Makapuku Forum

Makapuku Forum

Asante Obe Ubarikiwe,tutakutana kwa Maveteran kesho

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Obe... Voda wanasema :"kazi ni kwako"
Muziki: Ni Jumamosi Tulivu

Huwa hatuweki maneno Jumamosi, tunabaki kusoma ya kwenye kanga tu maana kila mmoja anakuwa ametulia nyumbani na kwa sisi tunaokaa kwenye nyumba za kupanga basi ni burudani tu, huku kunakaangwa nyama na biriani , hapa ndondo na tembele zote zikichagizwa na maneno mazuri ya kwenye kanga. Vitenge subiri mbio za mwenge ndo uvae.

Ni jumamosi wadau, nawasalimu sana na kiufupi wikend ndo inaisha hivyo. Umuhimu wako wewe kapuku hapa Jukwaani sina namna ya kuuelezea maneno yakatosheleza. Yaani ni nusu na robo jumlisha roba

Muziki sasa, leo turudi bakulutu kidogo. Nani hapendi muziki ambao ulikuwa ukipangiliwa sawia. Studio kubwa kama kiwanja cha mpira, sio studio za kileo ambazo kachumba kadogo tu kama tule tuvyumba twa pale Buguruni au Temeke basi studio inatosha kutoa muziki wa kina Diamond. Tuyaache haya usije uliza nimejuaje, hata Kigamboni si hutu tuvyumba pendwa tupo pale karibu na viwanja vya Shababi? Huwa naenda kupasha kama veteraani kwenye viwanja hivi, ondoa shaka. Ukitaka nitakupeleka, tunapasha Jumamosi asubuhi na Jpili.

Burudika na sauti-midundo mitamu ya wakongwe

 
Haya mapenzi yenu ya kikapukukapuku siyawezi mie. Mtafutie mke mwingine..

Sure, haya mapenzi ya kikapukukapuku huyawezi wewe, ndiyo vizuri na hata yeye hayawezi. kwa hiyo mko sambamba
...kwani mimi ninamtafutia? Na hata kama kumtafutia si angeweka tangazo kwanza? yeye kavutiwa na wewe na kawasilisha ujumbe wake kwako
 
Sure, haya mapenzi ya kikapukukapuku huyawezi wewe, ndiyo vizuri na hata yeye hayawezi. kwa hiyo mko sambamba
...kwani mimi ninamtafutia? Na hata kama kumtafutia si angeweka tangazo kwanza? yeye kavutiwa na wewe na kawasilisha ujumbe wake kwako
Ha haaa haya bwana! Namtakia kila la kheri apate hitaji la moyo wake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom