Makapuku Forum

Makapuku Forum

ZABURI 4

8.Katika amani nitajilaza,na kupata usingizi mara.Maana wewe,BWANA peke yako ndiwe unijaliae kukaa salama

Baba asante kwa ulinzi wako mchana kutwa,tunaomba toba kwayote tuliyokosea kwa mawazo maneno mtendo na kwa kutotimiza wajibu mbalimbali zinazotuhusu,asante kwa uzima asante kwa amani asante kwa kutupatanisha na asante kwa upendo mahali hapa,MUNGU wewe ndiye kimbilio letu na kiongozi wetu tujalie neema ya kujua dhambi zetu kukusudia kuacha,kujuta na kutubu na kuacha kabisa yale yasiyokupa utukufu,tujaze upendo wa kweli,mshikamano,uvumilivu ili tuje kuvikwa taji

Usiku huu BABA tukumbatie kama kuku anavyokumbatia vifaranga vyake,damu ya Yesu takatifu itufunike,wangalie wagonjwa,wenyechangamoto zozote,watie nguvu Mfalme wa Amani

Baba asante maana utatenda sawa na fadhili zako.

Tunaomba katika jina la Yeu Kristo Amen

SHALOM USIKU MWEMA WAPENDWA

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Nawe pia mamy
 
BABA MUNGU wa mbinguni asante kutuamsha salama tutakase ,tuongoze,tufundishe Ee Roho Mtakatifu siku ya leo ibarikiwe,tunakuomba tuepushe na mabaya yote tuepushe na dhambi za aina yoyote kwa kunena ,kutenda hata kutotimiza wajibu..tunaomba tuwe wanyenyekevu miongoni mwetu na mbele yako kila mtu akamhesabu mwenzake kuwa ni bora na muhimu katika safari hii ya Kurudi kwako BABA,Safari ambayo inahitaji mshikamano na kutiana moyo,safari ambayo inahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tusirudi nyuma katika kumtumikia Mungu wetu.

BABA tunaomba ponya wagonjwa,fariji wafiwa ,wajane na yatima watie moyo waliopondeka na kukata tamaa wale waliorudi nyuma wainuke tena na wafahamu bado unatupenda na unatusamehe na kutufutia makosa yetu kila iitwapo leo.

Wabariki watoto wetu majumbani na mashuleni wawe na hofu ya MUNGU na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.waimarishe katika masomo yao wawe vichwa na si mikia.

Ponya ndoa,ponya mahusiano,ponya familia na imarisha upendo kati yetu MAKAPUKU

Tuimarishe katika kazi zetu na mipango yetu ikafanikiwe BABA kila mmoja wetu akafaidi matunda ya kazi za mikono yake.

Asante Baba kwakuwa unatupenda na utatenda sawa na mapenzi yako.

Katika jina la Yesu naomba na kushukuru

Amen,Asante.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA

Aminaaaaa

Asantee sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom