaka, huyo mtu unaemtafuta kagongwa na gari juzi kafariki na sasa hivi yupo mochwariiiiiii, hapa tunatafuta pesa tumsafirishe.... Wewe kama vipi twende ukanitumie, mimi pia ni msumbufu kama yeye, mana unaonekana unapenda wasumbufu sana"
"ati unasemaje we dada??... Sauda amefariki dunia"
"sasa unashangaa nini?, ina mana hujui kifo wewe?"

Je?? Nini kitaendelea??? USIKOSE

ITAENDELEA.....
 
THE DOM

Sehemu Ya 18

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

sikiliza we kaka, usitake kutuingiza majaribuni,... Sisi hatumjui huyo mtu"
Sasa sahi akakumbuka alimuulizaga jina yule dada siku ileee,
"enheeee, huyo mdada anaitwa sauda"
Sasa waliposikia jina la sauda, wenyewe walisikitika sana tena sana.
"we leah?? Sauda si yule mgeni wenu cha uvivu"
"ndio yeye, na siku anayo ongelea huyu kaka ndio siku ya kwanza sauda anaingia kazini"
Sasa huyu huyu leah ndio alikuwa anaishi na sauda, je atamjuaje kama huyu ndio aliokuwa anaishi nae
"pole sana kaka yangu kwa nitakayokwambia kuhusu huyo mdada unaemtafuta"
Aliongea leah huku akisikitika sana
"kwani kafanya nini???... Kaacha kazi ya kujiuza au??"
"bora hata angeacha kazi na kubaki mjini.. Lakini sasa, pole mwaya kaka, kama ni huyo umemkosa"
"we leah??... Usimwambie ukweli bwana hata sisi ni wanawake tunahitaji wanaume..... We kaka, huyo mtu unaemtafuta kagongwa na gari juzi kafariki na sasa hivi yupo mochwariiiiiii, hapa tunatafuta pesa tumsafirishe.... Wewe kama vipi twende ukanitumie, mimi pia ni msumbufu kama yeye, mana unaonekana unapenda wasumbufu sana"
"ati unasemaje we dada??... Sauda amefariki dunia"
"sasa unashangaa nini?, ina mana hujui kifo wewe?"

ENDELEA.........

Kawaida ya wadada wanaojiuza ni moja tu, hua ukipita mitaa yao wao huona kuwamba umefuata miili yao, hivyo unaweza kupatwa na hasira za bure uje kumjeruhi mtoto wa watu,.. Sahi alikuja danguro hapa almaarufu kama shivaz, ili kupata angalau fununu kuhusu dom, mana yeye ni mpelelezi hivyo hata akikuangalia kwa macho tu anaweza kukuhisi kuwa una jambo unalotaka kulisema,
Sahi akiwa katikati ya wasichana watano wazuri waliokuwa wakihitaji mwanaume, lakini kwa bahati mbaya sahi hakufuata swala hilo, hivyo kila anachokiuliza anajibiwa tofauti

Sasa unashangaa nini??, ina mana hujui kifo wewe?"
Aliongea dada mmoja ambaye ni mmoja kati ya hao machangudoa, lakini kabla sahi hajatamka neno, ghafla Leah akasema
"weee nisha, kumwambia mqenzio kafa sio vizuri, kwa mfano ni wewe afu unasikia unaambiwa umekufa ungejiskiaje... Acha hizo bwana nisha"
Aliongea Leah baada ya nisha kuongea uongo juu ya kifo cha sauda,
"aahhh, unajua leah sio kosa langu, hata sisi ni wanawake tunahitaji mwanaume, iweje umuelekeze alipo sauda, yaani akafanywe yule sisi tuachwe? Kwani hatutaki hizo pesa"
"ni sawa nisha, lakini sio kwa kumtakia mwenzio mabaya....... Sikiliza we kaka, huyo mtu unaemtafuta, karudi kijijini, maisha ya kujiuza yamemshinda"
Sahi kusikia tu kuwa mtu huyo karudi kijijini, alikata tamaa ya kuipata dom, mana huyo ndio anaemhisi kuwa ndio kachukuwa dom
"sikiliza wewe dada leah, mi naona tuachie hapo tu mana matumaini ya kumpata hakuna... Nashukuruni sana kwa msaada wenu"
Sahi aliwaambia hivyo wadada hao huku akirudisha mguu nyuma ili kuondoka,
"kaka si unichukie basi"
Aliongea dada aitwaye nisha, eti achukuliwe na sahi aende akatafunwe,
"Kiukweli mimi ni mtu hadhi yangu, ukikijua cheo changu, hutotamani hata kulala na mimi... Nyote ni wasichana wazuri sana cha kuwashauri tafuteni mitaji muachane na hizo kazi, mkumbuke kuwa mtazeeka, na mkisha zeeka hamuwezi kuifanya hio kazi tena, sasa kama hujajichumia sidhani kama utaweza kuishi mjini tena"
Sahi aliongea kweli kila mtu aliingiwa na maneno hayo lakini kwao haikuwa na jinsi mana ni ukosefu wa ajira Tanzania hivyo hawana budi kuifanya kazi hiyo
Sasa baada ya sahi kuongea hivyo, ndio wakaamini kweli huyu mtu hakuwa akihitaji mwanamke kwa ajili ya mapenzi
"samahani kaka etu, kwani ulikuwa unamtakia nini"
Aliuliza nisha yule yule aliokuwa kimbelembele wa kutaka ngono zembe...
"Kiukweli, sina uhakika na hili, ila siku ya kwanza kufanya mapenzi na yule dada, siku ile kuna kifaa nilikipoteza, lakini sikua nimekagua begi langu, hivyo jana ndio nikaligundua hilo na kuwaza nije nijaribu hata kumuuliza yule dada,.. Lakini sasa hayupo Nitafanyaje"
Masikini ya mungu sahi aliongea kwa uchungu sana mana anajua dom ndio imeshapotea hivyo... Sasa baada ya sahi kuingea hivyo, nisha akadakia juu kwa juu
"leah, au ni kile kidude alichokuja nacho siku ile"
"labada itakiwa ndio hicho"
Sasa sahi kusikia kuwa kuna kidude alikuja nacho, ikabidi atoe simu yake na kuwaonyesha
"hicho kidude ni kama hiki"
Sahi aliwaonyesha pocha kupitia simu yake,
"ndio"
"ndio"
"ndio.... Tena nikamwambia aende akakiuze ili tupate pesa ya kula, Kiukweli hakurudi nacho kile kidude, tena akatuomba nauli tukampa arudi zake kijijini mana anatuletea jam tu"
Sahi alipandwa na kichaa kuskia hicho kidude kweli alikuwa nacho,
"nani anajua kijijini kwao"
Wote wakamnyooshea kidole Leah
"huyu hapa huyu, mana ndie aliemleta"
"eti dada, unapajua kwao vizuri"
Sahi alimuuliza leah ambaye ni mkuu wa kikosi hicho cha watu kama saba hivi, ila sasa wamepungua kwasababu sauda hayupo, ila hapa wapo watano na mmoja wa sita haijulikani alipo
"ni kweli napajua, mana ni kijiji kimoja na mimi"
Aliongea leah mschana mzuri aliobarikiwa kila ina ya uzuri wake, yaani umbo lake Mashalaah, sura yake Mashalaah.. Kifua chake Mashalaah, rangi yake ya maji ya kunde, ndio iliomfanya akawa mzuri kupitiliza, ila sasa kazi yake tu ndio chafu, yaani leah hata usiwe rijali lakini huezi kosa kumtamani, yaani ni bonge la toto wacha mchezo,... Alibarikiwa kupewa kalio mtoto wa kike, figa analo... Lakini kakosa mume, kakosa kazi ya maana... Serikali yetu hii bwana, inapoteza warembo, na pia sio leah tu karibia wote ni wazuri tena hua wanazidiana kwa vitu tofauti tofauti...

"tafadhali sana dada yangu, naomba unipeleke hapo kesho Please dada yangu"
Sahi alitamani hata kupiga magoti ili dada huyo akubali,...
"leah, mpeleke tu kaka wa watu"
Waliongea wale rafiki zake, huku leah akitamani kweli kumpeleka,... Machangudoa walikuwa wengi sana eneo hilo, yaani kila kikundi kinatamani sahi aponywe na kile kikundi kingine cha akina leah mana wanakaa kikundi kikundi, kwasababu kuna mijidume MoonVisioner.Blog.Com ngine inachukuaga wote wakamshike shike tu..
"sawa, nioo tayari kufanya hivyo... Lakini mimi sina nauli afu kwao ni huko tanga ndani ndani huko wanakuita magoma"
Aliongea leah tena kwa upole
"kuhusu nauli, kula, kuvaa, kulala, kila kitu niachie mimi... Kikubwa ukubali kunipeleka"
"basi nimekubali kukupeleka... Kesho njoo geto kwetu twende mana sisi mchana tupo nyumbani tu"
"hapana, yaani tunakwenda sasa hivi, yaani hata kukuacha hapa naona nitakupoteza na wewe"
Sahi aliongea hivyo huku akitoa waleti mfukoni na kutoa kiasi cha laki nne na kuwapa akina nisha laki moja moja kila mmoja, mana walikuwa watano pamoja na leah sasa kwakuwa leah anaondoka hivyo wapewe hao wanne kwanza...
"jamani, tunakwenda kulala hoteli gani"
Aliuliza leah huku akitamani naye apewe pesa,
"usijali mama utakwenda tu"
Sahi aliongea kwa furaha kubwa sana huku leah akisema tena
"mbona mi hunipi"
"wewe malipo yako ni tofauti na hawa, endapo kazi utakapoimaliza"
"mmmhh sawa, sasa hata ya matumizi sipati"
"sasa kula kwangu kulala kwangu, kuvaa kwangu shida yako nini dada leah"
"ok poa"
Leah alikubaliana na sahi... Huku wakiwaaga akina nisha, lakini nisha hakuacha kumtumia rafiki yake meseji,
"LEAH KIPENZI CHETU, KAMA KUTAKUWA NA TATIZO TUJULISHE... MANA WANAUME HAWAAMINI NDUGU YANGU... KUWA MAKINI SANA"
nisha alimtumia leah meseji hio, wakati huo leah ndio anapanda gari la sahi, kisha haoo

Wakiwa njiani, Leah ndio anaifungua ile meseji kisha akamjibu
"USIJALI NISHA NITAKUWA MAKINI, ILA NAWASIHI MSIGOMBANE, AFU PIA SIONI HAJA LEO YA KUWEPO HAPO, MUMESHAPATA PESA BORA MUONDOKE TU HAPO... KALALENI TU"
Leah anawapenda sana rafiki zake, na anawajua hawaishi kugombana pindi wanapoulizana vipatao walivyoingiza kwa siku fulani....

Leah kwa mawazo yake anajua anapelekwa hotelini, lakini alishangaa kaletwa Ostabei kwenye jengo la kifahari, yaani leah alibaki kushika mdomo kwa jengo lilivyo zuri na la kifahari hajawahi hata kuingia, yaani licha ya kuishi, hata kuingia kwa kuomba maji katika majengo kama hayo hajawahi...
"hapa ndio wapi kaka"
Leah aliuliza,... Machangudoa ni watu wenye hekima kwa wachache sema kazi yao ndio inawafanya kuwa wabaya...
"hapa ni nyumbani"
Sahi alijibu kwa ufupi, lakini leah hakuridhika na jibu hilo
"ni nyumbani kwako"
"ndio"
Leah kashangaa sana kusikia ni nyumbani kwake,... Afu kijana mwenyewe ni mdogo sana, hafananii na jengo hilo,...
"mkeo akiniona je"
Aliuliza leah
"sina mke"
"jumba lote hili unaishi peke yako"
"ndio"
"kwanini usioe na una maisha mazuri hivi"
"nitamuoa nani na wanawake wenyewe ndio nyie mliojikita kwenye kazi hizo..... Uliona wapi mwanaume akaoa changudoa"
Leah alijiskia vibaya kwa maneno hayo, mana pamoja na uzuri wake wote kuolewa kwake ni bahati sana, tena ataolewa na mwanaume ambae hamjui,.. Leah alitamani hata asishuke katika gari kwa aibu ya maneno ya sahi,... Lakini alishuka tu mana hawezi kukaa moja kwa moja katika gari
Lakini sasa sahi alipomwangalia, alimwona kavalia nguo zake zile za uchangudoa.. Yaani kigauni kilikuwa chepesi alafu kifupi kilichoishia katika mapaja juu kabisa... Sahi alimsogelea mpaka karibu yake na kumuuliza
"ivi huna nguo nyingine katika mkoba wako"
"mh mh sina kaka angu"
Jamani leah ni mzuri acheni utani, ni mtoto aliobarikiwa vyote kasoro kazi tu,.
"ukiwa na mimi hizi ngu hazifai, ni kqeli si kweli"
Aliongea sahi huku akikashika kale kagauni
"afu hata chupi hujavaa, ni kweli si kweli"
"kweli kaka angu, umejuaje"
"si nnaona hapo jinsi ulivyo mlaini"
"Samahani kwa hilo"
"siwezi kwenda na wewe hio safari ukiwa na nguo hizo... Naomba twende Kariakoo ukachukue nguo"
Aliongea sahi huku akirudi katika gari, leah hakukataa aliingia katika gari kisha haooo wakatoka

Jijini Dar es Salaam, ikifika saa mbili za usiku, utafikiri ndio kumekucha mana biashara ndio zinashamiri kwelikweli,.. Na ndio wakati wenyewe wa majira ya saa mbili za usiku,.. Kariakoo katika duka kubwa la nguo ambalo hata leah hakutazamia kuingia hapo mana ni maduka ya nguo za kike za matajiri... Na ni sehemu inayouza nguo aina zote
"fanya fasta twende"
Aliongea sahi huku leah akishuka na kuuliza swali
"nani atalipa"
"we kachague nguo mi nakuja kulipa"
Sahi anamueshimu leah kwakiwa anampa msaada mkubwa sana juu ya kupata dom,.. Mara kinasa sauti cha sahi kinasikika kikisema
"GU"
Ukisikia tu hio GU ujue ni raisi GU anampigia simu kupitia simu ya siri ambayo ipo oni muda wote,
"yes GU"
"BB, kesho una misheni gani"
"kesho naelekea tanga mkuu"
"kuna nini huko tanga"
"Nimemisi dom ipo eneo hilo"
"ok, kuna kazi nilitaka kukupa ya kumpeleleza waziri wa fedha.. Sasa maliza kwanza hio kisha utafanya kwa wakati mwingine"
"sawa..."
"afu hii sauti ya mtoto wangu,.. Uliirekodi ukiwa wapi"
"nilikuwa TSS"
"na alimpigia nani"
"alimpigia General Nyange"
"ahaaaa.... Ngoja kesho nitawaita Ikulu wote, nataka niwatumbue mbele ya kadamnasi"
"mzee, hata mtoto wako"
"hata baba yangu, kama ana kosa mlete nimtumbue jipu"
"mama yako je"
"BB, unaleta utani na kazi"
"nalo pia ni swali, mfano nimemkuta mama yako ni Jipu"
"aahhhhh mama tutaangalia na kosa bwana.... Weww fanya kazi maswali ya kijinga sitakic
"ahahahahahahahahahahaah.... Nimeshaju mama yako huezi mtumbua majipu wewe"
"pumbavu wewe"
Simu ilikata, lakini sahi aliingizia utani kidogo na mzee GU,.. Ila kale a taarifa kuwa General nyange na Joseph John kesho ni jipu mbele ya kadamnasi, shuguli nzima itafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam....

Huku ndani ya duka, leah kachukuwa nguo nyingi kweli, Madera, mahijabu na wakati yeye Mkristo, sketi za heshima magauni marefu, yaan nguo nyingi sana zilikuwa ni za heshima, mana kuambiwa na sahi kuwa akiwa naye hataki nguo aina hizo fupi fupi, hivyo leah kachagua nguo nyingi za heshima... Dukani palikuwa na mama wa makamo aliokuwa akiuza duka hilo,... Kumbe yule mama ndie aliekuwa akimchagulia nguo nzuri tena mama alikuwa akimsifu sana leah,...
"naona umekuja na mumeo.... Kiukweli ni wanawake wachache sana tulio bahatika kuwa na wanaume kama wakwako"
Aliongea mama huyo huku leah akitabasamu na kusema
"Ahsante mama angu"
"unajua binti, nyinyi wasichana wengi hamjui jinsi ya kuishi na wanaume zenu, na ndio mana hamuishi kuachwa"
Aliongea mama huyo, lakini alipomwangalia leah aligundua hakuwa na chupi, yaani nguo nyepesi ukivaa, lazima ijulikane
"hata hili nalo ni kosa... Unapotoka na mumeo kwenda sehemu yeyote ile nje ya nyimba yenu, unatakiwa uvae kiheshima, ili mumeo asifiwe kapata mke bora,.. Hiki kingua ulichovaa, unatakiwa ukivae chumbani kwako... Hii ni ishara ya kumtamanisha mwanaume mwingine ingali unae wakwako... Hili nalo ni tatizo wanaume wengi hawapendi kuona wake zao wanatoka nje na nguo za ajabu ajabu,.. Hebu njoo huku kuna taiti nzuri za kischana"
Mama alizidi kumtapikia leah maneno. Mazuri yaliomfanya leah kukaa kimya muda wote..
"ukivaa taiti kama hii, makali yako hayawezi kutetemeka na kumtamanisha mwanaume asie wako"
Leah alichukuwa nguo hizo, lakini sasa ni kazi bure kwa leah mana kazi yake haimruhusu kuvaa nguo kama hizo, na akivaa atakosa wateja, mana hatovutia tena...
"njoo huku kwenye chupi... Sasa hapa chagua chupi ambazo mumeo anapenda kuziona.."
Masikini ya mungu leah machozi yalimtoka, yqani maneno anayo yapewa laiti kama ingelikuwa ni kweli sijui ingelikuwa, sasa hapa leah ndio anajua kuwa changudoa, yaani anajuta mno...
"ona kama hii, yaani ukivaa chupi nyepesi kama hii, mmeo lazima apande mlima hata kama kachoka kiasi gani,.. Sikiliza binti yangu, mimi najua wasichana wengi hamjui sheria za ndoa, hamjui jinsi gani ya kuwashawishi waume zenu,.. Sio lazima umuite apande mlima... Nguo tu yenyewe inamuita"
Leah ndio kabisa machozi yanamtoka masikini ya mungu, wakati huo kawa mpoleew, maneno ya huyo mama yalimuingia vizuri sana..
"ivi ulisema unaitwa nani vile"
"naitwa leah"
"sasa unalia nini leah?"
"maneno yako Anti,.. Nahisi maneno yako yananitoa pangoni"
Leah alimaanisha kuwa maneno ya mama huyo yanamshawishi kuacha uchangudoa...
"una maana gani binti"
"anti, mimi nilikuwa siyajui hayo, naona unanifumbua maskio"
"usijali binti yangu, nanhata siku nyingine ukipenda kuja hapa njoo tu nikufundishe jinsi ya kuishi na mume wako"
"sawa anti, nitakuja tu"
"ok sasa hapa, pia una kosa moja tu"
"kosa gani anti"
"hapa kwenye nguo za ndani, unatakiwa uje na mumeo akuchagulie nguo anazopenda yeye... Hebu muite"
Maskini Leah ndio anazidi kuumia roho yake,.. Mtu huyo sio mume wake tena hapo anamtendea msaada tu wa kumpeleka tanga,..
"binti, we binti"
"abee anti"
"una nini??...muite baba watoto mje msaidiane kuchagua... Mana sharti mume ajue vigagula vyako, mana ni kazi yake kuvivua... Hebu muite"
Leah anafikiria ataanzia wapi, sahi wala hana mazoea nae tena ndio kwanzaa wamekutana leo, sasa aanzeje kumuita mume, na mbaya zaidi ni changudoa, yaani hata yeye mwenyewe anajionea aibu kujiita mke wa fulani,... Leah alilia sana huku akifikiria jinsi ya kumuita sahi aje wachague nguo za ndani, na mbaya zaidi hata jina la sahi halijui.. Yaani hamjui kabisaaaaaa... Leah anatamani kumwambia huyo mama kuwa yeye ni changudoa tu, na huyo sio mume wake.. Wakati huo mama anakazania leah amuite mume wake waje wachague nguo za ndani na hio ndio furaha ya ndoa mahaba ya dhati katika ndoa......

Je? Nini kitaendelea???... Leah atafanyaje na wakati keshasifiwa vya kutosha??? USIKOSE
 
TOP TEN
Week end imeanzaje mdau?
Mimi nipo fresh tu na hapa nimekuja kushusha kumi kubwa ya kumalizia week kisha kunapo majaliwa tutakutana Jumatatu halafu Premier League inaanza leo hivyo tutegemee kelele za vibanda umiza
Kuna usemi kwamba Hujafa hujaumbika ukiwa na maana kwamba usimcheke/dharau mlemavu maana hata kama umezaliwa na viungo kamili muda wowote unaweza kuwa mlemavu kutokana na maradhi au ajali
a1675050124b96678c02fd2d34e348f9.jpg

Kwa nchi zilizoendelea walemavu wanafaidi tu maisha maana wamejengewa miundombinu rafiki kuanzia shule,hospitali,makazini,barabarani n.k wakati kwa nchi zinazoendelea ulemavu ni kama laana maana ukiwa mlemavu tegemea kupigika haswa kuanzia shuleni hadi kufukuzia ajira ni shida
5d3879a9d19ff2d3a47b5b90fbbd6c55.jpg


Sasa lep tuangalie walemavu 10 wa macho (wasioona/vipofu) ambao walifanya mambo makubwa na hivyo kuonyesha walemavu wanaweza

Karibuni
........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom