VITA YA MAREKANI NA VIETNAM.
Sehemu ya 01:
Written by STILL B Dapeople.
Miongoni mwa vita isiyosahaulika kwa taifa la marekani ni vita kati yao na Vietnam iliyoanza mnamo mwaka 1955.
Vita maarufu ya Vietnam ni moja ya vita ktk historia ya marekani ambayo taifa kubwa na lenye nguvu Duniani lililazimika kuondoka uwanja Wa mapambano baada ya kushindwa vibaya. Mbio nyingi.......
Ilikuaje???????????.
Vita hii ilipiganwa kuanzia mwaka 1955 mpaka 1975, ilipiganwa maeneo ya Vietnam kwenyewe maana marekani hawana kasumba ya kupigania kwao.
Wao wakishalianzisha wanakufata wanahalibu kwako kwao RAIA wanakula bata.
Vita hiyo iliyowatoa jasho na kuambulia wahenga waliobaki na ulemavu aidha kupoteza siraha nyingi ilipiganwa maeneo ya loss, Vietnam na Cambodia.
Kw juu juu ilikua vita iliyopiganwa kati ya Vietnam kaskazini na Vietnam kusini.
Lkn nyuma ya pazia ilikua ni vita ya kijasusi kati ya wababe wa dunia Wa wakati huo. Yaani MAREKANI na URUSI ya kisovieti( proxy war) huku kila mbabe akitaka kupandikiza itikadi yake kwa upande huo.
Marekani alitaka UBEPARI utawale na Mrusi alitaka UKOMONISTI utawale. hapo chacha kimakonde tunaitaga chamaki ntu na ntu vitani.
Vietnam ya kaskazin ilisapotiwa na urusi ya wakati huo (USSR), China na nchi nyingine za kikomonisti. Huku Vietnam ya kusini ikisapitiwa na marekani, Korea kusinna Australia, Thailand na nchi nyingine zilizokua zikiponga ukomunist.
Wakati vuguvugu la vita limeanza kukolea mwaka 1950 marekani alituma kikosi cha majasusi wake chini Vietnam wakati huo ikiwa koloni la mfaransa ikijulikana km French indochina kw ajili ya mafunzo , udukuzi, na kukusanya taarifa za kijasusi kwa askari wa Vietnam ya kusini na kuviandaa vikosi vyake kw ajili ya mipango ya kukata na shoka.
Ilipofika mwaka 1961, wakati vita imekolea, marekani kw kutumia taarifa za kijasusi ilizokusanya ilipeleka kikosi maalum cha makomandoo wa jeshi la anga maarufu km Green Berets kw kazi kuu ya kufanya operations za kimyakimya za anga ili kulidhoofisha jeshi la Vietnam kaskazin.
Kikosi hiki kiliungana baadae na kikosi cha makomando wa anga waliojulikana km ECO 31 na US marines.
Hata hivyo kutokana na udhaifu wa taarifa za kijasusi vikosi hivi havikufanikiwa sana hali iliyopelekea kuvunjwa na kuundwa kikosi maalum kingine mwaka 1962, kilichoitwa U.S military Assistance command , Vietnam (MACV) kilichokua chini ya idara ya Usalama ya marekani .
..ITAENDELEA.........
ikumbukwe story hii imepatikana ktk vitabu vya stories zilizowahi kuikumba dunia hiii.