Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jumamosi Fleva

Habari Makapuku wenzangu, ni jumamosi nyingine na kwa heshima kabisa nawakaribisha katika Jumamosi Fleva, nimepata hii idea baada ya kuona post ya Shunie na wadau wengine hata BlessedHope naye anavutiwa na fleva za kileo. kwanini nawataja hawa na kuwajuisha na wengi humu makapuku, sababu ni moja tu, jana nilipandisha wimbo wa Chidinma na ulilaikiwa na wengi, na kama mdau naamini tukiwa na hiki ki Jumamosi Fleva itakuwa poa sana.

Hapa tutakuwa tunapata miziki ya kileo zaidi, si ya zamani, miziki maarufu ya kileo. Usichoke kutoa maoni au kusema wimbo gani unapenda uwepo hapa. Wadau Bitoz anko lee empire , shululu ,Tumosa , Clkey ,Sakayo ,Nyagei mzeewakungoa , Transcend , Mondray , EMMYGUY , husna muba na wengine nilosahau kuwatag nakaribisha maoni yenu kuhusu hii Jumamosi Fleva.

Maoni yako ni muhimu na hata ukiweza unaweza kuichukua uwe unapandisha Jumamosi Fleva kila siku au utavyoona inafaa. na kama nitakuwa nayo mie basi unaruhusiwa kupendekeza muziki ukishindwa naweka ninaovutiwa nao.

na leo naanza na chagua la aunt yangu Shunie wimbo Leo toka kwa Kassim Mganga

Burudika


Asante Obe
 
...ewaaa, hapa umenipa na nguvu ya kwenda kununua unyunyu😀 na maua zidisha kuyatuma mengine atunze kwenye furiji yasinyauke. Au tuma ya kichina yale ya plastiki
Hahaha nipo Machava
Sure, haya mapenzi ya kikapukukapuku huyawezi wewe, ndiyo vizuri na hata yeye hayawezi. kwa hiyo mko sambamba
...kwani mimi ninamtafutia? Na hata kama kumtafutia si angeweka tangazo kwanza? yeye kavutiwa na wewe na kawasilisha ujumbe wake kwako
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Oh! Some emotional stuff takes time to heal, najua utakuwa sawa na hutaandika tena hicho ulichoandika na hasa kama utampata mtu jasiri wa kukutamkia kwa maandishi kuwa anakutaka kwa uwazi bila kificho kama pilau makinikia.

Yaani Mondray hataki kuwa anyone bali someone kwako, kawa wazi kama ndege za bombadier, unazijua?
Hahaha Obeeee
 
ndugu zangu..! ni imani yangu wote mna enjoy jumapili hii njema kabisa..
wachawi kaeni mbali nina upako wa mtume Paul... oooh Allelujah Bwana Yesu asifiwe utukufu kwa Bwana, sifa na utukufu ni kwake..
natamani ninene kwa lugha lakini roho mtakatifu ananiambia hapana

mbarikiwe....!!
 
0bdd6885bc5357ab0dceaa093431e740.jpg
Ni vita kati ya wanaume na wavulana
Wachile wanatandaza ubabe uwanjani.....Wajerumani wao wanatandaza soka
Itakuwa ni mechi ngumu maana walishakutana hatua ya ma kundi na kisha 1:1 ila leolazima mmoja afungwe hata kwa penati
......
hapo mjerumani atampa mtu wiki... wale majamaa awapotezi nafasi golini
 
...huhitaji kuwa na uwezo wa kuongea mbele za watu, kwani unataka kuwa mbunge?

Hapa umejieleza kwa mtu, mtu mmoja tu tena mtu maalum uliyemdondokea! Kwa kuwa demi kasema hakufai ilhali wewe unasema anakufaa basi hapa ndo ile sheria ya sumaku inapokuja, like poles repel while unlike attracts. Mngekuwa mnatakana pamoja basi kusingekuwa na maana. sasa mmoja anamtaka mwenzie na mwenzie anaona hamfai, ukisikia mapenzi ndo haya sasa, nyie ni sumaku zisizofanana hivyo huvutiana
 
ndugu zangu..! ni imani yangu wote mna enjoy jumapili hii njema kabisa..
wachawi kaeni mbali nina upako wa mtume Paul... oooh Allelujah Bwana Yesu asifiwe utukufu kwa Bwana, sifa na utukufu ni kwake..
natamani ninene kwa lugha lakini roho mtakatifu ananiambia hapana

mbarikiwe....!!

Unganeni muanzishe kanisa mtapiga hela


.....
 
  • Thanks
Reactions: Obe

Similar Discussions

Back
Top Bottom