Makapuku Forum

Makapuku Forum

558d5eceac9adaa10b6a0c010b434226.jpg
7290cf6a4f152d457e75be3b9c243a79.jpg
a70f58b2ef8ca5570cc72fde5b9c94fd.jpg

Ni mmoja kati ya mabeki bora wa muda wote kashinda karibia kila kombe
f752fee5ec5e9d9fe372c9a2d018aa42.jpg
Ni mtoto wa kocha maarufu marehemu Cesare Madini
.....
Hakutwaa kombe la dunia.
 
fd32d34b43d5954223923a69dd1be651.jpg


TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 26.06.2017
Maduka ya kamari yameweka dau la kuashiria kuna uwezekano mkubwa wa Harry kane kuondoka Tottenham na kwenda Manchester United (Daily Star).

Hata hivyo Tottenham wametupilia mbali uwezekano wa Harry Kane kwenda Old Trafford na kusema thamani ya mshambuliaji wao ni karibu pauni milioni 200 (Independent).

Alex Sandro, 26, amekubali kujiunga na Chelsea huku mabingwa hao wa England wakikaribia kukamilisha mkataba wa pauni milioni 61 kumsajili beki huyo wa Juventus (Corriere della Sera).

Sandro huenda akaungana na Virgil van Dijk, 25, kutoka Southampton, na mshambuliaji Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton na kiungo mkabaji wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, wakati Chelsea ikijiandaa kutumia pauni milioni 240 msimu huu (Daily Express).

Arsenal na Manchester City wanafikiria kubadilishana washambuliaji, Alexis Sanchez, 28, kwa Sergio Aguero, 29 (Daily Star).

Hata hivyo Alexis Sanchgez ameshawishiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Arturo Vidal, kwa kuambiwa aachane na Arsenal na kwenda katika “klabu bora duniani” Bayern Munich (Sun).

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, amewasiliana na rais wa Lyon, kabla ya kufanikisha uhamisho wake kwenda Ufaransa msimu huu (Independent).

Dau la Everton la Pauni milioni 30, la kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, limekataliwa (Mirror).

Chelsea huenda wakapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka beki wa Roma Kostas Manola, 26, ambaye inasemekana alikuwa anakaribia kuhamia Zenith St Petersburg ya Urusi (Express).

Meneja wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson amemhakikishia mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 31, kuwa atapata ‘uzoefu mzuri’ iwapo ataamua kwenda kucheza ligi ya China (Daily Mail).

Renato Sanches, 19, anayenyatiwa na Manchester United amejiweka mbali na taarifa zinazomhusisha na kuhamia Old Trafford na kusema anatarajia kubakia Bayern Munich (Record).

Juventus watapanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares (Sun).

Mshambuliaji Kylian Mbappe, 19, atapewa ongezeko la mshahara la asilimia 900 na klabu yake ya Monaco ili kumzuia asiende Real Madrid au Arsenal au Liverpool zinazomtaka (Sun).

Rais wa Real Madrid Florentino Perez alikutana na familia ya Kylian Mbappe mapema mwezi huu (Telefoot).

Arsenal na Barcelona zinapigania kutaka kumsajili kinda wa Braga, Pedro Neto, 17, ambaye huenda akawa mchezaji wa miaka 17 aghali zaidi katika historia ya kandanda, nyuma tu ya Alexandre Pato. Tayari Braga wamekataa dau la Arsenal la pauni milioni 13.2 (A Bola).

Mshambuliaji wa AC Milan M’Baye Niang ana matumaini kuwa Arsenal watapanda dau la kumtaka, baada ya kuchelewesha uhamisho wake wa kwenda Everton (Calciomercato.com).

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Radja Nainggolan kutoka Roma (Il Tempo).

Liverpool wanamfuatilia Max Meyer, 21, anayeichezea timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21 kwenye michuano inayoendelea nchini Poland, lakini wanakabiliwa na ushindani pia kutoka Tottenham kumsajili kiungo huyo wa Schalke (Daily Star).

Crystal palace watamuulizia mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20, ambaye pia anasakwa na West ham, na Leicester (Mirror).

RB Leipzig hawana mpango wa kumuuza Naby Keita kwa bei yoyote chini ya euro milioni 80. Liverpool wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Guinea (Bild).

Liverpool wamekataa mkataba wa kubadilishana Faozi Ghoulam kutoka Napoli kwenda Anfield na Alberto Moreno kwenda Italy (Liverpool Echo).

Kiungo mchezeshaji wa Real Madrid James Rodriguez bado anataka kuhamia Manchester United baada ya kukubaliana maslahi binafsi na Old Trafford (Diario Gol).

Manchester United huenda wakamfuata winga wa Fiorentina Federico Bernardeshi iwapo watashindwa kumsajili Ivan Perisic (Football Italia).

Borussia Monchengladbach wanataka kumchukua mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen (Sunday people).

Barcelona huenda wakamgeukia kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez iwapo watashindwa kumpata Marco Verratti (AS).

Meneja mpya wa Barcelona Ernesto Valverde anataka kupiga hatua ya kushangaza ya kumtaka kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic (Don Balon).

Bournemouth wanakaribia kukamilisha mkataba wa kudumu wa pauni milioni 20 kumsajili beki wa Chelsea Nathan Ake (The Sun).

Na hatimaye….

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang alifunga magoli sita akicheza na baba yake timu moja katika mechi ya kirafiki dhidi ya maveterani wa Paris FC (tovuti ya Paris FC)
Asante kwa tetesi za Usajili.
 
Wakuu leo ni sikukuu hivyo ni vizuri tujumuike na familia zetu zaidi, wale wa kipika tulieni mpike mapochopocho,wale wa kulewa tulieni tu mlewe,wale wa viwanja nendeni tu mkajirushe

Mimi kama binadamu mpenda starehe lazima ninywe,niende kiwanja kijirusha n.k hivyo leo hata segment zangu sidhani kama zitakuwepo
Sikukuu kwanza.....mengine hata kesho yatakuwepo
Eid Mubarak wadau
.........
 
Wakuu leo ni sikukuu hivyo ni vizuri tujumuike na familia zetu zaidi, wale wa kipika tulieni mpike mapochopocho,wale wa kulewa tulieni tu mlewe,wale wa viwanja nendeni tu mkajirushe

Mimi kama binadamu mpenda starehe lazima ninywe,niende kiwanja kijirusha n.k hivyo leo hata segment zangu sidhani kama zitakuwepo
Siku kuu kwanza.....mengine hata kesho yatakuwepo
Eid Mubarak wadau
.........
Eid Mubarak
 
Wakuu leo ni sikukuu hivyo ni vizuri tujumuike na familia zetu zaidi, wale wa kipika tulieni mpike mapochopocho,wale wa kulewa tulieni tu mlewe,wale wa viwanja nendeni tu mkajirushe

Mimi kama binadamu mpenda starehe lazima ninywe,niende kiwanja kijirusha n.k hivyo leo hata segment zangu sidhani kama zitakuwepo
Siku kuu kwanza.....mengine hata kesho yatakuwepo
Eid Mubarak wadau
.........
 
Wakuu leo ni sikukuu hivyo ni vizuri tujumuike na familia zetu zaidi, wale wa kipika tulieni mpike mapochopocho,wale wa kulewa tulieni tu mlewe,wale wa viwanja nendeni tu mkajirushe

Mimi kama binadamu mpenda starehe lazima ninywe,niende kiwanja kijirusha n.k hivyo leo hata segment zangu sidhani kama zitakuwepo
Sikukuu kwanza.....mengine hata kesho yatakuwepo
Eid Mubarak wadau
.........
Same to u
 
Ngoja nipande juuu huko nitafute story sijui kivuruge wangu kaweka

Nilikua huko kumjua mwizi wa jf wa kiume anayetapeli watu jf hii jaman tuweni makini na kuzoeana na watu inasikitisha sana
 
ZABURI 20

6.Sasa najua kuwa BWANA anamwokoa masihi wake,Atajibu toka mbingu zake takatifu,Kwa matendo makuu ya wokovu Ya mkono wake,Ya mkono wake wa kuume.

7.Hawa wanataja magari na hawa farasi Bali sisi tunalitaja jina la BWANA Mungu wetu.

8.Wao wameinama na kuanguka Hali sisi tumeinuka na kusimama.

9.BWANA ,umwokoe mfalme Utuitikie siku tuitayo

BABA asante kutuamsha salama ,asante Kutupa pumzi hii tena bure ,asante kusikia maombi yetu kila iitwapo leo,tunajikbidhi kwako tena siku ya leo tuongoze,tusamehe,tuponye,tubariki ..wasaidie wote wenye changamoto mbalimbali waendelee kukutumaini wewe tu wasikate tamaa.Bariki kila mmoja mahali hapa mpe haja ya moyo wake ,ponya majeraha ya kila mmoja wetu tujifunze upendo wa kweli na kusamehe bila sababu.

Asante kwakuwa utatenda sawasawa na mapenzi yako

Jina lako libarikiwe
katika jina la Yesu Amen

SIKU NJEMA MBARIKIWE...EID NJEMA NA MAPUMZIKO MEMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom