Makapuku Forum

Makapuku Forum

Niunge mkono na kiwiliwili

022ba017e48838552ba563e5dbbe1707.gif
na mama yangu je
 
YOSHUA 1

8.Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo;maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapositawi sana

9.Je,si mimi niliyekuamuru?uwe hodari na moyo wa ushujaa,usiogope wala usifadhaike,kwa kuwa BWANA yu pamoja nawe kila uendako

BABA katika jina Takatifu la Yesu ,asante kutuamsha salama,tunaomba rehema yako tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea,utuepushe na majaribu tulinde,tuongoze tuweze kutenda mema siku ya leo na siku zote za maisha yetu,katika hii safari ya maisha yapo mengi tunayoyapitia BABA wewe unamajibu ya kila changamoto,tusaidie tuhesabu baraka zote ulizotujalia na kutusaidia kuwa na tumaini kwako tu kwamba hata changamoto ni sehemu ya baraka maana zinazidi kutusogeza karibu na wewe.

Tusaidie kulisoma na kuliishi neno lako takatifu liwe taa ya miguu yetu popote tuingozwe na neno lako.

Walinde watoto wetu walioko mashuleni na majumbani,waimarishe katika mausha ya kiroho wawe na hofu ya MUNGU ,waepushe na vishawishi,wape hekima na busara katika kuchagua marafiki ...

Baba Bariki kazi za mikono yetu zikapate kibali mbele zako na daima ziwe kazi za kukutukuza wewe.

Bariki vipato vyetu viweze kuwa vya manufaa katika maisha yetu na kila tupatacho katika kazi zetu kiwe na manufaa kwetu na kujenga mwili wa Kristo,pesa na mali tunazopata zionekane tuweze kufaidi mapato ya kazi za mikono yetu.

Asante BABA Maana utafanya sawa na mapenzi yako

Tunaomba katika jina la Yesu Amen.

NAWATAKIA SIKU NJEMA MUNGU AWABARIKI

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
YOSHUA 1

8.Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo;maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapositawi sana

9.Je,si mimi niliyekuamuru?uwe hodari na moyo wa ushujaa,usiogope wala usifadhaike,kwa kuwa BWANA yu pamoja nawe kila uendako

BABA katika jina Takatifu la Yesu ,asante kutuamsha salama,tunaomba rehema yako tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea,utuepushe na majaribu tulinde,tuongoze tuweze kutenda mema siku ya leo na siku zote za maisha yetu,katika hii safari ya maisha yapo mengi tunayoyapitia BABA wewe unamajibu ya kila changamoto,tusaidie tuhesabu baraka zote ulizotujalia na kutusaidia kuwa na tumaini kwako tu kwamba hata changamoto ni sehemu ya baraka maana zinazidi kutusogeza karibu na wewe.

Tusaidie kulisoma na kuliishi neno lako takatifu liwe taa ya miguu yetu popote tuingozwe na neno lako.

Walinde watoto wetu walioko mashuleni na majumbani,waimarishe katika mausha ya kiroho wawe na hofu ya MUNGU ,waepushe na vishawishi,wape hekima na busara katika kuchagua marafiki ...

Baba Bariki kazi za mikono yetu zikapate kibali mbele zako na daima ziwe kazi za kukutukuza wewe.

Bariki vipato vyetu viweze kuwa vya manufaa katika maisha yetu na kila tupatacho katika kazi zetu kiwe na manufaa kwetu na kujenga mwili wa Kristo,pesa na mali tunazopata zionekane tuweze kufaidi mapato ya kazi za mikono yetu.

Asante BABA Maana utafanya sawa na mapenzi yako

Tunaomba katika jina la Yesu Amen.

NAWATAKIA SIKU NJEMA MUNGU AWABARIKI

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Amina mama
 
Sehemu ya 27


"Huu.. missss..ta.X ni... nii..aaaghhhrrr...niii....." Alihangaika kusema mzee yule na kabla hajamalizia kutamka juu ya huyo mr. X mara kichwa chake kilifumuliwa vibaya huku ubongo ukitawanyika sambamba na damu. Ilikuwa ni risasi ya kichwa iliyommaliza mzee yule ikitua bila kutoa mlio wowote mbele ya macho ya Kamishna Shebby, Ocs John na Sajent Kimaro.
"Ooooooh! hatariiiiiii kuna mdunguaajiiiiiiiiii!." huku akijichopa pembeni kwa sambasoti alitoa ukelele Shebby baada ya kugundua wapo katikati ya mtego wa mdunguaji hatari.
* * * *
Wakati Mkuyuni hali ikizidi kuwa tirigivyogo upande wa pili makao makuu ya gereza mzee Mwinchande alighadhibika kuona simu ya mwanae imekatwa tena na haikupatikana hata aliporudia kupiga.
"Kijana hebu naomba nisaidie aitwe huyo mfungwa mwenyewe nimuone anambie nini alichomuhadaa mwanangu hadi afikie huko kote." alitoa hitaji mzee Mwinchande bila kupingwa ndipo yule askari alipoamua kumpigia simu ya mkononi coplo aliyesimamia jela za watu maalum.
"Enhee njoo na yule mfungwa namba 8707" Baada ya kutoa agizo haukupita muda Hussein bubu alifikishwa.
"Huyu hapa mkuu." Aliongea yule coplo aliyemleta huku akiwa ameongozana na askali wengine wawili waliomshika Hussein kipindi wanamkokota kwenda nae mahala pale.
"oke sawa, mnaweza kusubiri nje." Alitoa amri yule msaidizi wa Shebby na hatimaye ndani wakabaki watatu. Yaani mkuu msaidizi, mzee Mwinchande na Hussein babu Bubu.
"Mtu mwenyewe ndio huyu?" aliuliza mzee Mwinchande huku akimtazama kwa mshangao Hussein bubu.
"Ndiye huyo mzee."
"sawa unaitwa nani bwana?" Alimsogela yule mfungwa na kumuuliza huku akimuagalia kwa jicho la kumshusha.
"We bwanaa wee si nakuuliza miye!?" Aliuliza tena mzee Mwinchande baada ya Hussein kubaki kimya akiwatazama tu pasipo kusema. Aliuvaa ububu wake kama kawaida na ghadhabu kutuama moyoni mwake. Mbali ya kuwa mfungwa lakini Hussein hakupenda dharau wala hakuwa mwenye hofu.
"Mzee wangu huyu muda mwengine anakuwaga sanamu hivyo hivyo sasa ngoja tum-boost. Coplo Yonaaa..! Njoo afande!" Aliongea na kuita yule msaidizi wa Shebby. Muda uleule aliingia yule coplo ambaye alitumika kumleta Hussein pale. Alipopewa amri ya kumuadhibu Hussein ili azungumze, papo hapo alichomoa mkanda na kuanza kumtandika ovyoovyo. Hussein hakuugulia wala kujikuna zaidi ya kuganda kama jiwe pindi mikanda ikitalii mwilini mwake.
"Hebu basi inatosha!" Mzee Mwinchande alijikuta akizuia mwenyewe.
"Haya mzee mwenzangu mi nakwambia kwa ustaarabu lakini wewe unataka uambiwe kama ulivyozoeshwa. Sasa narudia tena kukuuliza kabla sijaendelea kukujuza kwanini nakuuliza hata umeletwa hapa. Unaitwa nani?" Alirudia swali lake mzee Mwinchande lakini Hussein alikuwa kiburi sana hasa anapogundua mtu anayeongea naye anamletea dharau. Vitasa viliendelea bila Hussein kujibu chochote. Mwishowe mzee Mwinchnde alijikuta akifoka.
"Yaani mwanangu anajitolea kusaidia mabubu yasiyo na fadhila wala mawazo kama hili? Duuh! sasa Shebby kasema sema nae vipi mbona sielewiii hapa?" Pindi alipolalama mzee Mwinchande na kumtaja Shebby ndipo hapo ubongo wa Hussein ulivubuka kwa kujua kumbe yule mzee ni baba wa kamishna yule aliyejitolea kumsaidia.
"Kumbe wewe ndiye baba wa Kamishna Shebby?" Alijikuta akiongea kwa sauti yenye mikwaruzo Hussein.
"Jamani msinipige kama huyu bwana ni baba wa Kamishna Shebby tafadhali niacheni niongee naye." Alisisitiza zaidi na hapo ndipo walipomuacha kumtandika mikanda na kumsimamisha aongee.
"Enhee! sema umemuhadaa na hadithi gani mwanangu mpaka haeleweki mambo yake."
"Lakini hapo sielewi kaka kwanini unasema nimemuhadaa."
"oke, utaelewa tu." aliongea mzee Mwinchande huku akisukuma kiti chake na kukaa vizuri.
"Sikia bwana bubu, kwanza samahani kwa kukufokea mzee mwenzangu ila unajua mtoto anauma sana. Sasa mi nilitaka kujua ni hadithi gani inayokuhusu uliyomsimulia mwanangu hadi kupelekea kuwa bussy kiasi hiki? Naomba unijibu kweli na unihadithie walau kiufupi kwa sababu mimi ni baba mzazi wa Shaaban pia ni mkuu mstaafu wa jeshi la polisi nchini kwa hiyo usiwe na hofu wala woga wa kunihadithia ukweli ulichomwambia mwanangu tujue nini cha kufanya maana mpaka sasa nahisi mwanangu kajibebesha mzigo asioujua wapi pa kuutua." Aliongea mzee Mwinchande na ndipo hapo Hussein alipofikiria na kukata shauri kuamua kuzungumza ukweli kile ambacho alikizungumza kwa Kamishna Shebby.
"Uuuuuppphhhhh!! yaani hadithi yako imenishangaza sana na kuniumiza pia pole sana bwana." Alihema mzee Mwinchande na kuonesha kuguswa mno na mkasa wa Hussein.
"Sasa Hussein hivi we humkumbuki hata kidogo huyo mr. X walau tetesi zake alikuwa nani au yukojeyukojeee..?"
"Kiukweli kaka sio kwamba sikumbuki bali simjui kabisa na sijawahi kumuona wala kupata tetesi zake hapo kabla zaidi ya barua ile ya utata."
"Duuh! sasa kama muhusika uliyekuwepo enzi hizo humjui?! Je, mwanangu atawezaje kumjua? Atapitia njia zipi wakati wewe mwenyewe huna hata wazo? Huoni kama ni kazi ya ajabu isiyokuwa na kichwa wala miguu. Mi nina wasiwasi na kazi aliyojitumbukiza mwanangu inaweza kumletea hatari kwa huyo mr. X kwa jinsi ulivyonisimulia kama ndio kweli na yuko hai hadi sasa..! Naamini anaweza hata kumuua kabisa mwanangu tena itakuwa rahisi kwa kuwa yeye hamjui..! looh!" Aliongea kwa unyonge mzee Mwinchande na kubaki anamtazama mkuu msaidizi na Hussein ambao wote walibaki wanakuna vichwa wakilifikiria swala lile. Hapo ndipo kwa mara nyengine mzee Mwinchande aliamua kupiga namba ya Shebby lakini bado majibu yalirudi yaleyale kuwa haipatikani.
Safari hii sasa alianza kuingiwa na mashaka juu ya huko alipo Shebby. Muda ulishatokomea na giza lilianza kubisha hodi angani.
*******
Sekunde zilezile hali ilizidi kuwa si hali pale Mkuyuni. Shebby aliporuka huku akijiandaa kujibu mashambulizi ya risasi kwa mdunguaji ambaye hakuna aliyejua amejificha upande upi, mara ukelel mwengine mkali wa maumivu ulisikika. Alikuwa ni Sajent Kimaro ambaye alitandikwa risasi ya kifua eneo lile la moyo.
"KIMAROOOOOO!" Alipiga ukelele huku akiruka tena na kujitupa upande wa pili alipokuwa Kimaro ambaye tayari alikuwa njia panda ya mauti. Askari walianza kupiga risasi ovyo juu ya miti kwa hofu na kujihami ingawa hawakujua ni mti gani aliojibanza huyo mdunguaji. Jua lilikuwa linakuchwa na kwa jinsi miti ilivyokuwa mikubwa na pori lilivyoshona ndivyo kiza kilizidi kuongezeka na kuwafanya askari wapatwe hofu zaidi. Chozi lilimtoka Shebby alipomshuhudia Kimaro akikata roho mikononi mwake baada ya kufika na kutaka kumnyanyua amtoe eneo lile. Maumivu yalimkaba kifua zaidi na kudata.
"Kimaaarooo! usife tafadhaliii aaaaah! Kimaro wewe ni askari shjaa. Hapana Kimarooo usiendeeeee!" Alilia na kulalama Shebby na mara kelele za maumivu zilizidi kutawanyika kila pande kwa zamu. Askari mmoja mmoja sasa alidondoshwa na mdunguaji hata kupelekea wengine waanze kukimbia kuokoa nafsi zao lakini hawakuponyeka. Mdunguaji hakuwa na papala wala mchecheto. Mahala alipojificha alitulia mno mbali ya risasi nyingi zilizopigwa na askari kuelekea kwenye miti iliyowazunguka. Shebby alizidi changanyikiwa alipowaona vijana wadogo wa polisi wakipoteza roho zao huku wakizililia kwa maumivu. Alijitahidi kuwalinda wenzake na kuilinda nafsi yake Shebby kwa kuruka huku na huko huku akipiga risasi mitini alikohisi huenda muuaji amejibanza. Lakini hakufua dafu wala kuambua kitu zaidi ya kupoteza risasi na kuwapoteza wenzake.
"Oooooh!! Sheeebbb..Sssheeebbby Unatuuuuuaaaaa." Iliisikia sauti ya maumivu ya Ocs John iliyomfanya kufumba macho Kamishna Shebby huku machozi yakimtoka kwa uchungu alipomuona akitandikwa risasi ya kifua upande uleule wa moyo kama ilivyokuwa kwa Sajent Kimaro. Alijilaumu na kujitukana kwa kuwaponza wote waliokuwa wanapoteza maisha muda ule. Alijiona yeye ndiye mkosaji wa roho zote zilizokuwa zinanyofolewa na mdunguaji yule. Laiti isingekuwa imani yake ya kumsaidia Hussein bubu na kutaka kumjua Mr. X basi yale yanayotokea muda ule huenda yangekuwa njozi. Lakini siku zote neno 'Ningejua' huja baada ya kitendo. Alijibanza chini ya mti mmoja huku akihema na kubaini kuwa yuko peke yake.
"Kwanini najificha? Ina maana nami naogopa Kufa? Hapana! damu za rafiki zangu lazima nizilipe kwa damu yangu." Sauti ilimuamuru moyoni baada ya kuona ukimya umekaa kitako kwa muda.
"Jitokezeeeee Mwanaharaaaamuuu Mkubwaaaaaa weeeee kama mwanaumeeee jitokezeeee Tupambaneeee wenyeeweee.." Alijitokeza na kuipaza sauti kamishna Shebby huku akiwa kasimama sehemu ya wazi. Nguo zake zote zikiwa zimetapakaa damu za baadhi ya wenzake waliouawa akiwemo Kimaro aliyekufa mbele yake na yule mzee wa kibaraghashia.
"Aaaaaaaaghhhh Jitokeeezeeeee Ku**aaa weeeee kama Mwanaumeee kweliiiiiiii.. Mbona unajifichaaa?" Aliongea kwa nguvu Kamishna Shebby huku akiwa kachanganyikiwa na kuitupa chini pisto yake na kujipiga piga kifua kwa hasira huku akiunguruma na kuhema kama duma mzee aliyetoka kukimbiza swala jangwani.
"ha ha ha ha ha ha haaaa.."
Kilisikika kicheko kikitokea maeneo ya nyuma hatua chache na aliposimama Kamishna Shebby. Aligeuka haraka kujihami huku akishangaa kusikia kicheko kile cha sauti ya kike. Alipotazama alichokuwa anakiona Kamishna Shebby hakuamini macho yake mara baada ya kumuona mtu akishuka tokea juu ya mti mmoja mkubwa sana kwa kutumia kamba maalum aliyojifunga kiunoni huku akiwa kavaa 'full Combat Ninja' (Mavazi kamili ya Kininja). Machoni alitinga miwani maalum iliyojulikana kitaama kama 'Night vission' Ambayo iliweza kuadilisha hali ya hewa na kuonea vyema kuna kiza ama moshi. Mikononi mwake akiwa kakamatia bunduki kubwa ya udunguaji iliyomuelekea Shebby na kumuweka chini ya ulinzi Kamishna kipindi akishuka taratiiibu.
Shebby haraka alitaka afanye ujanja wa kuiwahi ile bastora aliyoitupia pembeni lakini ile anaruka tu yule ninja aliidungua ile pisto na kuipeleka mbali zaidi na Kamishna Shebby kuangukia patupu. Hakuchoka wala hakujali Shebby alitaka kumrukia hivyo hivyo yule Ninja aliyemtia hasira zaidi baada ya kubaini alikuwa ni mwanamke lakini ile ananyanyuka tu alipigwa risasi ya goti na kuubong'onyoa mguu wake na kuanguka chini kama aliyepigwa mweleka. Ninja mdunguaji alifika chini kabisa na kuifatua kamba aliyokuwa ameshuka nayo. Alipiga hatua na kumsogelea Shebby aliyekuwa amelala chali pale chini akijaribu kusotea mgongo huku mguu wake ukizidi vuja damu.
"Kamishna Shebby... ha ha ha haaa wewe ni kijana mzuri sana mwenye bahati katika maisha yako. Ila kinachokuponza ni kutaka kujifanya bingwa wa kuutafuta ukweli ulioshindwa kuonekana kwa zaidi ya umri wako pasi na kujiuliza je, hawakuwepo watu kama wewe waliotaka kuujua huo ukweli? Na kama walikuwepo kwanini waliacha kuutafuta? Nadhani ulitakiwa kwanza utafute majibu ya maswali hayo mawili ndipo uchague uutafute ama nawe uache kama walivyoacha wenzako waliopita.... Lakini wewe umejitia shujaa umekurupuka na kuwaponza wenzako wafe bila hatia.
Ona sasa maisha yako yalipofikia. Nani ataweza kukutetea hapa hahahahahaaaaaa Nilitakiwa nikubebeshe kesi hii ya kuwaua wenzako wote kisha na wewe kujipiga risasi ya mguu ili kupoteza ushahidi kwa maslahi ambayo unayajua mwenyewe. Lakini una bahati sana kwa sasa nakuacha salama ili nikupe nafasi ya mwisho ya kukuonya na hili ni ONYO kutoka kwa Mr. X unayemtafuta kuwa USIJE KUTHUBUTU KURUDIA TENA KUTAFUTA UKWELI WOWOTE KUHUSU MR. X. Na kwa msaada alioutoa Mr. X kwako, amesema kuwa Kama utakuwa bado m'bishi na ukataka kujaribu kumtafuta tena basi amekupa zoezi dogo ambalo kama utaliweza basi utaweza Kumpata na kumjua.
Na zoezi lenyewe ni hili...... SIMAMA JUANI UKIKAMATE KIVULI CHAKO KWA MIKONO YAKO MWENYEWE. NA UKIDHIBITI KISIWEZE KUKUFATA. Ila kama utashindwa kufanya hivyo...............KUMBUKA.....BAHATI HAIJI MARA MBILI..."
Alimalizia kuongea yule Ninja ambaye alikuwa na sauti nzuri sana ya kike japo hakujifunua uso upate kuonekana lakini alionesha dhahili alikuwa ni mwanamke tena msichana kabisaaaa.
Kipindi hiko chote Kamishna Shebby alikuwa anamtazama yule Ninja muuaji na maneno yake yalizidi kumtia mwili ganzi pale chini. Alilaani na kutoamini kama kikosi kizima kimechezeshwa kindumbwe ndumbwe na mwanamke.
"Aaaagh!! Kweli nyie wanawake ni wauaji tu. Tena ni wauaji msiorudi nyuma wala kufiria hasa pale mnapopewa nafasi ama amri huitumia vizuri kwa akili zenu mbovu lakini hamfanyi mazuri. Mnapenda muonekane bora kuliko wanaume na mnajishaua tu kila afanyalo mwanaume nanyi mnaweza kufanya. Ila kumbuka kuwa wewe si wa kwanza kutumiwa na mr. X na laiti ungejua huyo anayekutuma kesho anaweza kukuua hata wewe endapo atasikia upo kwenye mazingira hatarishi na maisha ya siri yake. ha ha ha ha a a a Tatizo wanawake hamfikirii kabla ya kutenda. Ila nami nakwambia hii uliyoipata leo ni bahati kubwa sana ni bora tu uitumie vizuri. Nakuahidi ukiniacha hai lazima nije kukutafuta na utalipa damu zote zilizovuja leo wewe na Mr X. Naapa sitokuja kukuacha hai kama leo utaniacha hai na umwambie mr. X asijidanganye mwisho wake UPO na atakufa kifo kibaya na cha mateso!" Alinena kishujaa Kamishna Shebby japo kwa taabu. Lakini maneno yake ndio kwanza yaliongeza kicheko kwa yule ninja wa kike. Hapo ndipo alipomshuhudia akiitupa chini ile bunduki ya udunguaji na kuchomoa bastola ndefu na kuiload kisha kumuelekezea pale chini usawa wa paji la uso. Kamishna Shebby alisali sala zake za mwisho nafsini na kufumba macho kusubiria risasi itavyofigisa nyama zake na kuutoa uhai wake bila kupata jibu ya kile alichojitoa kukitafuta.

........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom