Wale wa mr x....
~ SIKU MOJA KABLA ~
"Ndio bosi ni Holt Mandu Academy, sawa kabisa nimeielewa na leo ndio nakutana na vijana niliopanga nao issue na ili waone tofauti nawalipa asilimi 60 kabisa katika makubaliano.... sawa bosi hilo halina shida kabisa andika kabisa The Game is Over"]
alionekana Tyga akiongea kwa simu akiwa chumbani mwake kule hotelini na baada ya hapo alitoka nje na kukodi taxi kama kawaida mpaka maeneo ya kusini mwa jiji la Mumbai aliposshuka na kuingia kwenye bar moja huku muda mwingi alionekana kuwa bussy na simu.
Alifika na kukutana na jamaa mmoja baada ya kusalimiana alimpa ishara amfate na hapo ndipo walipoelekea usawa wa kauta na kufungua kilango kilichotokea kwenye kiukumbi kidogo kirefu kilichokuwa kinawaka taa zenye mwanga hafifu huku kikiwa na milango mingi pande zote.
Baada ya mwendo kidogo ndipo yule mwenyeji wake aliyekuwa na asili ya ki Asia alipofungua moja ya mlango uliowakutanisha kwenye ukumbe mwengine ambao kulionekana watu wakijidunga wengine wakifanya mapenzi bila kujali huku moshi wa marujuana ukiendelea kufuka kwenye vinywa vya wale watu.
waliachana nao na kufika mbele ya mlango mmoja ambao juu yake Tyga aligundua kumetegwa kamera kimtindo.
Baada ya mwenyeji wake kubonyeza alarm sauti ilisikika kutokea kwenye kitasa kilichokuwa na spika ikiwaruhusu waingie na huko walikutana na Bonge la mtu (mnene sana) aliyekuwa kakaa kwenye kiti cha kuzunguka huku mwili wake ukiwa umepigwa machata ya michoro ya ajabu ajabu.
"Umeleta Advance?"
aliuliza yule bonge pindi Tyga alipotoa bahasha ya khaki iliyovimba ambayo ndani yake kulikuwa na noti za dollar mia mia karibu vibunda kumi na kila kibunda kimoja kilikuwa na noti mia.
"Safi sana hahahaaa. umefanya nikupe vijana wangu wa daraja A hahaha Zanjili, Jackson, Vijay, nyinyi ndio mtafanya kazi tuliyotoka kuijadili na huyu jamaa kesho"
aliongea yule kibonge mara baada ya kuchana bahasha na kuzihesabu zile pesa.
Baada ya kila kitu kuwa sawa Tyga alikabidhiwa funguo za gari ambayo ndio alitakiwa atokee nayo eneo la tukio na kisha alipewa bastora mbili ndogo zilizojazwa risasi za bandia.
"Mchezo ni mwepesi sana na utachukua dakika kumi tu, wewe itakubidi uwe makini kuifatilia gari yao pindi itapokuwa inatoka mpaka kukaribia ile kona subiri kama dakika tano then unatokeza mkuku na kumuhadaa binti unayemuhitaji kwa kuwapiga risasi za kifua vijana wangu wataojifanya wamekufa ili kumtoa hofu bint ndipo utadondosha bahasha yetu yenye hele zilizobaki na utokomee eneo lile then mchezo uliobaki watajua vijana wangu jinsi ya kuumalizia."
alitoa maelekezo ya mwisho yule kibonge na kupeana tano na Tyga aliyeikubali moja kwa moja ile mbinu na kuondoka.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kesho yake kumbe kuanzia muda mr Rajesh akiwa na mkewe na Asha wakitoka tayari Tyga alikaa sehemu husika na mara gari ya mr Rajesh ilipoanza kutoka aliifata nyumanyuma hadi yote yaliyoenda kutokea pale na yeye ndie aliyekuja kumuhadaa Asha kama muokozi wake baada ya kuwapiga risasi za uongo wale watu waliojiziba nyuso na kuangusha bahasha iliyokuwa na salio pale chini kisha kumfata Asha aliyekuwa ameinama chini ya gari ya mr Rajesh ambae alishafariki na mkewe kisha akamshika bega Asha ambae alipogeuka Tyga alimuonesha tabasamu kama alivyomfanyia siku ile aliyomzawadia mdori wa bata na siku waliposhuka uwanja wa ndege wa Mumbai na muda huo ilikuwa mara ya tatu wanatazamana uso kwa uso na mtoto Asha.
* * * * * *
"Usiogope bint ni salama sasa"
aliongea tena Tyga kwa lugha ya Kiswahili ambayo alijua ndio anaielewa kiufasaha sana mtoto Asha na kumuinua pale chini na kumkumbatia.
Hakuwa na jinsi Asha zaidi ya kumkumbatia yule baba (Tyga) aliyegeuka kuwa mkombozi wa maisha yake muda ule huku akifarijika pia kusaidiwa na mtu aliyemuona tangia uwanja wa ndege nchini kwao (Tanzania) na aliamini moyoni mwake kuwa Mungu ameamua kumuonesha muujiza ambao hakuwahi kuuota wala kusimuliwa hata siku moja kama upo.
Yaani anawapoteza wenyeji wake waliojitolea kumchukua tangia huko kwao katika mazingira ambayo hata kama asingeuwa na wale watu bado aliamini angekufa kwa kuuawa hata na wanyama wakali katika msitu ule kwa kukosa muelekeo wapi aende vipi aombe msaada nani angemuelewa ikiwa hajui kihindi hata kidogo? tena mbaya zaidi alisikia sifa za ubaguzi za watu weusi tokea yupo shule..!
Lakini leo hii anasaidiwa na mtu wa kwao kabisa baada ya kumfariji tena kwa maneno ya lugha ya Kiswahili.
"Pole sana mtoto usiogope haya twende haraka tuondoke hapa kabla hawajaja wengine"
aliongea Tyga na kumshika mkono Asha ambae awali alisita na kugeuka kutazama walipolala wafadhili wake mr&mrs Rajesh
"Tuwachukue babaaa na mamaa"
"Hatutaweza binti wameshakufa hao"
ndivyo alivyojibiwa na Tyga ambae alimshika mkono nae Asha alimfata hadi kwenye gari aliyokuja nayo Tyga na kuingia ndani yake ambapo gari ilichekechwa na kugeuzwa kiufundi palepale na kuanza kurudi ilipotoka huku Asha akiwa hajui wanapoenda lakini hakuacha kuchungulia nyuma kupitia kioo cha ndani cha ile gari akiwa haamini kama kweli maisha ya watu wenye hela zao aliotokea kuwapenda na kuwazoea wiki chache tu alizokaa nao kama ndio kweli yameishia pale msituni.
Hakuna aliyejua kilichoendelea baina yao baada ya kufika maeneo ya mbali na eneo la msitu huku Asha akiwa hana la kufanya zaidi ya kumsikiliza yule aliyeamini ni muokozi wake chochote atachomwambia.
"Unaitwa nani binti?"
"Asha"
"Ooh! Asha nani?"
"Asha Hussein"
"Sawa mimi unaweza kunita Uncle Tyga"
"Anko Taiga!!"
"Eeh, Uncle Tyga ni mfanyabiashara wa Tanzania ninaezunguka hapa India na kwengineko, nilikuona kwenye ndege si ndio wewe?"
"Eeh, Uncle Tyga"
"Basi usiwe na wasiwasi sawa eeh"
"Sawa lakini naomba nisaidie unirudishe kwetu"
"Hilo halina tatizo Asha kwani huku uliokuja nao wale kina nani?"
"Wafadhili walinichukua ili wanisomeshe na ndio walikuwa wananipeleka shule"
"Oooh! pole sana kumbe unapenda kusoma?"
"Ndio"
"sasa kama anatokea mfadhili mwengine akachukua nafasi ya wale waliokufa ili akusomeshe huku, utakuwa tayari tena kurudi nyumba?"
"Hapana kama nitapatiwa shule napenda sana nisome"
"Basi vizuri"
Ndivyo walivyoanza kuzoeana baina ya Tyga na Asha kipindi hiko gari ilikuwa katika High Way speed kali na kuanza kuliacha jiji la Mumbai huku Tyga akimsemesha semesha Asha ambae mwishoe alipitiwa na usingizi na baada ya gari kutembea kwa zaidi ya masaa manane tena kwa speed ya nguvu hatimae waliingia katika jiji la Delhi ikiwa tayari majira ya usiku.
aliamshwa Asha na kumfata mwenyeji wake mara walipofika kwenye nyumba moja ya kizamani ambayo ilionesha ilikuwa haikaliwi na mtu kwa muda mrefu hasa mara baada ya kuingia ndani na kukuta mazingira yalivyo.
"Karibu Asha utakuwa unakaa hapa kwa muda na habari njema ni kwamba nimelifikiria sana swala lako na nimezungumza kwa ujumbe wa simu na bosi wangu ninayefanya biashara zake kuwa yuko tayari kushika nafasi za wale wafadhili na atakusomesha hadi pale unapohitaji mwenyewe na kukuhudumia kwa kila kitu"
habari hizi ziliukonga moyo wa Asha na kujikuta anasahau matatizo yalliyotokea muda mfupi na kumpigia magoti Tyga kwa kumshukuru.
"Hapana usinishukuru sana mimi. Utamshukuru vizuri bosi wangu siku ya kumuona"
"sawa Uncle Tyga, kwa hiyo nitasoma?"
"Utasoma Asha"
"Lini Uncle"
"Kesho jioni nitakupeleka kwenye hiyo shule ni nzuri na ni salama zaidi ya ile waliyokuwa wanakupeleka wale, si umeona mwenyewe njiani kulikuwa na majambaza..?"
"Ndio Uncle"
"Basi usijali Asha, si umesema unataka kuwa daktari"
"eeh"
"Basi huko utakuwa zaidi ya daktari na hii ni kwa mujibu wa bosi wangu ambae kumbuka ndie msaada mkuu kwako"
alisisitiza Tyga na kumpatia Asha mfuko uliojaa nyama za kuku wa kukaangwa sambamba na mikate ya maziwa huku mfuko mwengine ukiwa na Juice kubwa ya matunda.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana kwa Asha na Tyga ambae mpaka muda huo hakumuambia Asha jina halisi la huyo bosi wake ambae Asha nae alimjengea moyo wa upendo na ukarimu kabla hata hajamuona huyo bosi na aliamini kuwa ndie mkombozi wake wa elemu ambayo alidhani kashaikosa pindi aliposhuhudia wafadhili wake wakiuawa.
* * * * *
Siku mbili baadae Tyga akiwa sambamba na Asha ndani ya gari majira ya jioni walifika eneo moja lenye mitimiti mingi baada ya mwendo mrefu na kufika kwenye geti moja lililoandikwa kwa lugha ya kijapani na kuingia mara baada ya kufunguliwa na walinzi walioonekana eneo lile.
Asha hakujua kama pale anapoletwa ndio shule kwenye hadi baada ya kuambiwa na Tyga ashuke kwani wamefika shule.
Mazingira hakuyaelewa kwani hayajakaa kishuleshule na hakukuonesha dariri ya watu kufika mara kwa mara eneo lile kutokana na kupooza kwake.
Lakini ukweli ukabaki kuwa pale ndio shule penyewe alipoahidiwa na bosi wa Tyga kuwa atasomeshwa bure mpaka atimize ndoto zake.
Hali ya mazingira awali yalimuia ugumu sana kutokana na uchache wa wanafunzi ambao asilimia kubwa walikuwa wanawake lakini siku hadi siku alianza kuyazoea na kuyapenda masomo ambayo walikuwa wanafundishwa pale shuleni na walikuwa wanalala pale pale huku zile siku za mwisho wa wiki alikuja Tyga na kumtembelea huku akimletea zawadi mbalimbali kutoka kwa bosi wake ambae sasa na Asha alimtambua kwa jina la mr X.
"Msalimie sana mr X uncle mwambie nampenda sana nashukuru kwa msaada wake"
yalikuwa ni maneno ya Asha siku moja mara baada ya kuletewa zawadi nyingi na Tyga huku akimwambia zimetoka kwa bosi wake ambae ni mr X na Asha alizidi kumpenda na kumuhusudu mr X kupita maelezo kwa kuamini ndie mfadhili wake na mtoa msaada kwa yote yale yanayofanikishwa na Tyga bila kujua kumbe yupo katika mchezo wa vipofu alioingizwa na mr X na kupofuka pasi na kujitambua Asha.
Ile shule mbali na kuwa na walimu wachache waliokuwa wanadeal na swala la mifupa ya binaadamu tu lakini ilikuwa na mazoezi mengi kila siku ya viungo na walimu wakubwa wa mazoezi walikuwa wajapan na huu ndio ukawa mwanzo wa Asha kujifunza ushupavu pasi na yeye kujua huku akiendelea na masomo ya mifupa ya binaadamu bila kusahau practical kibao walizifanya pale shule na baada ya miaka miwili ugeni wote ulimtoka Asha na akawa mzuri sana kwenye mazoezi ya viungo na kutokana na kuwa bado msichana aliweza kuwa mwepesi zaidi hali iliyomfurahisha sana Tyga aliyekuwa anaenda pale mara kwa mara.
Baada ya miaka mitano Asha alimaliza mafunzo pale na wakati huo tayari alikuwa na umri wa miaka kumi na tano ndipo alipohamishwa na kupelekwa kusini kabisa mwa India na Tyga na huko ndipo mchezo mzima ulipoanza mara baada ya kukutanishwa na mzee mmoja Ninja wa Kijapani ambae alijiekea makazi kusini mwa India na haikujulikana alifahamiana vipi na mr X zaidi ya maelekezo tu aliyopewa Tyga kuwa ampeleke Asha huko.
"Kwanini nalazimika kufanya hivi Uncle Tyga?"
"Kwa sababu ya usalama wako wa baadae Asha na msaada kwa bosi"
"Usalama kivipi Uncle na msaada gani tena kwa bosi?"
"Dunia sasa kuna watu wabaya sana Asha, si unakumbuka kilichotokea kwa mfadhili wako wa kwanza bwana Rajesh?"
"Ndio"
"sasa pale kama ungekuwa na taaluma nyengine zaidi ya kulia ungeweza kumsaidia na kumuokoa na ndivyo ilivyo kwa mfadhili wako huyu hadi ameamua kujificha kwa kuogopa watu wabaya wanaomfatilia kila siku wakitaka wamjue na wamuue"
"kwanini sasa Uncle?"
"kwa sababu watu wabaya sana na wana wivu hasa kwa watu wema wanaosaidia wengine."
"Daaah!! kama ni hivyo Uncle nami niko tayari kabisa kulipa fadhila na kumlinda bosi mr X kwa watu wote wabaya sitokubali nae wamuue kama Rajeesh"
"sasa itakubidi uvumilie na ukubali haya mafunzo na huyu babu tutakuwa pamoja siku zote, shika simu hii ongea na mama"
aliongea tena Tyga na kumtolea Asha simu na kumshangaza mno baada ya Tyga kuipiga na kuzungumza na mama mdogo wa Asha aliye Tanzania.
Hili ndio jambo kubwa ambalo Asha hakuwahi kujiuliza Tyga alianza vipi mawasiliano na mamaake lakini ni kwamba Tyga miaka yote alikuwa na mawasiliano na mama Asha na kumliwaza juu ya maendeleo ya mwanae japo kwa upande wa mama mdogo wa Asha alikuwa anajua anaongea na walewale wafadhili ambao walimchukua mwanae kwenda kumsomesha India.
*
MIAKA 10 BAADAE)
............
Ilikuwa ni ndani ya uwanja wa Ndege wa Mumbai walionekana wasafiri wakipanda ndani ya ndege ile kubwa iliyokuwa inafanya safari zake moja kwa moja mpaka bara la Afrika ktk nchi yaTunisia.
Ndani yake alionekana msichana mrembo sana Asha akiwa kakua sasa tofauti na alivyoingia kwa mara ya kwanza kwenye ule uwanja miaka kumi na tano iliyopita.
Safari hii hakuwa na mtu mwengine yeyote katika safari yake, hata yule mtu aliyewahi kumpa mdori miaka ile na kuja kugeuka ndugu yake wa pekee mara baada ya kumuokoa katika shambulizi lililopoteza nafsi za watu waliomfadhili na kumfikisha katika ile nchi, pia nae hakuwa nae kwenye ile ndege safari hii.
Akiwa anaendelea kujisomea kitabu huku akiwa haamini kama leo hii amekuwa Daktari Special wa mifupa na mishipa ya binaadam tena akiwa na vyeti vya uthibitisho kutoka kwenye chuo kikubwa sana India ambacho kiukweli hakuwahi kabisa kusomea hiko chuo japo ni kweli alikuwa na ujuzi mkubwa wa kutibu mifupa iliyovunjika na kuifanyia uparation kuiunga samba na mifumo ya mishipa yote ya mwili wa binaadam.
Hakujua mbinu gani zilitumika katika kumsaidia kupata kile cheti kilichoonesha alidumu kwenye kile chuo tangia angali na miaka kumi lakini alikumbuka maneno ya Tyga pindi alipokuwa anamuaga na kumpa jukumu la kuhakikisha usalama wa bosi wake Mr.X unakuwa mikononi mwake.
{{'''"Asha, kumbuka wewe ni Lady Ninja uliyevaa kivuli cha Dokta kwaajili ya ulinzi wa siri na usalama wa bosi wetu Mr X ambae kuna maadui ndani ya ngazi ya serikali wanamuinda kutokana na kuwafichua watu wabaya na kuwasaidia kwake wanyonge.
Nakukabidhi nafasi yangu niliyodumu kwa muda wa miaka ishirini sasa nikiwa kama mlinzi wa siri wa Mr X.
Sidhani kama tutaonana tenahuku ninapoenda ila nategemea utafanya vyema na kulipa fadhila kwa bosi mr.X ... Namba yako ya siri ni 9121 ktk code maalum utayokuwa unawasiliana nae mkuu"''}}
{"sawa Uncle Tyga, vipi nitaonana nae sasa maana natamani kumuona pia nimshukuru mbele yake."}
{{"Utamuona lakini kwanza inabidi umuoneshe kivitendo mission yoyote atayokupa ambayo itahatilisha maisha yake hakikisha unaimaliza haraka kabla haijawa tatizo, naamini ukiweza mission tatu atakuamini zaidi na utakutana nae ana kwa ana. Kuna kiasi kikubwa cha pesa ushawekewa kwenye account yako.
Mama tayari anaishi kwenye nyumba maalum aliyoijenga mkuu kwa kupitia jina lako ila hii siri ya huku ibaki kwenye kifua chako, kumbuka kile kiapo unatakiwa kila mtu akujue wewe ni Daktari bingwa wa mifupa lakini usikubali kuajiliwa popote. Safari njema My Lady Ninja"''}}
Aliyakumbuka maneno haya aliyokuwa amezungumza na Tyga mara ya mwisho pindi alipofuzu mafunzo ya udunguaji wa Kininja na kupewa jalibio la kustukiza mara baada ya siku moja kutelekezwa kimakusudi na Tyga na kumuacha katika balaa kwenye kundi la wahuni zaidi ya 25 lakini aliweza kuwadhibiti na kuwavunja vunja wote lakini mwishoni alipotaka kuondoka eneo lile ambalo lilikuwa nyuma ya bustani moja kulipokuwa na Bar na kambi ya siri ya kuuza madawa ndipo ghafra alitokea Ninja ambae alisumbuana nae sana kupambana nae ili kuokoa maisha yake mbali na kwamba yeye Asha hakuwa na nguo zake za kininja wala silaha na alishatoka kupambana na watu zaidi ya ishirini lakini aliweza kula sahani moja na yule Ninja hadi baada ya nusu saa alipoanza kuzidiwa mbinu Asha ndipo yule Ninja alimuacha Asha baada ya kuona ameanza kumzidi huku nae akiwa kakiona cha mtema kuni kutoka kwa yule binti na hapo alikubali na kumsogelea kisha alijifunua uso na kumshangaza Asha baada ya kugundua kuwa alikuwa anapambana na Uncle Tyga.
Ndipo Tyga alipomwambia maneno hayo ya kuagana nae kisha alipotea kwa kutumia uchawi wa Kininja mbele yake.
Alitabasamu Asha wakati akikumbuka yale kipindi hiko ndege ilikuwa tayari iko angani ikikata mawimbi na kuzidi kuliacha bara la Asia.
* * * * * *
Na kweli Asha mbali na kupokelewa kwa shangwe pindi alipounganisha ndege kutoka Tunisia mpaka Jijini Dar, Tanzania alipomkuta mamaake ambae ni Zena akiwa na wapambe kadhaa waliokwenda kumpa sapoti hususani sifa aliyorudi nayo ilimfurahisha sana wazili wa Afya wa Tanzania kwa kuona wataalam wanazidi kuongezeka nchini, lakini kitendo cha Asha kukataa ajira yoyote nchini na kutangaza kuwa atajiajili mwenyewe yaani awe anakodiwa kwa kazi maalum itayowashinda madaktari wa pale hususani maswala ya mifupa na mshipa basi atakuwa radhi kusaidia lakini si kuajiriwa kabisa na kuwa mfanya kazi wa kila siku.
Kauli hii kila mtu aliielewa anavyojua yeye lakini hakuna aliyejua nini kinaendelea nyuma ya pazia ya maisha ya Asha na kwa kutumia kode maalum aliyokuwa anawasiliana na mr X aliweza kupata maelekezo yote muhimu na siri ya nyumba ile hususani chumba chake ambacho kumbe kilikuwa na sehemu maalum iliyotengenezwa kwa mfumo wa lifti na chini yake ndipo kulikuwa na chumba cha mawasiliano na maelekezo juu yake nini afanye kuhusu usalama wa bosi wake ambae alimpenda na kumuhusudu kama muokozi wake mbali ya kuwa hajawahi kumuona katika miaka yote toka afahamu uwepo wake.
* * * * * *
Ikiwa ni miezi mitatu imepita tangia arejee nyumbani Tanzania huku akiendelea na mawasiliano ya siri na bosi wake ambae siku zote hakuwahi kufikiria sana wala kuhoji sababu za kujificha kwake ama kutopenda kuzungumza nae ana kwa ana.
Kila akikumbuka wema aliofanyiwa na Uncle Tyga kule india hadi alivyomuokoa na kumsomesha hata kumuunganisha na kuaminiwa na bosi wao kuchukua nafasi yake ndivyo alivyozidi kumpenda mr.X na mara zote usiku aliingia kwenye chumba chake cha siri na kuwasiliana nae na ndipo siku hiyo alipokutana na ujumbe wa picha ya kijana askali magereza pamoja na maelezo kiurefu yaliyosema.....
^^^
^^Huyo ni Shaaban Mwinchande, Kamishna wa polisi na mkuu wa gereza la Nyato lile la wafungwa wenye makosa makubwa nchini.
Babaake ni adui wangu mkubwa na sasa anamtumia mwanae ili aweze kujua nilipo kwaajili ya kuniangamiza^^
^^Picha hii ya chini huyu ni mzee mganga wa muda mrefu anaitwa Mnyungunyungu, aliwahi kuwa rafiki angu miaka ya nyuma lakini baadae akawa msariti kwa tamaa na kujiunga na mzee Mwinchande babaake huyo Kamishna Shebby anayetaka kunijua kwa udi na uvumba na kuniua^^
^^Sasa My Lady Ninja location ya tukio ni Mkuyuni Morogoro
huko utakutana na mzee huyu unayemuona hapa chini... Anaitwa Aly77 namba zake ni hizo yeyey ndie anayechunga usalama wangu pale na ndie alietuma taarifa za huyo kijana aliyeenda kunitafuta kwa mzee Mnyungunyungu ambae ni kweli kuna baadhi ya taarifa zangu muhimu ila Aly77 ameshamdhibiti mzee Mnyungunyungu na huyo Kamishna kaondoka huko, lakini najua lazima atarudi tena kutaka habari zangu toka kwa mtoto wa mzee Mnyungunyungu ambae ni huyu umuonae sasa kwenye picha, yeye ndie mganga wa pale anayejua fununu zangu na ni hatari kwa maisha yangu kama atabaki hai na kuzitoa siri kwa maadui zangu. ^^
Kazi kwako Lady Ninja okoa maisha yangu.^^
^^^
Baada ya kuupata ujumbe ule na kuzirusha zile picha kwenye Memory yake, Asha aliandaa mavazi yake ya kazi na kuyaweka kwenye begi dogo kisha usiku uleule aliandika ujumbe mfupi na kuuacha mezani akimuarifu mamaake pindi atapoamka kuwa amepata dharura kisha alitoka na kuingia kwenye gari yake ndogo ya kifahari taratibu safari ya Morogoro Mkuyuni ilianza.
Kwa kutumia code alizopewa aliweza kuwasiliana na huyo mzee aliyeitwa Aly77 ambae ndie aliyemuekea sumu maalum iliyokuwa inamtafuna mganga Mnyungunyungu taratibu hadi kufikia kuwa hoi bin taaban.
Miaka yote alijichomeka pale kijijini yule mzee ambae alionekana mcha Mungu kutokana na tabia yake ya kupenda kuswali na kuvaa kanzu na kibaraghashia kumbe nyuma ya pazia hakuwa hivyo alikuwa anafanya kazi ya mtu ambae alikuwa anamsaidia kipato na kuiwezesha familia yake pia mzee Aly77 ndie alikuwa baba mzazi wa Tyga na alijitolea kufanya kila kitu kwa mr X mara baada ya kusaidiwa miaka iliyopita pindi mwanae alipopata ugonjwa m baya uliotakiwa asafirishwe India nae kwa kukosa uwezo alijikuta anapita huku na huko kuomba msaada ndipo alipokutana na msaada wa mr X kupitia mwana mama Mrembo ambae alisafiri na Tyga hadi India pamoja na babaake na huko waliishi mwaka mzima mara baada ya oparation na siku zote yule mama aliwasisitiza kuwa msaada ule walipatiwa na Mr X na hiko kikawa chanzo cha yule mzee kumuhusudu mr X hasa baada ya kuambiwa kuwa mwanae ambae ni Tyga atasaidiwa zaidi na mr X kusomeshwa nchini Japan hadi atimize malengo yake nae mzee Aly alipewa kisa kizima kama alivyopewa Asha na Tyga juu ya kujificha mr X lakini yote hayo mzee Aly hakujali wala hakuwa na haraka ya kumjua huyo mr X zaidi ya kuwasiliana nae kwa simu zenye code maalum, na kupewa maelekezo muhimu huku kila mwisho wa wiki pesa iliingizwa kwenye account yake.......
Itaendelea. ...