Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo katika Historia

1964 - Jim Reeves anafariki.
Alikuwa ni mwimbaji mashuhuri wa muziki huko Marekani.
Alifariki kwa ajali ya ndege.
5cfddcf308c3f8bca1e2ad1729b50ef0.jpg
Alikuwa na miaka 40 tu
:
Silent Night
Merry X mass
......
 
Leo katika Historia

2012 - Michael Phelps ambaye ni muogeleaji anavunja rekodi ya kushinda medali nyingi kwenye michuano ya Olimpiki baada ya kushinda jumla ya medali 22 kwa kushiriki michuano mitatu ya Olimpiki ambayo ni ya mwaka 2004, 2008 na 2012.
Jamaa anajua kupiga mbizi huyo aisee
 
THE DOM

Sehemu Ya 7

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

Ghafla simu ya muarabu inaita...
"hello mr nyange"
"yes mnaweza kuondoka sasa"
Aliongea mr nyange, huku mwarabu akikubali na kusema
"ok, see you next month"
"ok, wish you a good luck"
"ok... "
Mwarabu aliwasha gari ikawaka, na hapo wapo tayari kwa kuondoka...

Sasa huku chumbani, kumbe sahi aliacha simu, na huezi amini simu yake ilionewa na mwaju, na kama unavyojua simu ya sahi ilivyo beba siri nzito ambazo anawasiliana na Mheshimiwa rais, sasa mwaju keshaipata simu hio,....
"yes, nimefanikiwa kupata simu,.. Sasa wacha nimpelekee General Nyange aichunguze"
Lakini sasa cha ajabu na cha kushangaza, mwaju aliitupa simu kitandani baada ya kuona picha juu ya screen sever, mwaju alishangaa huku akiishika tena hio simu na kuangalia hio picha kwa makini...
"huyu kijana, ana uhusiano gani na huyu mtu, mbona picha yake ipo hapa"
Mwaju Alijiuliza swali hilo huku akisema tena kuwa
"lazima General nyage mjue huyu kijana"

ENDELEA..........

Wakati huo General nyange akiwa ndio anaweka simu yake katika mfuko, kisha wakaingia ndani wakiwa na makamanda wasiopungua 15,ambao alikuwa nao kwenye sakata lile la kupakia silaha katika gari la kawaida,...
"sasa, kila mmoja afe na mzigo wake, afu longo longo sipendi"
Aliongea general nyange, huku makamanda ambao ndio walimu wa wanafunzi wote,...
"sawa kamanda,.. Lakini mkuu mbona ishu hii tunayo muda mrefu na hakuna aliejua"
"nalijua hilo, lakini bingo la leo,... Mtafurahi... Kuleni milioni kumi kumi kila mmoja"
Aliongea general nyange huku akiweka briefcase mezani ili kutoa vitita kadhaa kwa ajili ya kugawanya.. Kweli kila kamanda alipewa kiasi cha milioni kumi, huku akiwataka waelekee katika nyumba zao za hapo hapo kambini,... Kumbe wanafanya biashara ya uuzaji wa silaha za serikali

JAMANI SIMULIZI HAINA UKWELI JAMANI, MSIJE MKAANZA KUSEMA KUWA NI KWELI.... MANA NYIE DUUU

Sasa huku ndani kwa sahi, mwaju akiwa ndio kaishika ile simu ya kijana BB,... Lakini ghafla alishangaa kuona picha moja ikiwa katika screen sever, mwaju aliitupa ile simu mezani na kuzidi kujiuliza, huyu kijana ni nani hasa, yaani licha ya kazi yake hii ya upelelezi, bado ufamilia wake una mashaka, mana inawafanya watu kujiuliza mara mbili mbili,...
"huyu mkaka ni nani haswa.. Na hii picha inamhusu vipi"
Aliongea mwaju huku akiichukiwa ile simu na kutaka kumpelekea General ambae ndio mkuu wa majeshi,...

Lakini kabla hajapeleka, kwanza alijiuliza,...
"au General atakuwa ananichezea akili, mana naweza kumlipoti mtu kumbe ndio najilipoti mimi mwenyewe"
Aliongea mwaju katika moyo wake
"ngoja niiweke kwanza... Nikipata kitu kingine, itakuwa bora zaidi..
Mwaju aliirudisha ile simu kisha akawa anaendelea kutafuta kitu kingine, lakini ukumbuke kuwa sahi hakuja na begi lolote hapa jeshini, kwani hakutarajia kuanza mafunzo siku hio hio, hivyo nafasi ya kwenda nyumbani kwao kuchukuwa baadhi ya vitu, alikosa kabisa na ukizingatia leo ana siku ya pili toka aanze mafunzo yake,.... Mwaju hakutaka kuipeleka ile simu kwanza kabla mpaka apate kitu kingine tofauti na simu... Mwaju aliendelea kutafuta uvunguni, funua makabati ambayo sahi bado hajayawekea kitu chochote kile,...

Sasa huku msituni pembeni na eneo la jeshi palipokuwa na kazi ya kupakia silaha za jeshi,...
Sasa Mwarabu akawasha gari ikawaka, lakini kila akiingiza gia na kutaka kuondoka, inakataa alishangaa ni kwanini gari imekuwa na hitilafu kabla ya kuondoka pembezoni mwa jeshi,...
"hebu kaangalie au kuna jiwe"
Mwarabu alimtuma mtu wake, na wakati huo kiza totoro, yaani hata tochi hazikuwepo eneo hilo, kutokana na kazi waliokuwa wakifanya watu hawa... Yule kijana alitoka katika gari, na kuanza kumulika mulika kwa siri sana, ili tochi isionekane na watu wengie,.. Sasa kijana akaona propela imefunguliwa,.. Akaona wacha akaifunge,... Kitendo cha kusogea ni kitendo hatari mno kwa kijana huyo,...

Ukimya ulitawala chini ya gari, hakuwa na mtu akicheza cheza wala kuhema,...
"mbona harudi huyo,.."
Mwarabu Alimuuliza jamaa mwingine aliokuwepo eneo la kibini, mana hamuoni akirudi baada ya kuchungulia,...
"si unamjua jamali alivyo kalegea? Unaweza ukakuta kalala huko ndani"
Aliongea jamaa mmoja huku akishuka naye kwenda kumwangalia jamali, kweli alipofika chini ya gari alimkuta jamali akiwa kalala, lakini hajajua kuwa ni mtego..... Wakati huo Mwarabu anachukuwa simu yake na kuwapigia wanajeshi waasi ambao waliasi jeshi, ila sio kuwa ni wa kitanzania, bali mwarabu huyu ni raia kutoka kenya, hivyo anawapigia makamanda wao wanasubiri katika njia fulani ya chocho mana hawapitii njia ya moshi ya moja kwa moja, watapita chochote na watapitia boda ya namanga,... Hivyo wanatakiwa kusubiri upande huo huo wa Kenya,..
"eee halo jabir"
"yes mkuu"
"maili tisa tusubirini"
"sawa mkuu, tupo ready kwa hali yeyote ile"
"ok"
Mwarabu anakata tu simu, alishangaa anamulikwa tochi ya macho kisha ikazima,.. Alijua ni watu wake, kumbe sio, ni sahi, jeshi la mtu mmoja.... Mwarabu alitolewa ndani ya gari na wakati huo hakuwa na silaha yoyote ile kutokana na mazingira walio kuwepo, yaani silaha wanazo katika viuno vyao, lakini hazikiwa tayari kwa tukio, mana pembezoni ya jeshi, gaidi gani anaweza kuja.... Sasa kumbe sahi alikuwa akiwavunja shingo mmoja baada ya mwingine,... Hata mwarabu kwake alikuwa mlaini sana kitokana na kustukiza, yaani hakutegemea kukutana na swala kama hilo....
"General nyange umetusaliti"
Aliongea mwarabu huku akiwekwa vizuri,
"hakuna cha General hapa.... Nataka uniambie, silaha mnapeleka wapi"
"kwani we nani????.............aaaiiiiiii"
Sahi hatakagi kuulizwa wakati yeye kauliza, Ajibiwe kwanza ndipo aulize,
"nakuuliza tena, silaha mlizipakia mnapeleka wapi"
"hapana kamanda, sisi tumeagizwa tu, tuna wakuu wetu nchini Nairobi"
"kwahio hizi silaha mnapeleka Nairobi?"
"ndio... Tumeagizwa tu... Lakini wewe si nilikuwa na wewe hapa, mbona umenisaliti"
Sahi kuona mwarabu anaropoka ujinga, zake ni kuvunja shingo tu, mana mambi ya kutumia silaha kwa sehemu kama hio ni hatari sana,.. Sahi baada ya kummaliza yule gaidi la kiarabu, aliingia katika gari na kuutoa ufunguo, ila aliuweka humo humo kwenye gari ila sio kuupata kirahisi,... Baada ya hapo alizunguka katika gari na kuimulika pleti number ya gari hio, kweli ilikuwa ni gari ya kenya..... Sasa kumbe hio saa ikikumulika sio kuwa ni tochi, bali ni flashi ya kamera, hivyo hapo kapiga picha vizuri sana...

BB hakuwa na haja ya kuondoka wala kulisumbua gari, alivua gropsi zake baada ya kazi kisha, akazificha mahali kana kwamba hazikufaa kutumika tena, mana kama angewashika bila gropsi, katika upelelezi angejulikana kupitia finger print,... Sahi taarabu anarudi kambini tena kwa umakini wa hali ya juu, wakati huo ni mida ya saa nane za usiku,... Sasa saa ngapi mwaju hajatafuta mpaka kachoka, kila kona ya makabati anakutakana na zana za kijeshi tu, mana kila chumba cha mwanafunzi kinatakiwa kukaa na kila kitu cha kijeshi,.. Sasa mwaju baada ya kutafuta mpaka kuchoka, alijikuta kapitiwa na usingizi,.. Wakati huo sahi ndio anaruka ukuta na kuingia katika anga za jeshi... Yaani ndani ya jeshi, huku akianza kukroo, taratibu... Kwa bahati mwaju anazinduka na kujikuta yupo chumbani kwa sahi,.. Mara moja bila kuchelewa aliamka kwa haraka haraka ili arudi alipotoka

Sasa ile anafika tu nje, ndio anakumbuka kasahau simu ya sahi, ili ampeleke general nyange,.. Lakini alichelewa ilimbidi tu aendelee na safari yake ya kwenda bwenini kwake, wakati huo sahi ndio anaingia chumbani kwake, yaani mwaju angerudi tu, lazima angelikutana nae njiani..... Sahi alipoingia ndani, kwanza alihisi harufu ya mtu aliotoka muda sio mrefu,.. Aliingia kwa umakini zaidi lakini hakukuwa na mtu, kitu cha kwanza kwanza kabisa alikimbilia simu yake, kisha akafungua na ile saa yake ikawa katika mfumo wa simu,... Kumbe sahi alilirekodi lile tukio mwanzo mwisho walipokuwa wakipakia silaha, sahi aliituma ile video iingie kwenye simu yake,.. Pia zile picha za magaidi pia alizikopi katika simu yake ya kwaida, ila kwenye saa bado vipo vyote,

Asubuhi kama kawaida ni mazoezi kwa kwenda mbele, sahi hakutaka kumwambia mtu kitu chochote kile juu ya tukio la jana, mana hatakiwi kujulikana kama ni yeye ndio kafanya hivyo,... Katika mazoezi kuna makundi mawili, sasa sahi kachagua kundi la kwenda mbali kidogo kwa ajili ya mazoezi, yaani sahi hana wasiwasi mana anajiweza kivyovyote vile,... Sasa hili kundi la pili, katika mazoezi yao likaona kuna gari, ndani ya kundi hilo mwalimu anajua kuhusiana na gari hilo, ila wanafunzi hawajui jambo kama hilo, na nia ya sahi ni kwamba anataka wanafunzi wote wajue kuwa kambi yao inatoa silaha na kuwauzia nchi jirani,.. Kwakuwa mwalimu hawezi kuifanya kuwa siri tena, alijifanya na yeye hajui kisha akapiga simu kwa General nyange,
"mkuu, kuna gari hapa imetelekezwa"
"gari??.... Gari gani"
"gari hii inaonesha ilipakiwa silaha mkuu"
Sasa kamanda kusogea karibu, ghafla anawaona wale majangili waliouziwa silaha....
"mkuu... Kuna watu watatu wanaonekana kupoteza maisha"
Unajua huyu kamanda, anajua kila kitu, lakini hapo ni mbele ya wanafunzi, ambao hawajui lolote, hivyo lazima ajifanye hajui chochote kile kuhusu kupakia kwa silaha hizo..

Nusu saa mbele, gari limesukumwa mpaka kambini, tena lina silaha zake zote, hakuna hata moja ambayo imesafirishwa,.. Gari lilifikishwa katika kambi ya jeshi, huku maiti waliokutwa katika eneo la tukio wakipelekwa hospitali iliopo hapo hapo jeshini, yaani hospitali ya jeshi
"kamanda kuti??, haraka sana naomba upelelezi ufanyike"
Aliongea general nyange huku akiwa na wasiwasi juu ya tukio hilo mana wao ndio waliouza silaha za jeshi na kushindikana kwenda,..
"sawa mkuu"
Kamanda kuti alikwenda katika ile hospitali akiongozana na General nyange,
"dokta, tunaomba uangalie finger print za muuaji katika hizo maiti"
Wakati huo kikosi cha pili cha akina sahi bado kipo msituni na hakijui lolote kuhusu suala la kukamatwa kwa gari yenye silaha, ila sahi mwenyewe kimyaa, nazidi kujifanya hajui mazoezi...

Sasa katika hali ya kuwageuza wale maiti,... Kumbe kuna mmoja alikuwa hajafa vizuri, saa ngapi hajatoa macho, na kumwona General nyange uso kwa uso,...
"vp kijana... Habari yako... Nini kilitokea usiku wa jana??"
General Nyange aliuliza kwa presha ya hali ya juu mno,...
"eti, unamjua mtu aliowafanyia tukio hilo"
Yule gaidi alitikisa kichwa kuashiria ni kweli anamjua mtu aliowafanyia hivyo, kwahio yupo tayari kumwambia General nyange kwakuwa ni mtu wao,... Wakati huo sahi hajui lolote lile kama huku kumbe kuna mmoja hajapatwa na umauti,....
"dokta, tunaomba ututolee huyu kijana na kubaiskeli cha wagonjwa... Afu kamanda kuti, naomba unikusanyie wanafunzi wote hapa kambini"
Aliongea general Nyange huku akiwa na hasira juu ya tukio hilo,....
"lazima tufahamu..... "

Nusu saa mbele, kundi la pili linawasili kambini kutoka mazoezini, wakati huo kundi la kwanza lipo katika paredi ya utulivu,.. Mbele ya paredi yupo yule gaidi alio tayari kwa kumtaja mtu aliohusika na tukio hilo..
Sasa sahi hajui hili wala lile,... Alitahamaki kuona sura ya yule gaidi ipo hai,..
"mungu wangu... Kumbe hili fara halijafa"
Aliongea sahi huku wasiwasi ukimjia, kwani nia yake ni kugundua mengi zaidi katika kambi hio, sasa endapo atagundulika mapema, itakuwa tabu
General leo ndio aliokuwa akiwapanga line wenyewe, yaani mpaka wanafunzi wote waka kaa sawa katika line zao,...
"gidi... Naomba utuonyeshe mhusika wa tukio la jana"
Sahi pale alipo moyo ulikuwa unakwenda mbio,.. Mana lazima ajulikane ni yeye,... Sasa kumbe huyu gaidi ha......

Itaendelea.......

Je?, gaidi ana nini??... Na je atafanikiwa kutaja.... Sahi atagundulika kwa njia gani??? USIKOSE

ITAENDELEA.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom