Ha hahhahaha, am too old for shits my dear aunt.
Huwa naamini kila mmoja anaweza kukasirika na kunikasirikia anavyotaka na ninapokuwa sioni kama nimesababisha mikasiriko hiyo., huwa sisumbuki.
Kukaa kimmya na kupuuza ni sifa kubwa ya kuwa mature na wala si uoga au ujinga. Ni kupuuza mpuuzi

Najua aunt na kwa hilo nakupa heshima sana. Naamini katika jokes kama sehemu ya kumaliza siku na kuianza siku. Unajua kabisa nakupenda na siku moja, siku moja, tutaweza kutiana machoni na pedeshee ataangusha moja moja kiutaratibu siku hiyo hakuna makinikia wala majirani zangu wahamiaji haramu.
Utamkaribisha na BH basi😉

AiseeBandika banduaa leo. ...
SEHEMU YA 15
Baada ya yule dogo kumaliza ndipo niliposikia kuna shahidi upande wa mshtakiwa. Hapo moyo ulipata faraja kidogo mara baada ya kumuona ba'mkubwa akisogea kizimbani. Nilimtazama kwa jicho la kushukuru kwani nilijua yeye ndiye tumaini pekee lililobaki. Alipanda ba mkubwa na kupewa kitabu tukufu cha msahafu akala kiapo cha kusema kweli. Hapo ndipo alipopewa nafasi ya kuzungumza. Maneno yaliyosafirishwa kwa sauti yake ba'mkubwa yalipenya vizuri masikioni mwangu na kuingia katika milango yangu ya fahamu kabla hayajaenda kutua kwenye moyo wangu na kuufanya ustuke kupita maelezo huku nikijihisi viungo vyangu vyote vimeshindwa kufanya kazi hadi macho yalishindwa kupepesa na kubaki yameganda kwa ba'mkubwa kwa kutoamini kama ndie yeye au..?!
Naukumbuka vizuri ushahidi alioutoa ba'mkubwa baada ya kula kiapo. Muendeesha mashtaka alisimama na kumuuliza.
"Unamtambua vipi mtuhumiwa na una mahusiano gani naye?"
"Ndio namtambua bwana Hussein Muhondogwa ni mwanangu mtoto wa marehemu mdogo wangu wa tumbo moja."
"Sawa, kumbe Hussein ni mwanao kwa namna moja je unajua nini kuhusu tukio alilofanya la mauaji? Hebu ifafanulie mahakama kile ukijuacho?"
"Nipo hapa kwa ajili ya kutoa ushahidi kwa kile ninachokijua kuhusiana na tukio zima na kesi inayomkabili mwanangu." Aliongea ba mkubwa maneno ambayo yalinijenga moyo. Niliamini amekuja kunitetea na kuongea ukweli kama alivyoniahidi. Lakini baada ya hakimu kumuashiria aongee kile alichokijua ndipo nilipostaajabishwa na maneno ya ba'mkubwa na kunifanya niachame kinywa kwa fadhaa.
"Muheshimiwa hakimu nakumbuka miezi miwili kabla ya tukio mwanangu Hussein alikuja katika kijiwe changu cha kazi. Mimi ni mtaalamu wa tiba asilia na ofisi yangu ipo Kibamba. Alipokuja mwanangu alionesha hali ya kuchanganyikiwa kidogo hata nikamuuliza kulikoni? Lakini hakunambia ukweli zaidi ya kulalama amechoshwa na ugumu wa maisha. Baada ya maongezi ya hapa na pale aliniuliza katika dawa zangu hivi sina dawa ya kumfanya mtu awe tajiri? Hapo nilicheka na kumwambia mwanangu kuwa hutajiri hauletwi kwa dawa bali ni juhudi tu binafsi katika kazi bila kusahau kumuomba Mungu. Aliondoka siku hiyo lakini miezi miwili baadae, wiki moja kabla ya tukio. Nilipigiwa simu na mkwe wangu marehemu mkewe na akanambia kuwa wana ugomvi baina yao kuhusu mtoto. Nilipouliza zaidi kulikoni ndipo mkewe alinambia kuwa kutokana na kuchoshwa na ugumu wa maisha mumewe alienda kwa mganga mmoja ambaye hakunitajia ni wapi na anaitwa nani, lakini alichosema ni kuwa alienda kwa lengo la kupata dawa ya kuweza kuwa tajiri ili wajikwamue na maisha magumu waliyokuwa nayo. Sasa huyo mganga wake alimwambia masharti ya dawa hiyo ili itengenezwe inapaswa amtoe kafara mamaake mzazi au mtoto wake mwenyewe na apeleke kiganja chake cha mkono, ndipo atafanyiwa hiyo tiba na kuwa tajiri mkubwa. Hivyo kwa kuwa mamaye alishafariki lakini mtoto anaye, ndipo alipomfikishia mkewe habari zile na kumshauri wamtoe tu kafara mtoto wao ili watajirike na baadae watazaa wengine. Lakini mkewe alimkatalia na ndipo ugomvi ukaanzia pale. Baada ya kuambiwa ukweli na mkwe wangu ndipo kwa busara zangu niliwaambia waje wote kwangu lakini hawakuja. Ikawa kila siku napiga simu kuwahimiza na hata siku moja kabla ya tukio mapema nilipiga simu ambapo nikasikia ugomvi mkubwa baada ya simu kupokelewa. Baadae ndipo alipoanza kuongea mkewe ambapo niliwaomba waje kwangu haraka huku nia na madhumuni nimuonye mwanangu Hussein kwa kile anachotaka kukifanya. Nilikumbuka hata safari ile alipokuja nilimsikia kwa masikio yangu na kwa bahati nzuri nilimrekodi.
Lakini siku ya tukio walipokuwa wanakuja kwangu ndipo alipombadilikia mkewe walipofika sehemu ambayo aliamini hawaonekani na kufanya kilichotokea. Ki ukweli muheshimiwa hakimu mbele ya mahakama hii tukufu sina budi kuusema ukweli huu japokuwa Hussein ni mwanangu lakini kuongopa kwa ajili ya kutetea uovu nitakuwa nimejiekea mzigo wa dhambi mbele za Mungu. Nina ushahidi wa sauti katika simu niliyopiga siku hiyo napenda kuuwasilisha mbele ya mahakama. Ila pia naiomba mahakama imsamehe tu mwanangu aliyeponzwa na tamaa. Aaaaa mwanangu uuuuwww."
Alimalizia maneno yake kwa kilio bila haya ba'mkubwa alinikandamiza zaidi. Muendeesha mashtaka na wakili upande wa serikali aliichukua ile simu yenye rekodi ya sauti na ui'play'. Mahakama ilibaki tuli na kweli sauti zilisikika za ugomvi wa mwanaume na mwanamke wakigombania kumuua mtoto wao. Nilizidi kustaajabu na kufadhaika kwani sauti ya mwanamke kweli ilikuwa ni ya Zai wangu na pia sauti ya mwanaume ilifanana kabisa na yangu japo kiukweli hatukuwahi hata siku moja kuzozana na Zai. Lakini daaah!!! Mchezo niliofanyiwa pale ulinichosha sana na kuamini kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Ina maana hawa watu waliikopi hadi sauti yangu na kuiigizia?
Imekuaje ba mkubwa naye ameshirikiana nao kuniangamiza ilihali awali aliapa kunisaidia?
Nilimtazama kwa hasira ba'mkubwa alipomalizia kunipigilia msumali wa moto kwenye utosi. Sikuwa na cha kupoteza zaidi ya kukubali kuwa sina jipya hata nikitolewa kuwa huru sitokuwa na manufaa yoyote ulimwenguni. Nilimpa ushindi huyo Mr X ambaye sikuweza kung'amua mpaka leo alikuwa nani. Nilikaa tayari kuisikiliza hukumu yangu ya kifo ili nami nikapumzike kwenye ulimwengu ambao sikuwa na uhakika kama upo ama laa.
Lakini nilishangaa sikuhukumiwa siku hiyo na badala yake hakimu aliisogeza kesi tena kwa kutakiwa nikafanyiwe vipimo vya ubongo kama sikuwa na tatizo lolote la kiakili. Kwa mujibu wa serikali na katiba kwa ujumla haikuamini uchawi wala imani za kishirikina. Nililirudishwa tena segerea baada ya kuchukuliwa vipimo na tukaisubiria tarehe tajwa kusikia majibu ya daktari.
Mwezi mmoja baadae ndipo niliporudishwa tena kizimbani ambapo daktari alisimama na kuthibitisha kile alichokiona kitaalamu. Aliiambia mahakama kuwa sikuwa na tatizo lolote la ubongo linaloweza kuharibu akili zangu. Kwa hiyo vipimo vya kichwa vilionesha niko safi kabisa. Na hapo ndipo hakimu aliponigeukia na kuniuliza kama nina lolote la kujitetea..?
Nilimuangalia hakimu yule ambaye safari hii hakuwa yule mama. Taarifa za hakimu yule wa kike nilikuja kuzipata nikiwa gerezani baadae kuwa kumbe wiki moja kabla ya kesi alipatwa ajali mbaya iliyomfanya alazwe wiki nzima mahututi na siku chache baada ya hukumu yangu naye alifariki.
Nakumbuka siku hiyo kabla ya hukumu kutoka pindi nilipopewa nafasi ya kujitetea mwenyewe, nilimtazama hakimu na kusema.
"Ndugu Hakimu, mimi ni mkosaji niliyepoteza nafsi za watu wasio hatia. Sina chochote cha kujitetea kwa kuwa tayari nipo mikononi mwa sheria. Naiomba mahakama hii tukufu inihukumu kama nilivyoihukumu familia yangu kwa mujibu wa sheria ya nchi ili iwe fundisho kwa wengine. Naiweka nafsi yangu mikononi mwa mahakama hii tukufu niko tayari kuhukumiwa."
Maneno yangu yalimshangaza kila mtu aliyekuwa pale mahakamani. Hata hakimu mwenyewe aliniangalia vizuri kwa umakini na kuupisha ukimya kama wa dakika tano ndipo aliposoma hukumu yangu.
||........|.........||
"Bwana Hussein Muhondogwa. Baada ya mahakama hii tukufu kufanya uchunguzi yakinifu kwa kuzingatia sheria na taarifa za mashahidi mbalimbali sambamba na vipimo vya madaktari juu ya tukio lililotokea. Mahakama inakutia hatiani moja kwa moja bwana Hussein Muhondogwa kwa kosa la mauaji ya mke na mtoto.
Na kupitia kifungu namba 94 sheria ya mahakama iliyopitishwa mwaka 1981 kuwa endapo mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ikaonekana dhahiri aliua kwa makusudi basi hukumu yake ni kunyongwa mpaka kifo. Lakini pia kifungu hiki kilihakikiwa upya mwaka 1990 kuwa endapo mtuhumiwa huyu akakiri na kuonesha majuto mbele ya mahakama juu ya kosa lake kabla ya hukumu, basi mahakama itaangalia chaguo juu ya hukumu yake aidha ahukumiwe kifo ama ahukumiwe kifungo cha maisha jela sambamba na kazi ngumu.
Nami kupitia kifungu hiki cha mwaka 1990 nakitumia kukuhukumu bwana Hussein kutokana na majuto uliyoyaonesha mbele ya mahakama, utaenda jela kutumikia kifungo kwa maisha yako yote yaliyobaki sambamba na kazi ngumu. Na hii iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hizi.
Mwisho wa kuhukumu... Askari mchukueni kufungo chake kimeshaanza sasa."
||............|.............||
Nyundo iligongwa askari wawili walinitoa kizimbani na kunifunga pingu. Lakini hukumu ile haikuniridhisha kabisa nafsini. Nilishakinai uhai na kuutamani ufu.
"Hapanaa Hakimu umekoseaaa....Hapanaaa sistahili kuishi mimiiii? Muheshimiwa hakimu kumbuka aliyeua anapaswa auaweee. Kwanini mnaniacha nikaishi? Niueni tuuu... Niueniii tuuu hiyo sio hakiii.." Nilipiga kelele hadi askari walionichukia wakawa wananishangaa. Hakuna aliyejali kelele zangu zaidi ya kusukumwa kwenye karandinga na muda mfupi baadae safari ilianza kwenda kutumikia kifungo changu.
Lakini nikiwa nachungulia kwa nje ndipo nilishangaa kuna mtu alikuwa akilikimbilia gari lililotubeba na kulisimamisha huku mkononi mwake akiwa na barua. Askari walijaribu kumzuia lakini alilalamika huku akiinyoosha juu ile barua. Japo nilimuona lakini sikumsikia alichokuwa anaongea. Alinitibua kwa kuwa nilimtambua vizuri mwanamke yule. Alikuwa Mamu kwa mara nyengine. Sikujua alikuwa na jipya gani na kama barua ile ilinilenga mimi ni kwa nia na dhumuni gani hasa. Nilipotezea na kuzungusha shingo yangu ndani na kuinamisha kichwa chini. Sikupenda kabisa kuendelea kuuona uso wa mariam wala wa mwanamke yeyote. Karandinga lilichochea mwendo baada ya kuviacha viwanja vya mahaka na kuikanyaga barabara ya lami.
Kwa mara ya kwanza nilipewa namba ndani ya gereza na kukabidhiwa mavazi ya mfungwa kuanza maisha yangu mapya. Kazi ngumu zilizokosa malipo zikaanza kuwa sehemu ya maisha yangu. Sikutaka kuzungumza hata nilipoongeleshwa. Nilijitahidi kutafuta nafasi ya kujitoa uhai lakini niliikosa. Nilitamani kujivunja hata shingo lakini ujasiri huo ulinishinda.
Lakini baada ya wiki chache toka niingie gerezani nililetewa barua. Ilikuwa siku hiyo tukiwa tunavunja mawe, niliitwa na afisa mmoja wa magereza na kunikabidhi barua. Barua ambayo sitokuja kuisahau kwani ilinitonesha zaidi na kuniliza. Barua iliyonisukuma kula kiapo kuwa sitozungumza na yeyote kuhusu yaliyonikuta. Niliamua kuishi maisha ya ukimya na ububu ndio ukazidi kuwa jirani nami. Naikumbuka sana barua ile. Kwa mwandiko tu wa nje ya ile barua nilijua fika imetoka kwa Mariam. Japo tulishaachana muda mrefu lakini hati yake niliielewa vizuri mno. Nilikumbuka mara ya mwisho kumuona na ile siku aliyokuwa analikimbilia karandinga huku akilia na kuionesha barua. Nilijua lazima ile barua ndiyo hii iliyo mikononi mwangu sasa.
Nilitulia kwenye kivuli na kuichana bahasha na kuitoa karatasi ya barua ambayo ilikuwa imeandikwa pande zote mbili kwa wino mweusi. Aaah! Macho yalinitoka na moyo kunidunda kila niliposoma neno moja baada ya lengine aliloandika Mamu.
EndeleaSEHEMU YA 14
Daaaaaagh!!!! Ama kweli ulimi huponza kichwa. Kwa kilichonikuta sikukitarajia baada ya mwana mama hakimu kunitazama kwa hasira na kunichambulia jalada la vifungu vya sheria vilivyonifanya nipagawe mbele ya mahakama.
"Kutokana na kifungu namba 279 sheria ya mahakama iliyopitishwa na kuhakikiwa upya mwaka 1972 kuwa endapo mtuhumiwa ama mtu yeyote atatamka lugha inayoashiria matusi au dharau ndani ya mahakama, hilo ni kosa la jinai na adhabu yake ni kuchapwa viboko kumi sambamba na kifungo cha mwaka mmoja jela. Viboko vitano atachapwa siku ya kuingia jela na viboko vitano vyengine atachapwa siku ya kutoka. Na kama muhusika ni mtuhumiwa itapaswa kutorudi uraiani ila baada ya hapo atarudishwa mahakamani ndipo kesi yake husika itatajwa tena na kusikilizwa.
Nami kwa kufata kanuni na sheria hiyo naisimamisha hii kesi kwanza nakuhukumu bwana Hussein Muhondogwa kwenda jela mwaka mmoja sambamba na adhabu hizo nilizozitaja ili ukajifunze adabu na heshima utaporudi tena mahakamani uoneshe utiifu." Aligonga nyundo mezani hakimu alipomaliza kusema hayo. Nilistuka na kupiga magoti haraka.
"Naomba nisamehewe sikujua mheshimiwa hakimu wala sikusikia chochotee, aaah! Skuisonya mahakama jamaniii eeeh!" Mbali na kulalama kuomba huruma inipitie lakini hakuna kilichobadilika. Askari wakaja kunitoa pale kizimbani na kunifunga pingu. Nilimgeukia tena yule hakimu kwa uchungu nikamuangalia na yule mtu aliyeniponza. Alikuwa ni mwanamke aliyempakata mtoto mdogo. Nilimtazama kwa jicho la hasira zaidi kipindi nikitolewa msobe na polisi. Hakuwa mwengine yule mwanamke bali ni Mariamu. Mwanamke wa kwanza kumpa moyo wangu na kumthamini kabla hajanigeuka na kunisaliti tena akinikana mchana kweupe! hata kusababisha nipigwe na kuumizwa. Nilimuangalia kwa jicho baya sana Mariam. Ingawa alikuwa analia lakini machozi yake niliamini kuwa ya kinafki kwani kama kweli alikuwa ananipenda na kunihurumia mbona hakulia siku ile niliyokuwa nachezea kichapo kwa baunsa wake hadi almanusura ninyofolewe roho? Lakini ndio kwanza siku ile alivunjika mbavu kwa kicheko pale nilipotimua mbio kujiokoa. Eti leo hii anajifanya kunisikitikia na kunililia? kwa lipi hasa! yaani nipo katika mkondo wa sheria anajifanya kunililia ila nilipokuwa kwenye mkondo wa mtu aliyekuwa anajichukulia sheria mkononi alinicheka..! Ebo! kama si unafki ni nini?
Kipindi natolewa kila mwanamke niliyemuona mbele yangu nilimtazama kwa jicho baya. Niliwafasiri wanawake wote ndio wale wale. Wazuri tu machoni lakini vichwani mwao vigeugeu. Muda wowote hubadilika, wanaweza kukuchekea machoni hapohapo kukuchukia moyoni. Nikiwa nimelikaribia karandinga mara ilikuja sauti ya yule mlemavu kichwani mwangu kana kwamba ananinong'oneza.
)''Usimshangae hakimu wala yule aliyekufanya usonye kwa sababu wote ni wanawake Hussein. Wengi hawawajui walivyo lakini ni wazuri tu kwa nje ila mioyo yao mibaya sana. Japo wana sifa ya huruma lakini wanaponzwa na vichwa vyao vyenye ubongo wenye kiza ambao shetani hupendelea sana kujificha ndani yake na kuwaongoza anavyotaka. Siku zote hutoa maamuzi kwanza ndipo huyafikiria baadae. Tazama hata wanavyojidhalilisha wenyewe hawaoni wala hawafikiri! Wanatembea utupu kama wanyama hadharani.
Jivunie wewe wwanaume una ubongo mng'avu unaoweza kumulika na kuusaidia ubongo wa mwanamke na kumuongoza vizuri. Lakini kwa kuwa shetani hataki hilo na amejiekea makazi kiurahisi kichwani mwa mwanamke! Ndio sababu wengi hawataki kuongozwa na mwanaume hata wanapoolewa. Wanataka wawe sawa kwa kila kitu wakisahau kuwa hata kimaumbile hawako sawa. Hiyo yote kwa sababu ya shetani aliye vichwani mwao. Ndio maana Mungu amewataka wanawake kufunika vichwa vyao. Tazama Hussein wako wapi wale wanawake wanaowaonea aibu wanaume? Wanawake ambao ukikutana nao njiani husimama na kuchepuka! hawapo tena Hussein siku hizi wanawake wanasema wanakwenda na wakati ingawa hawawezi kwenda haja ndogo wakiwa wamesimama. Hawana haya machoni wala haiba moyoni. Wao ndio wanaongoza kuwa na wanaume wengi ingawa wanaume ndio wachache duniani. Wana mioyo ya ajabu kuweza kuzaa kwa uchungu na kuwaua watoto. Ni wauaji hawa Hussein.
Hata wanaojifanya wanapenda dini hebu ona tabia zao, tofauti kabisa na mafundisho ya hizo dini. Tazama Hussein wengine wanavyoenda makanisani wakiwa wamevaa viguo vifupi na visuruali vya kubana. Hawana haya si kwenye makanisa tu hata kwenye misikiti na madrasa huoni Hussein? Wanawake wanavaa mahijabu kama mapazia? vigauni kama vyandarua! pamoja na kanga nyepesi kama karatasi? Lakini bado ukiwaambia watakasirika. Wanataka wakivaa utupu wasifiwe. Wanataka wafanye kila wanachofanya wanaume. Lakini hapo hapo likitokea tatizo hukaa nyuma ya wanaume! Kwanini? ha ha ha haaa
Hakika mwanaume ataposhindwa kuutumia vizuri ubongo wake kwa wanawake na kujifunza jinsi ya kuishi nao basi ndio hutokea majuto mwishoni kama haya ya kwako Hussein.
Kumbuka wanawake wana nguvu ya ulimi kuliko akili. Miili yao mizuri lakini mioyo yao mibaya sana. Wanapopewa nafasi na wazifa kama wa yule hakimu hupenda kujionesha kuwa nao wanaweza kwa msukumo wa shetani na ndipo wanapoonesha makucha yao wakitaka ushindani. Amini laiti hakimu yule angekuwa mwanaume basi angekuonya na kesi ingeendea. Lakini ndio hivyo Hussein usishangae sana wala usiumie kwa sasa kwani hao ndio wanawake. Nilikwambia usiwaamini sana uwe makini nao ukapuuza....Wanawake ni wauajiii Hussein usiogope kusema haya maneno popote ili uwaokoe na wanaume wengine wasikie na waelewe wakajifunze jinsi ya kuishi nao. Hussein waambie ... waambie sasa... waambieeee kwanguvu wasikiee waambieee usiogopee .. usiogopee usiogopeeeeee.... waambiiieeeee ' '(
Sauti ilinisakama zaidi akilini. Kifua kilinijaa moyo ukanienda kasi. Maneno ya ndani fahamuni mwangu yalinipa ujasiri na kupayuka kwa nguvu pindi napandishwa kwenye karandinga na kusema.
"WANAAWAAAAKEE NI WAUAJIIIIIII"
Na hii ndio ikawa mara yangu ya kwanza kutamka maneno haya hadharani.
* * * *
Baada ya bakora tano za haja kunisurubu nilianza kukitumikia kifungo changu. Siku zilienda na muda huo wote sikuwahi kuwa na rafiki jela wala sikutaka urafiki na yeyote yule. Niliamini rafiki yangu ni mmoja tu yule aliyekuja kunitembelea na ndugu yangu ni mmoja tu nae ni ba mkubwa basi. Nilijua wengine wote wataniongopea kwa kuwa tupo katika hali moja, wakitoka kila mtu atafata yake kwa kuwa hata niliokuwa nao uraiani nao walinisapoti kwa kuwa tulikuwa katika hali moja ila leo nimepata matatizo tena ya kusingiziwa lakini wote wamenigeuka na kuniacha peke yangu. Na hapo ndipo nikaanza tabia ya kukaa peke yangu na kufanya kazi kwa nguvu muda wote. Mawazo yaliponichukua zaidi na kukumbuka yaliyonikuta ukichanganya na sauti ya yule bwana iliyokuwa inanijia kichwani mara kwa mara, ndipo nikawa nasema makusudi kuwaambia wengine kwa sauti kuwa 'Wanawake ni Wauaji'. Japo wengi waliishia kuniangalia na kudhani kuwa nimerukwa na akili lakini ukweli nilikuwa timamu.
Kwa tabu na misukosuko ya kufunzwa adabu mwishowe siku zilipita na kifungo changu kiliisha. Kabla sijatoka nilikung'utwa tena bakora zangu tano zilizobaki. Siku chache mbele baada ya kupata uwezo wa kusimama nilifikishwa tena kizimbani.
Eee.. asikwambie mtu zile bakora heri uzisikie tu kwa wenzako usiombe zikukute kwani ziko tofauti na bakora za shule nilizozizoea. Hebu fikiri bakora tano tu mtu wa mazoezi kama mimi nilishindwa kusimama. Je kama una afya mgogolo! si unaweza kukata upepo kabisa!.
Basi baada ya kufika kizimbani nilisimamishwa mbele ya hakimu yuleyule. Kesi ilianza tena kuunguruma ambapo kwa upande wa mashtaka ambao walikuwa serikali wenyewe walileta ushahidi wao zikiwemo zile nguo nilizovaa za tukio, panga na kiganja cha mtoto ambacho kilihifadhiwa muda wote. Nilipoulizwa kuhusu kuvitambua vile vitu nilikubali kuzitambua nguo tu kuwa ni kweli zilikuwa za kwangu lakini vile vyengine vyote nilikataa. Hapo ndipo alipopanda daktari aliyenichukua alama za mikono baada ya kukamatwa na kuleta majibu ambayo yalikuwa yamefanana na alama za mikono ya mtu aliyelitumia lile panga. Hali ile iliniogopesha baada ya kukumbuka ni kweli niliwahi kulishika lile panga lakini sikulitumia kudhuru chochote.
Ushahidi wote na maswali ya mawakili yalizidi kunibana. Niliumia zaidi alipopanda dogo mmoja ambae sikuwahi kumfahamu lakini ndiye alidai kupiga simu polisi.
"Hebu ithibitishie mahakama siku ya tukio ilikuwaje?" muendeesha mashtaka alimuuliza yule kijana baada ya kula kiapo cha kusema kweli.
"Ni kweli, siku ya tukio mimi nilikuwa natoka kwa rafiki yangu nikirejea kijijini. Sasa nikiwa kwa mbali nilisikia mabishano makali ya kugombania mtoto. Niliweza kujibana sehemu na kuangalia ambapo maongezi niliyosikia mwanaume akimwambia mwanamke wakamtoe tu kafara mtoto kwani watazaa mwengine, lakini mwanamke alitilia mkazo kuwa utajiri huo hakubaliani nao. Na hapo ndipo nilimshuhudia mwanaume akichomoa panga alilolisweka kwenye suruali na kuanza kumkata mkewe kichwani. Hapo ndipo nilipopiga simu polisi na kukimbilia kijijini kutoa taarifa kabla hatujaja na kumkuta mwanaume huyu mshtakiwa akiwa kashaua na ameanza kuondoka eneo la tukio." Bila aibu yule dogo alizidi kunichimbia kaburi mwenzake. Niliumia sana na kumtazama yule dogo alivyovuka mipaka kuongea kitu ambacho hakikutokea hadi akawa anatoa machozi pale mahakamani kukazia uongo wake.
Niliamini kuwa nimekwisha na nilishindwa kupiga kelele kumnyamazisha yule dogo nikihofia yasije kunikuta yale ya mwanzo. Nilimuacha anikandamize tu kwa kujua amepangwa lakini hata mwenyewe alijua kama asemacho si cha kweli. Baada ya yule dogo kumaliza ndipo niliposikia kuna shahidi upande wa mshtakiwa. Hapo moyo ulipata faraja kidogo mara baada ya kumuona ba'mkubwa akisogea kizimbani. Nilimtazama kwa jicho la kushukuru kwani nilijua yeye ndiye tumaini pekee lililobaki. Alipanda ba mkubwa na kupewa kitabu tukufu cha msahafu akala kiapo cha kusema kweli. Hapo ndipo alipopewa nafasi ya kuzungumza. Maneno yaliyosafirishwa kwa sauti yake ba'mkubwa yalipenya vizuri masikioni mwangu na kuingia katika milango yangu ya fahamu kabla hayajaenda kutua kwenye moyo wangu na kuufanya ustuke kupita maelezo huku nikijihisi viungo vyangu vyote vimeshindwa kufanya kazi hadi macho yalishindwa kupepesa na kubaki yameganda kwa ba'mkubwa kwa kutoamini kama ndie yeye au..?!
-..........
Asantee ..TumekumisEid Mubarak wapendwa
Dear shem kipenz ..usiquote simulizi unawakera wenginee plz...Aisee
Endelea
OoohDear shem kipenz ..usiquote simulizi unawakera wenginee plz...