Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Good to See You


Nakusalimia Kapuku mheshimika, unajua kabisa salamu katika kipengele hiki ni muhimu. Yaani salamu ni muhimu hata kile kidole pendwa ambacho natumia kutaipu kinajua nini cha kufanya katika para ya kwanza. naamini umekuwa na siku nzuri na muda huu wa usiku umejituliza kutafakari nini ufanikishe kesho. Hongera na ni jambo zuri kukuona hapa.

Kuonesha fuuraha huwa sishindwi na lazima niseme kuwa karibu sana Shunie , Mndali ndanyelakakomu na shedede , nyie watu tuliwamiss hapa na zaidi aunt yangu ambaye tuna mipango mkakati wa maana sana, mkakati wa kujamiiana (soscialize) tukiwa na safari ya maisha yangu kule Kigamboni.

Muziki sasa, kwanza Bobi Wine mwanamuziki wa kule Uganda kashinda Ubunge na ni furaha sana jijini Kampala, alikuwa ni mgombea huru na bungeni kakaa na wapinzani. Sasa hapa kwetu mwaka 2005 Twanga Pepeta, magwiji hawa wa dansi chini ya Le generali na rapa mkali Diof walinogesha mwaka kwa album yao Safari.

kwa niaba ya Shunie tafadhari burudika na wimbo huu.




Binamu nikupe nini jamaaan umeufanya usiku wangu uwe mzuri sana binamu

Nakupenda sana binamu nikitaka nyimbo yoyote unaniwekea Mungu azidi kukuweka na usumbufu wangu huuu nizoee tu mie ndio nilivyo

Naipenda sana hii nyimbo binamu na hiyo band ni band bora kwangu kuliko band zozote binamu si unajua mie kizazi cha dot.com sijakutakuna na bakurutu wala vijana jazz au msondo wala sikinde
 
Nakuunga mkono kwa hili, saa nyingien huwa nawaza huyu anko nilimkosea nini jamani, kumuomba zawadi ya simu tu, ukweli alinipa. Ila sasa simu haina maua, haina chip, yaani haina vingi tu.
Binamu ukipewa zawadi usitoe lawama binamu yangu ata kama kibaya we kichekee tu na asante juu ukiwa peke yako ndio ucheke weeeeh mbavu huna kwa ulichopewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom