Makapuku Forum

Makapuku Forum

5125be31c700e5e31010dc0596a1917a.jpg
 
YOSHUA 1

8.Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo;maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapositawi sana

9.Je,si mimi niliyekuamuru?uwe hodari na moyo wa ushujaa,usiogope wala usifadhaike,kwa kuwa BWANA yu pamoja nawe kila uendako

BABA katika jina Takatifu la Yesu ,asante kutuamsha salama,tunaomba rehema yako tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea,utuepushe na majaribu tulinde,tuongoze tuweze kutenda mema siku ya leo na siku zote za maisha yetu,katika hii safari ya maisha yapo mengi tunayoyapitia BABA wewe unamajibu ya kila changamoto,tusaidie tuhesabu baraka zote ulizotujalia na kutusaidia kuwa na tumaini kwako tu kwamba hata changamoto ni sehemu ya baraka maana zinazidi kutusogeza karibu na wewe.

Tusaidie kulisoma na kuliishi neno lako takatifu liwe taa ya miguu yetu popote tuingozwe na neno lako.

Walinde watoto wetu walioko mashuleni na majumbani,waimarishe katika mausha ya kiroho wawe na hofu ya MUNGU ,waepushe na vishawishi,wape hekima na busara katika kuchagua marafiki ...

Baba Bariki kazi za mikono yetu zikapate kibali mbele zako na daima ziwe kazi za kukutukuza wewe.

Bariki vipato vyetu viweze kuwa vya manufaa katika maisha yetu na kila tupatacho katika kazi zetu kiwe na manufaa kwetu na kujenga mwili wa Kristo,pesa na mali tunazopata zionekane tuweze kufaidi mapato ya kazi za mikono yetu.

Asante BABA Maana utafanya sawa na mapenzi yako

Tunaomba katika jina la Yesu Amen.

NAWATAKIA SIKU NJEMA MUNGU AWABARIKI

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Atubariki sote
 
😎 Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambae yuko London kwa ajili ya matibabu, amefanya mkutano wake wa kwanza na anaekaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili sasa.

😎 Mashindano ya riadha ya dunia ya IAAF kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 18 yanaanza hii leo jiji Nairobi Kenya

😎 Nchini Rwanda kuna mradi wa kutengeneza sodo zinazopatikana kwa bei chee ambazo hutengenezwa kwa nyuzi zitokanazo na mabaki ya migomba.

😎 Malaria bado ni changamoto katika nchi nyingi barani Afrika, huko nchini Tanzania kwa mujibu wa wizara ya Afya takribani watu milioni 18 huugua ugonjwa wa malaria kila mwaka. Katika kupambana na ugonjwa huo shirika la Afya la ifakara wamebuni mbinu mpya ikiwemo utengenezaji wa viatu vyenye kinga ya mbu hususani wakati wa mchana.

😎 kuna taarifa ya uwepo wa kampuni moja inayotengeneza viatu vya kwanza vya riadha kubuniwa nchini Kenya..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom