Makapuku Forum

Makapuku Forum

YOSHUA 1

8.Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo;maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapositawi sana

9.Je,si mimi niliyekuamuru?uwe hodari na moyo wa ushujaa,usiogope wala usifadhaike,kwa kuwa BWANA yu pamoja nawe kila uendako

BABA katika jina Takatifu la Yesu ,asante kutuamsha salama,tunaomba rehema yako tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea,utuepushe na majaribu tulinde,tuongoze tuweze kutenda mema siku ya leo na siku zote za maisha yetu,katika hii safari ya maisha yapo mengi tunayoyapitia BABA wewe unamajibu ya kila changamoto,tusaidie tuhesabu baraka zote ulizotujalia na kutusaidia kuwa na tumaini kwako tu kwamba hata changamoto ni sehemu ya baraka maana zinazidi kutusogeza karibu na wewe.

Tusaidie kulisoma na kuliishi neno lako takatifu liwe taa ya miguu yetu popote tuingozwe na neno lako.

Walinde watoto wetu walioko mashuleni na majumbani,waimarishe katika mausha ya kiroho wawe na hofu ya MUNGU ,waepushe na vishawishi,wape hekima na busara katika kuchagua marafiki ...

Baba Bariki kazi za mikono yetu zikapate kibali mbele zako na daima ziwe kazi za kukutukuza wewe.

Bariki vipato vyetu viweze kuwa vya manufaa katika maisha yetu na kila tupatacho katika kazi zetu kiwe na manufaa kwetu na kujenga mwili wa Kristo,pesa na mali tunazopata zionekane tuweze kufaidi mapato ya kazi za mikono yetu.

Asante BABA Maana utafanya sawa na mapenzi yako

Tunaomba katika jina la Yesu Amen.

NAWATAKIA SIKU NJEMA MUNGU AWABARIKI

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app


Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
 
IMG-20170712-WA0031.jpg
 
NUKUU YA LEO

A friend is someone who gives you total freedom to be yourself

Rafiki ni mtu ambaye anakupa uhuru kamili wa kuishi kama wewe


Haya maneno yaliwakusemwa na mwanamshairi wa kimarekani James Douglas ama jim morrison .

Jim morrison alizaliwa Dec. 8 1943 na kufariki July 3 1943.

Jim morrison alifariki nchini ufaransa kwa kile kinachosemekana kuwa ni Shambulio la Moyo.

Jim alikutwa akiwa amefariki bafuni kwake.

Be a friend! Live your life! Enjoy the short moment you have..

Life is too short..!

ef6f959eb0ab646f0fed1797a68b7aa7.jpg

9bc1d169e29b9441fa340bbacbfbc142.jpg
Asante T wa dada kwa nukuu

Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom