Makapuku Forum

Makapuku Forum

fd32d34b43d5954223923a69dd1be651.jpg


TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 26.06.2017
Maduka ya kamari yameweka dau la kuashiria kuna uwezekano mkubwa wa Harry kane kuondoka Tottenham na kwenda Manchester United (Daily Star).

Hata hivyo Tottenham wametupilia mbali uwezekano wa Harry Kane kwenda Old Trafford na kusema thamani ya mshambuliaji wao ni karibu pauni milioni 200 (Independent).

Alex Sandro, 26, amekubali kujiunga na Chelsea huku mabingwa hao wa England wakikaribia kukamilisha mkataba wa pauni milioni 61 kumsajili beki huyo wa Juventus (Corriere della Sera).

Sandro huenda akaungana na Virgil van Dijk, 25, kutoka Southampton, na mshambuliaji Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton na kiungo mkabaji wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, wakati Chelsea ikijiandaa kutumia pauni milioni 240 msimu huu (Daily Express).

Arsenal na Manchester City wanafikiria kubadilishana washambuliaji, Alexis Sanchez, 28, kwa Sergio Aguero, 29 (Daily Star).

Hata hivyo Alexis Sanchgez ameshawishiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Arturo Vidal, kwa kuambiwa aachane na Arsenal na kwenda katika “klabu bora duniani” Bayern Munich (Sun).

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, amewasiliana na rais wa Lyon, kabla ya kufanikisha uhamisho wake kwenda Ufaransa msimu huu (Independent).

Dau la Everton la Pauni milioni 30, la kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, limekataliwa (Mirror).

Chelsea huenda wakapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka beki wa Roma Kostas Manola, 26, ambaye inasemekana alikuwa anakaribia kuhamia Zenith St Petersburg ya Urusi (Express).

Meneja wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson amemhakikishia mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 31, kuwa atapata ‘uzoefu mzuri’ iwapo ataamua kwenda kucheza ligi ya China (Daily Mail).

Renato Sanches, 19, anayenyatiwa na Manchester United amejiweka mbali na taarifa zinazomhusisha na kuhamia Old Trafford na kusema anatarajia kubakia Bayern Munich (Record).

Juventus watapanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares (Sun).

Mshambuliaji Kylian Mbappe, 19, atapewa ongezeko la mshahara la asilimia 900 na klabu yake ya Monaco ili kumzuia asiende Real Madrid au Arsenal au Liverpool zinazomtaka (Sun).

Rais wa Real Madrid Florentino Perez alikutana na familia ya Kylian Mbappe mapema mwezi huu (Telefoot).

Arsenal na Barcelona zinapigania kutaka kumsajili kinda wa Braga, Pedro Neto, 17, ambaye huenda akawa mchezaji wa miaka 17 aghali zaidi katika historia ya kandanda, nyuma tu ya Alexandre Pato. Tayari Braga wamekataa dau la Arsenal la pauni milioni 13.2 (A Bola).

Mshambuliaji wa AC Milan M’Baye Niang ana matumaini kuwa Arsenal watapanda dau la kumtaka, baada ya kuchelewesha uhamisho wake wa kwenda Everton (Calciomercato.com).

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Radja Nainggolan kutoka Roma (Il Tempo).

Liverpool wanamfuatilia Max Meyer, 21, anayeichezea timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21 kwenye michuano inayoendelea nchini Poland, lakini wanakabiliwa na ushindani pia kutoka Tottenham kumsajili kiungo huyo wa Schalke (Daily Star).

Crystal palace watamuulizia mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20, ambaye pia anasakwa na West ham, na Leicester (Mirror).

RB Leipzig hawana mpango wa kumuuza Naby Keita kwa bei yoyote chini ya euro milioni 80. Liverpool wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Guinea (Bild).

Liverpool wamekataa mkataba wa kubadilishana Faozi Ghoulam kutoka Napoli kwenda Anfield na Alberto Moreno kwenda Italy (Liverpool Echo).

Kiungo mchezeshaji wa Real Madrid James Rodriguez bado anataka kuhamia Manchester United baada ya kukubaliana maslahi binafsi na Old Trafford (Diario Gol).

Manchester United huenda wakamfuata winga wa Fiorentina Federico Bernardeshi iwapo watashindwa kumsajili Ivan Perisic (Football Italia).

Borussia Monchengladbach wanataka kumchukua mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen (Sunday people).

Barcelona huenda wakamgeukia kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez iwapo watashindwa kumpata Marco Verratti (AS).

Meneja mpya wa Barcelona Ernesto Valverde anataka kupiga hatua ya kushangaza ya kumtaka kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic (Don Balon).

Bournemouth wanakaribia kukamilisha mkataba wa kudumu wa pauni milioni 20 kumsajili beki wa Chelsea Nathan Ake (The Sun).

Na hatimaye….

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang alifunga magoli sita akicheza na baba yake timu moja katika mechi ya kirafiki dhidi ya maveterani wa Paris FC (tovuti ya Paris FC)
 
Hii serikali kiboko haitaki kupigwa
Kila anayewapinga kwao anakiwa adui yaani wanataka tu ndiooooooo
TLS waliitishia lakini ipo inadunda
NDO's nazo wanazotishia
Wafanyakazi wanatishiwa
Wafanyabiashara wanatishiwa
Wanasiasa wanatishiwa
Wasanii wanatishiwa

Sasa sijui wakati wa Uchaguzi watapogiwa kura na mbuzi? au wanategemea wakulima wasio na elimu wala kujua yanayoendelea nchini
.
.
.
Ahsante kwa magazeti
Eid Mubarak
......
Hatari
 
2003 - Marc Vivien Foe anafariki Dunia.

Alikuwa ni mchezaji wa Man city na timu ya taifa ya Cameroon.
9cc3a0e2c9b0f90de3e18c8083ddc45d.jpg
9d745243fb76915735bf7e5d5860dd38.jpg
59811a14b510b4d0e5398c5f110f5655.jpg
0d59e490e85e17011bd2298a013fe7e4.jpg
Alicia katikati ya dimba la Stade de Frame wakati wa michuano ya kombe la mabara dhidi ya Colombia
9310fb0d9234e8c39f8e350940c62fef.jpg
Jezi yake # 23 imestaafishwa pale Man City
Ikumbukwe msimu wake wa mwisho alicheza katika ubora wake
.....
 
Leo katika Historia:

Segment hii leo inatimiza mwaka mmoja rasmi toka ianzishwe!
Ilianza kama utani utani, ila baada ya kupokea maoni ya wadau hapa ikawa official kila siku ipo pale nipatapo muda na hatimae leo ni mwaka mmoja.

Na hii ndio post ya kwanza ya Segment hii, angalia tarehe na mwaka.


View attachment 530852
 
Leo katika Historia:

Segment hii leo inatimiza mwaka mmoja rasmi toka ianzishwe!
Ilianza kama utani utani, ila baada ya kupokea maoni ya wadau hapa ikawa official kila siku ipo pale nipatapo muda na hatimae leo ni mwaka mmoja.

Na hii ndio post ya kwanza ya Segment hii, angalia tarehe na mwaka.


View attachment 530852
Hongera sana mkuu Mussolin5 na Mkuu Bitoz kazi yenu ni njema mbarikiwe asante kwa historia na picha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom