Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Usile Nyama Mwisho

Ni siku nzuri leo, ukiwa huamini sio tatizo langu maana kuamini ni moja na kukubali ni jambo jingine. Nilicho na uhakika nacho ni kuwa wewe kapuku mheshimika uko hapa na unalifanya jukwaa letu kuwa ni mahali pazuri pa kukutana na kubadilishana mawili matatu. uzuri kila mmoja kula kwake kwa hiyo hata mwenye njaa inabaki kuwa ni ishu yake binafsi Ile kapuku hotel, it's a virtual hotel.

Furahiday leo, ni siku njema kabisa na ni mwendo kula na kunywa vizuri, usishangae pilau hupikwa katika majumba mengi. na kwa tabia ya ajabu kabisa na inayovutia ni kitendo cha wakati wa kula, nyama huliwa mwisho. yaani unatunza nyama hadi unapokaribia kumaliza kupiga mpunga ndo unaanza kula nyama. Ha hahahaha, sijui nimekumbuka nini kuhusu hili.

Leo tuwapongeze Mndali ndanyelakakomu na demi kwa kutuchangamsha jukwaani kwa penseli na kuchunga mbuzi huku mmoja akikataa kuwa buzi, you guys are awesome. Yote kwa yote sijawaona Mkushi wa kusi , BlessedHope na wadau wengine, fikisha salamu kwao kuwa wanamisika hapa, ila kwa kuwa wewe upo hakijaharibika kitu.

Muziki sasa, hivi unajua kuna wanamuziki wa Kiafrica ambao huhitaji nguvu sana kuwaongelea, yaani kazi zao zinawatambulisha, ukiwasikia tu unajua huu mziki wa kipekee ni wa sehemu fulani. Wasikilize Mahotella Queens, utajua hawa ni wa SA, msikize Ndour Youso, na zaidi msikize Angelique Kidjo.

Mshindi huyu wa tuzo za Grammy ni mBenin anayefanya muziki wake kiuasili akiuboresha kukuvutia, ni mwanaharakati wa kimataifa na zaidi ni mwanadada anayeamini kuwa urembo anao kila mwanamke na wala hahitaji kujiweka utupu kila wakati. Kwa hisani ya Jimena muite Jimena Jimenes (sounds Spanish) basi burudika. Kidjo kishaimba na kina Keys, Bono, Ziggy na wengi wa kimataifa na kufanya cover ya nyimbo za Bob Marley, Makeba

Hapa akifanya cover ya Malaika

uwe na wikend njema Kapuku mwenzangu

Asante mpendwa
 
ZABURI 91

1.Aketiye mahali pa siri pake,Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2.NitasemaBWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini

3.Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo.

4.Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio,Uaminifu wake ni ngao na kigao,

5.Hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana,

6.Wala tauni ipitayo gizani,wala uele uharibuo adhuhuri.

Muwe na usiku mwema
 
Huu ujumbe ni kwa wale wanasoma comments za Kapuku forum kimya kimya.

Karibuni sana kapuku..sie hatuna ubaguzi huku..

Karibuni sana, muache uoga wa kusoma tuu na kupita..

Hata wewe unayesoma kwenye browser , log in ...tia comment ! Sema hata hi..

Hii na kwa Manga ML na wengine woooooooooote mnaosoma posts za Kapuku forum kimya kimya

Cc

faiza Foxy
Mamndenyi
 
Aisee Sakayo ni asset.

Yaaani huyo mtoto ni mali,

Hicho kichwa chake ni kina akili hataree...

Sometimes huwa napiga Goti kwa Mungu na kusema Aksante Bwana kwa kunipa Sakayo.

She thinks and analyse things to an extra mile ...she know how to put things on track.
Kama ndiyo hivyo basi uache mapepe, maana ulijichanganya kidogo babu A akupige bao.
 
ZABURI 91

1.Aketiye mahali pa siri pake,Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2.NitasemaBWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini

3.Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo.

4.Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio,Uaminifu wake ni ngao na kigao,

5.Hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana,

6.Wala tauni ipitayo gizani,wala uele uharibuo adhuhuri.

Muwe na usiku mwema
Asante mdogo wangu wa dar
 
Huu ujumbe ni kwa wale wanasoma comments za Kapuku forum kimya kimya.

Karibuni sana kapuku..sie hatuna ubaguzi huku..

Karibuni sana, muache uoga wa kusoma tuu na kupita..

Hata wewe unayesoma kwenye browser , log in ...tia comment ! Sema hata hi..

Hii na kwa Manga ML na wengine woooooooooote mnaosoma posts za Kapuku forum kimya kimya

Cc

faiza Foxy
Mamndenyi
Wamekuelewa
 
Ninarudi tena yaani ninakuja kushinda anavyorudi sister P, ujio wangu ni kuwaunga mkono na mguu bila kupewa upaja na wote wanaenda kwenye maombi ya Ijumaa, haijarishi wanafanyia maombi wapi, iwe bar au kanisani au msikitini ilmradi wanatimiza ibaada zao wote tuwaunge mkono.

Ombi la Shunie aunt yangu huyu na Sakayo (huyu kama sio mhenga basi mimi nitajitoa kwenye uhenga- yaani anaijua hata ile nyimbo ya Paka kulia usiku)😀

Christina Shusho wa kwanza, huyu uzao wangu ningekuwa mwanakwaya kwenye kwaya yake

Na huyu ni mwinjilist Munishi, naamini nimesikiliza album zake karibu zote.

Paka kulia usiiiiku ndio kawaida wao hutimua mbiooo eti wamelogwa

enzi hizo bado sijawa muhenga

Big up mpendwa wangu na sakayo mmenikumbusha mbalii
 
Huu ujumbe ni kwa wale wanasoma comments za Kapuku forum kimya kimya.

Karibuni sana kapuku..sie hatuna ubaguzi huku..

Karibuni sana, muache uoga wa kusoma tuu na kupita..

Hata wewe unayesoma kwenye browser , log in ...tia comment ! Sema hata hi..

Hii na kwa Manga ML na wengine woooooooooote mnaosoma posts za Kapuku forum kimya kimya

Cc

faiza Foxy
Mamndenyi
Mkuu mimi hapa ni nyumbani ni mwanzo wa uzi huu utaona hilo sema si mshiriki wa kila siku imebidi niwe mtazamaji tu

Hivi Mosolin anapatikana?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom