Muziki: Usile Nyama Mwisho
Ni siku nzuri leo, ukiwa huamini sio tatizo langu maana kuamini ni moja na kukubali ni jambo jingine. Nilicho na uhakika nacho ni kuwa wewe kapuku mheshimika uko hapa na unalifanya jukwaa letu kuwa ni mahali pazuri pa kukutana na kubadilishana mawili matatu. uzuri kila mmoja kula kwake kwa hiyo hata mwenye njaa inabaki kuwa ni ishu yake binafsi Ile kapuku hotel, it's a virtual hotel.
Furahiday leo, ni siku njema kabisa na ni mwendo kula na kunywa vizuri, usishangae pilau hupikwa katika majumba mengi. na kwa tabia ya ajabu kabisa na inayovutia ni kitendo cha wakati wa kula, nyama huliwa mwisho. yaani unatunza nyama hadi unapokaribia kumaliza kupiga mpunga ndo unaanza kula nyama. Ha hahahaha, sijui nimekumbuka nini kuhusu hili.
Leo tuwapongeze
Mndali ndanyelakakomu na
demi kwa kutuchangamsha jukwaani kwa penseli na kuchunga mbuzi huku mmoja akikataa kuwa buzi, you guys are awesome. Yote kwa yote sijawaona
Mkushi wa kusi ,
BlessedHope na wadau wengine, fikisha salamu kwao kuwa wanamisika hapa, ila kwa kuwa wewe upo hakijaharibika kitu.
Muziki sasa, hivi unajua kuna wanamuziki wa Kiafrica ambao huhitaji nguvu sana kuwaongelea, yaani kazi zao zinawatambulisha, ukiwasikia tu unajua huu mziki wa kipekee ni wa sehemu fulani. Wasikilize Mahotella Queens, utajua hawa ni wa SA, msikize Ndour Youso, na zaidi msikize Angelique Kidjo.
Mshindi huyu wa tuzo za Grammy ni mBenin anayefanya muziki wake kiuasili akiuboresha kukuvutia, ni mwanaharakati wa kimataifa na zaidi ni mwanadada anayeamini kuwa urembo anao kila mwanamke na wala hahitaji kujiweka utupu kila wakati. Kwa hisani ya
Jimena muite Jimena Jimenes (sounds Spanish) basi burudika. Kidjo kishaimba na kina Keys, Bono, Ziggy na wengi wa kimataifa na kufanya cover ya nyimbo za Bob Marley, Makeba
Hapa akifanya cover ya Malaika
uwe na wikend njema Kapuku mwenzangu